Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu 22 Septemba 2014, Uwasilishaji wa Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, amani iwe kwenu.

Leo ni siku muhimu sana kwa historia ya nchi yetu ambapo historia mpya itaandikwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Mheshimiwa Andrew Chenge kuwasilisha Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya. Mtakumbuka kuwa Rasimu ya Kwanza na ya Pili iliwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. Hatua ya Andrew Chenge kuwasilisha Rasimu ya Tatu inakuja baada ya kazi iliyodumu kwa zaidi ya miezi minne ambapo wabunge wa Bunge Maalum la Katiba walikuwa wakijadili na kufanya marekebisho Rasimu ya Pili ambapo sasa wanatarajiwa kuja na Katiba inayopendekezwa kwa Wananchi ambayo itapigiwa kura mara baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwa vile leo ni siku muhimu sana, kama ilivyo ada yetu, tutawaletea moja kwa moja yale yanayojiri wakati wa uwasilishaji huo na tutaweka dondoo ya yale mambo muhimu yatakayowasilishwa na Chenge. Hii ni fursa muhimu ambayo hupaswi kuikosa. Kama utakosa fursa ya kupata taarifa za moja kwa moja kupitia Runinga na Radio, usijute. Kuwa nasi kupitia mtandao huu wa Jamiiforums ambako tutakuwa live.

Pamoja na wadau wengine, ungana nami kwenye tukio hili. Stay Connected.


*************************************UPDATES*********************************
* Mwenyekiti wa Bunge Maalum Sammuel Sitta anaingia ndani ya ukumbi wa bunge

*Sasa ni Azimio la kupitisha mabadiliko ya Kanuni za Bunge Maalum. Kabla ya hapo Mwenyekiti anasema kuwa Kamati ya Uandishi imeomba kuongezewa siku moja zaidi na hivyo kazi hiyo itafanyika siku ya Jumatano tarehe 24 Septemba 2014. Kutokana na hali hiyo, leo kamati hiyo haitawasilisha Rasimu kama ilivyopangwa. Anasema kuwa wabunge wanatarajia kupiga kura. Hivyo kuna haja kanuni zibadilishwe ili kuendana na muda uliopo. Anasema kuwa kwa sasa kuna wabunge 480 ambao wanawezamkuchukua dakika 960 endapo kila mbunge atapewa dakika mbili kupiga kura kwa ibara moja. Kwa hali hiyo itachukua muda wa masaa 16 kupitisha ibara moja. Ukizidisha jumla ya ibara zaidi ya 200 utaona kuwa kwa vyovyote vile hawataweza kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.

*Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Ameir Kificho anamuita mjumbe wa kamati hiyo Amon Mpanju kuwasilisha mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa. Mpanju anaanza kwa kutoa shukran kwa mwenyekiti wake kwa kumpa fursa yamkutosha ndani ya kamati hiyo bila ya kujali hali yake ya ulemavu. Kwa wale wasiomjua Amon Mpanju, ni kwamba huyu ni mlemavu wa kutoona lakini ni mtu makini sana.
*Mabadiliko yanayofanyika yanahusu kanuni za 36 hadi 39 zinazohusu upigaji kura. Amon anasema kuwa kanuni hizo zilirekebishwa zitawezesha wabunge walio nje ya ukumbi wa bunge kupiga kura popote walipo. Kuhusu kanuni ya 36, mabadiliko yanafanyika ambapo badala ya kupiga kura kwa kila ibara kwa wabunge wote, sasa wabunge watapigia kura sura husika. Amon anasema kuwa mbunhe ataeleza wakati wa kupiga kura ibara anazokubali na sile asizokubali. Hali hiyo itaokoa muda na hivyo zoezi hilo kufanyika kwa muda mfupi.

