Yaliyojiri Agosti 4/2015 katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA Ukumbi wa Mlimani City, DSM

Molemo

Mgombea pekee aibu Laana Usaliti wenu kwa Umma wa Watanzania na wapenda mabadiliko kote ulimwenguni itakua juu yenu na mtalipwa kwa kipimo sawa sawa.

Kama unashupaa shingo litavunjika.Ukifika ufipa ku chukua fomu ukanyimwa?Au umeshamsikia Dr analalamika kwamba amenyinwa fomu?Jihisi mjinga.
 
Last edited by a moderator:
Molemo, anza kuturushia picha, Mzee lazima atinge ngwanda leo !!
 
Tunamsubiri apitishwe rais wa kwanza asiyejua katiba ya chama chake
 
WanaJF,

Leo ni tarehe 4/8/2015 siku ya Jumanne.Ni alfajiri njema kabisa ambapo Taifa litasimama wakati likishuhudia mkutano mkuu wa CHADEMA mshirika wa UKAWA utakaokuwa na kazi moja kubwa ya kumpitisha mgombea pekee wa Urais kupitia CHADEMA na UKAWA.

Jina pekee mpaka sasa lililopitishwa na vikao vya juu ni la Kamanda mpambanaji Mzee wa maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa.Jina hili ndilo litawasilishwa kwenye mkutano mkuu ili kupigiwa kura.

Waziri Mkuu huyo wa zamani anatarajiwa kutoa hotuba mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu na mbele ya Taifa.Hotuba inayotarajiwa kuwa mwongozo wa Tanzania tunayokwenda kuijenga kuanzia Oktoba.

Timu nzima ya wapashaji habari wa CHADEMA ikiongozwa na Tumaini Makene ,Molemo ,Standalone na wengine kadhaa imepiga kambi usiku kucha hapa mlimani city ili kuwaletea kila kitakachojiri.Tunatarajia vituo kadhaa vya Televisheni kama ITV,Chanel Ten,Azam TV na radio kadhaa ikiwemo Radio One kurusha matangazo haya moja kwa moja kuanzia saa 5 asubuhi..

Karibuni sana

Ukumbi wa mlimani City unavyoonekana kabla ya wajumbe kuingia:
11229406_1639934206254065_1277029923211371118_n.jpg


Nilikuwa nadhani chadema wanauchungu kweli na nchi hii lakini kwa kumpokea EL tena kwa dau la 10billin sina imani nao tena, nawahesabu kama waganga njaa wabunge wa ccm ambao wakishatishiwa kuvuliwa uanachama wanapitisha hata ujinga ilimradi matumbo yao yashibe tu. Aliyeonesha msimamo wa dhati na mwenye dhamira njema ni Dr. Slaa pekee, huyu ndiye mwenye dhamira ya kweli na ukombozi wa nchi yetu. Wengine wote njaa tu inawasumbua hamna lolote.
 
Sasa watu wamemtenga Katibu Mkuu wao unategemea chombo serious kitangaze nini!atatangaza atayetoa kitu kidogo
 
Nimesogea tayari karibu na generator manake haya maccm hayachelewi kukata umeme!
 
mkuu utofauti wa ccm na chadema mbele ya mwananchi utakuwa ni up kwa sasa?
maana chadema kwa sasa wanasema la msingi ni ikulu potelea mbali unaingiaje kama ilivyo ccm kubaki madaraka potelea mbali.
pili chadema kwa sasa wamejaa mafisadi kama walivyo ccm

Mkuu Chadema inaendeshwa na SERA zake sio Mafisadi,uliona Zitto aliondolewa na Sera za Chama bado zinaendelea ,,Chadema Chama Cha Wananchi Sio Cha Watu Wachache,,Zitto yupo wapi sasa,?? Hata Hao mafisadi usemeo wewe pia makali ya Chama yanaweza kuwakuta,,Ndio ni kweli Madaraka ndio yanahitajika maaana ukiwa na Madaraka ndio unaweza kuamua ni mfumo gani ,Hii Nchi nzuri tuende nayo ,bila Madaraka utoweza kuona Sera za Chadema. Mkuu,,Kifupi Tanzania Nchi nzuri inahitaji Mabadadiliko ..Chama Tawala kipumzishwe kwanza wengine watuonyeshe nini wanaweza nini awawezi,miaka mitano tuna haki tena ya kupiga kura na kuamua.
 
Fisadi Leo anatangazwa kuwa mgombea urais was Chadema

Fisadi ni yupi kati ya hawa:
Aliyepitisha miswada mitatu kwa siku ya ibada( jumapili kwa nguvu) ambayo nchi imejifunga mkataba wa milele? Au yule anayepigania kuwaondoa watz kwenye Lindi la umaskini wa kuchangishwa kila siku kununua madawati na kujenga maabara?


2. Chama kinacholea rushwa kuanzia kumpata mgombea hadi kwenye kampeni kikiwanunua wapigakura mmijammoja kwa elfu 2000 au 5000?

3. Chama kilichokataa mkataba( katiba ya wananchi) uliozuia vigogo kuiba bali kikashadidia katiba ya wananchi ifutwe?
 
Back
Top Bottom