Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu 22 Septemba 2014, Uwasilishaji wa Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya

Chabruma, Samweli Sitta anataka kubaka Democrasia na kutengeneza kichaka cha wangunge wa UKAWA walionje ya Bunge kupiga kura za kuunga mkono bila kulazimika kuwa ndani ya ukumbi wa Bunge, hii ni hali ya hatari kwa amani ya nchi yetu. Samweli Sitta historia itamhukumu kwa kuangamiza amani ya taifa hili.

Haya mabadiliko ya kanuni ni ya kijinga kabisa kuwahi kufanywa ni lini mbunge aliye nje ya bunge anayeza kupitisha sheria au kuingie kwenye record ya kupitisha sheria yeye akiwa hayupo bungeni, kama sheria hiyo ni ya muhimu kwake kwanini asingepanga muda wa yeye kuwa bungeni?

Tumeshajua wananchi tutatoa hukumu kwa wajumbe wa UKAWA watakao tumia fursa ya mabadiliko ya hii kanuni kupitisha katiba ya CCM wakiwa nje ya Bunge, tutajua wamehongwa ila wanaona aibu kuingia kwenye ukumbi wa bunge.

Kwani wanalazimishwa na nani ukawa kutopiga kura democrasia inampa kila mmoja uhuru wa kuamu.vipi wewe unashabikia udikteta
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mimi ni mnazi wa JF.
Siwezi kuvumilia kuona watu wanatumia JF ku promote uhuni.
Ni hilo Mkuu na utaniwia radhi

Ukweli unaita unazi na unaziutaita nini mapenzi bila kuangalia ukweli ni upofu wabuge wako makini
 
ccm wanaitakia mema kweli nchi hi?hii itakua ya kwanza kushuhudia mtu akipiga kura akiwa nje ya bunge!

Maendeleo ya hali ya juu nadhani itafungua njia kwa ajili ya uchaguzi mkuu.ikishindikana magwanda msidai kwa nguvu kwani hamkushiriki utaratibu huu
 
Mkuu inadhihirisha ule utafiti unaoonesha kuwa Tz wananchi wake IQ ziko chini. You can imagine hao wabunge kama ndio sample ya watz

Unajitusi mwenyewe kwa hoja hiyo kwani nawe hujoni ni sample ya wasioelewa na kukubali ukweli
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Leo ni siku muhimu sana kwa historia ya nchi yetu ambapo historia mpya itaandikwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Mheshimiwa Andrew Chenge kuwasilisha Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya. Mtakumbuka kuwa Rasimu ya Kwanza na ya Pili iliwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. Hatua ya Andrew Chenge kuwasilisha Rasimu ya Tatu inakuja baada ya kazi iliyodumu kwa zaidi ya miezi minne ambapo wabunge wa Bunge Maalum la Katiba walikuwa wakijadili na kufanya marekebisho Rasimu ya Pili ambapo sasa wanatarajiwa kuja na Katiba inayopendekezwa kwa Wananchi ambayo itapigiwa kura mara baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwa vile leo ni siku muhimu sana, kama ilivyo ada yetu, tutawaletea moja kwa moja yale yanayojiri wakati wa uwasilishaji huo na tutaweka dondoo ya yale mambo muhimu yatakayowasilishwa na Chenge. Hii ni fursa muhimu ambayo hupaswi kuikosa. Kama utakosa fursa ya kupata taarifa za moja kwa moja kupitia Runinga na Radio, usijute. Kuwa nasi kupitia mtandao huu wa Jamiiforums ambako tutakuwa live.

Pamoja na wadau wengine, ungana nami kwenye tukio hili. Stay Connected.


*************************************UPDATES*********************************
* Mwenyekiti wa Bunge Maalum Sammuel Sitta anaingia ndani ya ukumbi wa bunge

*Sasa ni Azimio la kupitisha mabadiliko ya Kanuni za Bunge Maalum. Kabla ya hapo Mwenyekiti anasema kuwa Kamati ya Uandishi imeomba kuongezewa siku moja zaidi na hivyo kazi hiyo itafanyika siku ya Jumatano tarehe 24 Septemba 2014. Kutokana na hali hiyo, leo kamati hiyo haitawasilisha Rasimu kama ilivyopangwa. Anasema kuwa wabunge wanatarajia kupiga kura. Hivyo kuna haja kanuni zibadilishwe ili kuendana na muda uliopo. Anasema kuwa kwa sasa kuna wabunge 480 ambao wanawezamkuchukua dakika 960 endapo kila mbunge atapewa dakika mbili kupiga kura kwa ibara moja. Kwa hali hiyo itachukua muda wa masaa 16 kupitisha ibara moja. Ukizidisha jumla ya ibara zaidi ya 200 utaona kuwa kwa vyovyote vile hawataweza kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.

*Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Ameir Kificho anamuita mjumbe wa kamati hiyo Amon Mpanju kuwasilisha mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa. Mpanju anaanza kwa kutoa shukran kwa mwenyekiti wake kwa kumpa fursa yamkutosha ndani ya kamati hiyo bila ya kujali hali yake ya ulemavu. Kwa wale wasiomjua Amon Mpanju, ni kwamba huyu ni mlemavu wa kutoona lakini ni mtu makini sana.
*Mabadiliko yanayofanyika yanahusu kanuni za 36 hadi 39 zinazohusu upigaji kura. Amon anasema kuwa kanuni hizo zilirekebishwa zitawezesha wabunge walio nje ya ukumbi wa bunge kupiga kura popote walipo. Kuhusu kanuni ya 36, mabadiliko yanafanyika ambapo badala ya kupiga kura kwa kila ibara kwa wabunge wote, sasa wabunge watapigia kura sura husika. Amon anasema kuwa mbunhe ataeleza wakati wa kupiga kura ibara anazokubali na sile asizokubali. Hali hiyo itaokoa muda na hivyo zoezi hilo kufanyika kwa muda mfupi.

*Kuhusu haki ya kupiga kura kwa wabunge, kanuni ilivyo hivi sasa inatoa fursa ya mbunge aliye ndani ya ukumbi wa bunge pekee.mhali hii inamnyima fursa mbunge aliye nje ya ukumbi wa bunge kwa ruhusa ya mwenyekiti kupiga kura. Marekebisho yanayokusudiwa, yatawezesha wabunge walio nje ya bunge kupiga kura kwa njia ya mtandao na simu. Hivyo, Ibara ya 36 inafutwa na kuandikwa upya, pia kanuni ya 38 itaongezwa ibara ili kukidhi matakwa hayo. Anasema kuwa jedwali la marekebisho limegawiwa kwa wajumbe


************************************UPDATES********************************
*Mwalimu Oluoch anakuwa mchangiaji wa kwanza. Anasema kuwa yeye haungi mkono hoja ya wajumbe walio nje ya bunge kupiga kura. Anasema kuwa hiyo nimkinyume cha sheria. Aoaonesha wasiwasi kama wabunge wanaoenda Hija wanaweza kupata muda wa kupiga kura. Hata hivyo Mwenyekiti anamsahihisha kuwa anachoongea Oluoch ni sheria ya uchaguzi ambayo haina uhusiano na hii ya bunge maalum la Katiba. Pia anamsahihisha kuwa kanuni hiyo haijawahusu wanaoenda hija tu bali kwa wale wote watakaokuwa nje ya bunge kwa sababu mbalimbali.

*Seleman Jafu naye anachangia. Anasema kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilikuwa na mapungufu mengi. Hata hivyo anashukuru kuwa sheria hiyo imetoa fursa ya kutunga kanuni kwa kadri itakavyokuwa. Anakubaliana na mapendekezo ya kubadili kanuni badala ya kuongeza muda ambao kimsingi anasema kuwa ni kuvunja kanuni
*Paul Makonda anachangia sasa. Anashukuru Kamati ya Kanuni kwa kuleta mabadiliko hayo ambayo anayaona ni ya lazima. Anasema kuwa si rahisi wananchi wengi watu zaidi ya 600 kuwepo mahala pamoja kwa wakati mmoja. Anasema kuwa kinachofanyika si kuokoteza kura. Kura hazitawahusu wale ambao hawakushiriki kwenye mijadala. Anamshauri Oluoch kuwa ubunge hautafutwi kwa njia ya uongo bali kwa kusema ukweli. Hata hivyo Oluoch anatoa taarifa kuwa hajawahi kutangaza kuwa anataka ubunge na kwa taarifa hii anatangaza kuwa hana nia ya kugombea ubunge sehemu yoyote. Hata hivyo, Makonda anasema kuwa yeye na Oluoch wapo kwenye kamati moja na kwamba alimdokeza kuwa anataka kugombea ubunge. Hivyo kama leo Oluoch anakana, yeye anamshukuru Oluoch kwa kuwa muwazi


Aidha, Makonda anawashangaa wale wanaotishia kuandamana eti kushinikiza bunge lisiendelee. Anawashangaa vijana kutumika na wanasiasa kwa sababu zisizo na Msingi. Anamshangaa Mbowe kuchochea maandamano ilhali yeye yupo South Africa akilala kwenye Hotel yenye hadhi ya juu ambayo analipa Dola 700 kwa siku. Anasema kuwa katiba hii ina mambo mengi mazuri ambayo
hayakupiganiwa na wabunge wa upinzani ikiwa ni pamoja na uwepo wa baraza la vijana, haki za wakulima, wafugaji, wavuvi nk