*Kuhusu haki ya kupiga kura kwa wabunge, kanuni ilivyo hivi sasa inatoa fursa ya mbunge aliye ndani ya ukumbi wa bunge pekee.mhali hii inamnyima fursa mbunge aliye nje ya ukumbi wa bunge kwa ruhusa ya mwenyekiti kupiga kura. Marekebisho yanayokusudiwa, yatawezesha wabunge walio nje ya bunge kupiga kura kwa njia ya mtandao na simu. Hivyo, Ibara ya 36 inafutwa na kuandikwa upya, pia kanuni ya 38 itaongezwa ibara ili kukidhi matakwa hayo. Anasema kuwa jedwali la marekebisho limegawiwa kwa wajumbe


************************************UPDATES********************************
*Mwalimu Oluoch anakuwa mchangiaji wa kwanza. Anasema kuwa yeye haungi mkono hoja ya wajumbe walio nje ya bunge kupiga kura. Anasema kuwa hiyo nimkinyume cha sheria. Aoaonesha wasiwasi kama wabunge wanaoenda Hija wanaweza kupata muda wa kupiga kura. Hata hivyo Mwenyekiti anamsahihisha kuwa anachoongea Oluoch ni sheria ya uchaguzi ambayo haina uhusiano na hii ya bunge maalum la Katiba. Pia anamsahihisha kuwa kanuni hiyo haijawahusu wanaoenda hija tu bali kwa wale wote watakaokuwa nje ya bunge kwa sababu mbalimbali.

*Seleman Jafu naye anachangia. Anasema kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilikuwa na mapungufu mengi. Hata hivyo anashukuru kuwa sheria hiyo imetoa fursa ya kutunga kanuni kwa kadri itakavyokuwa. Anakubaliana na mapendekezo ya kubadili kanuni badala ya kuongeza muda ambao kimsingi anasema kuwa ni kuvunja kanuni
*Paul Makonda anachangia sasa. Anashukuru Kamati ya Kanuni kwa kuleta mabadiliko hayo ambayo anayaona ni ya lazima. Anasema kuwa si rahisi wananchi wengi watu zaidi ya 600 kuwepo mahala pamoja kwa wakati mmoja. Anasema kuwa kinachofanyika si kuokoteza kura. Kura hazitawahusu wale ambao hawakushiriki kwenye mijadala. Anamshauri Oluoch kuwa ubunge hautafutwi kwa njia ya uongo bali kwa kusema ukweli. Hata hivyo Oluoch anatoa taarifa kuwa hajawahi kutangaza kuwa anataka ubunge na kwa taarifa hii anatangaza kuwa hana nia ya kugombea ubunge sehemu yoyote. Hata hivyo, Makonda anasema kuwa yeye na Oluoch wapo kwenye kamati moja na kwamba alimdokeza kuwa anataka kugombea ubunge. Hivyo kama leo Oluoch anakana, yeye anamshukuru Oluoch kwa kuwa muwazi


Aidha, Makonda anawashangaa wale wanaotishia kuandamana eti kushinikiza bunge lisiendelee. Anawashangaa vijana kutumika na wanasiasa kwa sababu zisizo na Msingi. Anamshangaa Mbowe kuchochea maandamano ilhali yeye yupo South Africa akilala kwenye Hotel yenye hadhi ya juu ambayo analipa Dola 700 kwa siku. Anasema kuwa katiba hii ina mambo mengi mazuri ambayo
hayakupiganiwa na wabunge wa upinzani ikiwa ni pamoja na uwepo wa baraza la vijana, haki za wakulima, wafugaji, wavuvi nk

*Sasa ni zamu ya Said Arfi. Anasema kuwa yeye haungi mkono mabadiliko ya kanuni. Anasema kuwa haoni sababu za msingi zamkuwataka wajumbe walio nje ya bunge kupiga kura. Anasema kuwa utaratibu uliopo dunia nzima kuwa ni wabunge waliopo ndani ya bunge tu ndio wanapiga kura. Anasema kuwa hakuna hakika kuwa ni wabunge watakaopiga kura.

*Pindi Chana anachangia sasa. Kwanza anaunga mkono kwa vile utaratibu mpya wa kupiga kura utampa haki kila mbunge kupiga kura bila ya kujali mahali alipo. Pia mabadiliko hayo yanaokoa fedha nyingi ambazo zingeteketea kama kanuni ingqbaki kama ilivyo kwani ingehitaji zaidi ya siku 300 kupiga kura bila ya kujali weekend na sikukuu
 
Wadau, nipo ndani ya ukumbi wa bunge na kuna dalili zote leo Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi Andrew Chenge hatawasilisha Rasimu hiyo. Hii ni kutokana na kazi ya kuandaa rasimu hiyo kutokamilika. Tayari Mwenyekiti wa Bunge Maalum Sammuel Sitta amewasili kwenye viunga vya bunge
 
Asante! Huku pande zetu TANESCO washafanya mambo yao mida hii.
Poleni sana nyote msio na stima kwa siku ya leo. Ila kama nilivyowataarifu, kwa leo hakuna kitakachofanyika kutokana na Kamati ya Uandishi kutokamilisha kazi yake mpaka usiku wa kuamkia leo
 
Mwenyekiti wa Bunge Maalum Sammuel Sitta anaingia ndani ya ukumbi wa bunge
 
Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba ameomba dua na hv sasa anatoa taarifa kwamba rasimu ya mwisho haitawasilishwa leo kwa sababu ya ugumu wa kazi ya kuiandaa, kamati ya uandishi imeomba siku moja zaidi. leo bunge litajadili kanuni za upigaji kura.
 
Sasa ni Azimio la kupitisha mabadiliko ya Kanuni za Bunge Maalum. Kabla ya hapo Mwenyekiti anasema kuwa Kamati ya Uandishi imeomba kuongezewa siku moja zaidi na hivyo kazi hiyo itafanyika siku ya Jumatano tarehe 24 Septemba 2014. Kutokana na hali hiyo, leo kamati hiyo haitawasilisha Rasimu kama ilivyopangwa. Anasema kuwa wabunge wanatarajia kupiga kura. Hivyo kuna haja kanuni zibadilishwe ili kuendana na muda uliopo. Anasema kuwa kwa sasa kuna wabunge 480 ambao wanawezamkuchukua dakika 960 endapo kila mbunge atapewa dakika mbili kupiga kura kwa ibara moja. Kwa hali hiyo itachukua muda wa masaa 16 kupitisha ibara moja. Ukizidisha jumla ya ibara zaidi ya 200 utaona kuwa kwa vyovyote vile hawataweza kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Ameir Kificho anamuita mjumbe wa kamati hiyo Amon Mpanju kuwasilisha mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa. Mpanju anaanza kwa kutoa shukran kwa mwenyekiti wake kwa kumpa fursa yamkutosha ndani ya kamati hiyo bila ya kujali hali yake ya ulemavu. Kwa wale wasiomjua Amon Mpanju, ni kwamba huyu ni mlemavu wa kutoona lakini ni mtu makini sana.
 
Mwenyekiti SITTA amesema Kamati ya Uandishi inahitaji siku moja zaidi kukamilisha kazi hiyo, hivyo Rasimu ya Tatu ya Katiba itawasilishwa jumatano 24/09/2014
 
Sasa ni Azimio la kupitisha mabadiliko ya Kanuni za Bunge Maalum. Kabla ya hapo Mwenyekiti anasema kuwa Kamati ya Uandishi imeomba kuongezewa siku moja zaidi na hivyo kazi hiyo itafanyika siku ya Jumatano tarehe 24 Septemba 2014. Kutokana na hali hiyo, leo kamati hiyo haitawasilisha Rasimu kama ilivyopangwa. Anasema kuwa wabunge wanatarajia kupiga kura. Hivyo kuna haja kanuni zibadilishwe ili kuendana na muda uliopo. Anasema kuwa kwa sasa kuna wabunge 480 ambao wanawezamkuchukua dakika 960 endapo kila mbunge atapewa dakika mbili kupiga kura kwa ibara moja. Kwa hali hiyo itachukua muda wa masaa 16 kupitisha ibara moja. Ukizidisha jumla ya ibara zaidi ya 200 utaona kuwa kwa vyovyote vile hawataweza kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.

Ni kweli kiongozi wewe endelea kutujuza kinachoendelea
 
Mabadiliko yanayofanyika yanahusu kanuni za 36 hadi 39 zinazohusu upigaji kura. Amon anasema kuwa kanuni hizo zilirekebishwa zitawezesha wabunge walio nje ya ukumbi wa bunge kupiga kura popote walipo. Kuhusu kanuni ya 36, mabadiliko yanafanyika ambapo badala ya kupiga kura kwa kila ibara kwa wabunge wote, sasa wabunge watapigia kura sura husika. Amon anasema kuwa mbunhe ataeleza wakati wa kupiga kura ibara anazokubali na sile asizokubali. Hali hiyo itaokoa muda na hivyo zoezi hilo kufanyika kwa muda mfupi.
 
Back
Top Bottom