*Sasa ni zamu ya Said Arfi. Anasema kuwa yeye haungi mkono mabadiliko ya kanuni. Anasema kuwa haoni sababu za msingi zamkuwataka wajumbe walio nje ya bunge kupiga kura. Anasema kuwa utaratibu uliopo dunia nzima kuwa ni wabunge waliopo ndani ya bunge tu ndio wanapiga kura. Anasema kuwa hakuna hakika kuwa ni wabunge watakaopiga kura.

*Pindi Chana anachangia sasa. Kwanza anaunga mkono kwa vile utaratibu mpya wa kupiga kura utampa haki kila mbunge kupiga kura bila ya kujali mahali alipo. Pia mabadiliko hayo yanaokoa fedha nyingi ambazo zingeteketea kama kanuni ingqbaki kama ilivyo kwani ingehitaji zaidi ya siku 300 kupiga kura bila ya kujali weekend na sikukuu
Tutapataje 2/3 ya kila upande wa Muungano bila kuaandaa mazingira ya kuchakachua-Hongera six hapa hata kura za wajumbe wa Ukawa tutazipata-Si swala la machine tu mwisho wa siku itaonekana namba ya Lissu ndiyo ilipiga kura.Well done six
 
Mkuu huu ni utaratibu wa kawaida sana, rejea " Roberts Rules of order , tenth edition",In brief ni kuwa, inaruhusiwa bila shaka yoyote kutumia njia ya mawasiliano kupata kura za watu wasiokuwepo kwenye mkutano maalumu li kutimiza akidi au kupitisha jambo lolote ikiwa ni lazima kufanya hivyo.

Kama hujui Kaa kimya.

Katiba Itapita, na wananchi wataipigia kura ya ndio. Utake ni hivyo usitake ni hivyo. Nenda kaandamane.
Mtu mwenye hasira kama mie natakiwa kujitoa JF-Unaandika kwa confidence utadhani dunia yote ni yako na wewe ndo unatupa uhai watanzania
 
hakuna nchi rais kuongoza kama Tanzania,yaani serekali hata wafanye ujinga gani siye twashangilia tu..
shikamoo wabongo
 
Hii imetokea leo asubuhi wakati kamati ya kanuni ikiwasilisha mabadiliko juu utaratibu wa upigiaji wa kura ikiwagusa zaidi wajumbe watakaokua nje ya BMK wakati wa upigaji kura wa rasimu ya tatu ya katiba inayopendekezwa. Waliofokewa kutokana na kutokuunga mkono mabadiliko hayo, ni Oulochi, Said Arfi na Masoud Yosuf toka Zanzibar kama kawaida wakichagizwa na vijembe kutoka kwa walio wengi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Pesa kweli mwanaharamu haya mnayofanya huku mkijua mnafanya sio ni ujinga kuonyesha ujinga uliokuwa nao ila yatawarudia tuuu mtake msitake ujinga wenu mtauonja tu
 
Mkuu huu ni utaratibu wa kawaida sana, rejea " Roberts Rules of order , tenth edition",In brief ni kuwa, inaruhusiwa bila shaka yoyote kutumia njia ya mawasiliano kupata kura za watu wasiokuwepo kwenye mkutano maalumu li kutimiza akidi au kupitisha jambo lolote ikiwa ni lazima kufanya hivyo.

Kama hujui Kaa kimya.

Katiba Itapita, na wananchi wataipigia kura ya ndio. Utake ni hivyo usitake ni hivyo. Nenda kaandamane.

Ur true colors are shining now!
 
Kuna tatizo gani kama sheria zinaruhusu.
Tatizo lipo mkuu Cybercrime, wanapoteza muda ambao unatafuna posho za walipa kodi..........kwa nini kanuni na sheria zetu zinaflactuate........tunakurupuka ua kuna kitu kinawabana............?
 
Kumbe ndo maana watafiti wanasema watz wana IQ ndogo, hii mi inaniongezea imani ktk huo utafiti
 
hakuna nchi rais kuongoza kama Tanzania,yaani serekali hata wafanye ujinga gani siye twashangilia tu..
shikamoo wabongo

umeonae kaka.kila mtu anaibuka tu nakusema nimetumwa na wananch.eti mpaka akina kigwangala,mwigulu wanataka nch,watz wanadanganyika na ki2 kidogo tu.
 
Back
Top Bottom