YAH:Wabunge waitupia kombora NHC

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
8th July 2012

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

headline_bullet.jpg
Wasema inajikita kuwasaidia mafisadi, Waasia
headline_bullet.jpg
Mkurugenzi ang`aka, alalamikia utitiri wa kodi

Nehemia%20MchechuNHC(3).jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Nehemiah Mchechu

Wabunge wamelishukia Shirika la Nyumba (NHC) kwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha kisicholingana na uwezo wa wananchi wenye kipato cha chini kununua nyumba zake.
Wamesema bei za nyumba zinazotarajiwa kujengwa na NHC kwenye maeneo tofauti ya nchi, zinaweza kulipwa na watu wenye kipato kinachotokana na njia zisizo halali kama ufisadi na wafanyabiashara wakubwa hasa wenye asili ya Kiasia.
Hali hiyo imejitokeza jana mjini hapa kwenye warsha iliyoandaliwa na NHC kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi, Hawa Ghasia, alisema katika hali ya kawaida, gharama ya Sh. milioni 41 inayotozwa haimlengi mwananchi wa kawaida.
Alitoa mfano kuwa, alimtuma ndugu yake kwenda kuulizia nyumba katika eneo la Mchikichi jijini Dar es Salaam, ambapo aliambiwa inauzwa Sh. milioni 168 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratius Ntukumazina, alikosoa hatua ya NHC kuwatuma wataalamu wake kwenda Uturuki kujifunza namna bora ya kuboresha utekelezaji wa mradi huo.
“Kwa nini walikwenda kujifunza Uturuki nchi ambayo kipato cha wananchi wake ni kikubwa kuliko nchini,” alihoji.
Mbunge wa Urambo Magharibi, (CCM), Profesa Juma Kapuya, alihoji kama shirika hilo lina mlengo wa fikra za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kuwatumikia wananchi wa kawaida.
Alisema gharama ya nyumba za NHC zina utata ikiwa ni pamoja na zile zilizopo mkoani Dodoma penye upungufu wa miundombinu kuuzwa kwa Sh. milioni 100 wakati zilizopo Dar es Salaam zinatozwa Sh. milioni 198.
Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Rukia Kassim Mohamed, alisema shirika hilo haliwasaidii watu wa chini kwa kutoza kodi kubwa ya pango.
Alisema kodi katika nyumba za NHC ni kati ya Sh. 200,000 hadi Sh. 500,000, hafikirii kwamba wanalenga kumsaidia mtu wa chini.
“Shirika hili lipo zaidi kibiashara kuliko uzalendo, wanasema sababu kubwa hakuna maji wala umeme, gharama za nyumba hizi na VAT zinafikia hadi Sh. milioni 198, hivi kweli unamsaidia Mtanzania wa kawaida?” alihoji.
Alisema mazingira ya utozaji gharama za nyumba hizo yanakuwa rafiki wa mafisadi na raia wenye asili ya kiasia.
Mbunge wa Bukombe (Chadema), Profesa Kulikoyela Kahgi, alitaka shirika hilo kuwashirikisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na (Takukuru), katika kuhakikisha hati za nyumba ambazo ni mali ya NHC zisizoonekana, zinapatikana.
Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, alitaka fidia kwa wale wanaondolewa katika nyumba ambazo NHC imezibomoa na kujenga nyumba za ghorofa.
Alitaka NHC wapunguze faida wanayoipata ili kuwawezesha watu wenye kipato cha chini kumudu gharama za kununua nyumba zinazojengwa.
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema ramani na thamani ya nyumba za NHC, havionyeshi kutoa fursa kwa raia wa kawaida kumudu kuzinunua.
“Tumeona hapo kuna sehemu ya magari, siamini kwamba mnazungumzia kumkomboa mtu wa chini, ninawaomba NHC wawe wazi, watuambie wanawahudumia watu wa kipato cha kawaida ama lah?” alihoji.
Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, alihoji kama waliwashirikisha wapangaji katika kupanga kodi za nyumba zao.
Mbunge wa Nkenge (CCM), Assumpter Mshama, alisema hakuna mtu mwenye kipato cha kawaida ambaye anaweza kununua nyumba za NHC.
“Hamjafanya kumsaidia Mtanzania wa kawaida, mimi nilikuwa nakaa katikati ya mji, mimi peke yangu ndiye nilikuwa Mtanzania mweusi, nilikuwa nakaa na hao hao Wahindi watupu ambao tulikuwa tunalipa Sh. 100,000,” alisema.
Mbunge wa Mbulu (Chadema), Mustapha Akunaay, alisema bei kubwa ya nyumba za NHC ni matokeo ya sera na mfumo mbovu wa kodi uliopo nchini.
“Tulalamikie mfumo wa kodi zetu, tuzungumzie kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi, sisi tuzungumze na TRA na Wizara ya Fedha ili waiondoe,” alisema.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Mariam Msabaha, alihoji ni kwa nini NHC wasianze mradi huo kwa watu wa vijijini, badala ya kuwekeza mjini.
Alisema ujenzi wa nyumba za NHC unapaswa kuwaelekea wahitaji kama wazee wasiokuwa na uwezo, yatima na wajane badala ya mafisadi na raia wenye asili ya Kiasia.
Mbunge Hilda Ngoye alitaka muswada kwa ajili ya kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi wa nyumba za watu masikini.
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM), Dk. Lucy Nkya, alitaka mtindo wa watu kushikilia nyumba za shirika na baadaye kukodisha kwa watu wengine ukomeshwe.
Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Ibrahim Sanya, aliitaka NHC kwenda kujifunza nchini Morocco ambapo ghorofa moja huuzwa kwa bei pungufu ya dola za kimarekani 50,000.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM) Ally Kessy, alisema mshahara wa kima cha chini kwa watumishi wa umma ni Sh. 170,000 ambazo haziwawezeshi kumudu ununuzi wa nyumba hizo, hivyo akaihoji NHC inataka wakaishi wapi. Akijibu hoja hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Nehemiah Mchechu, alisema suala la bei ya nyumba zinazojengwa na shirika hilo wataliangalia.
Hata hivyo, alisema faida wanayoipata katika mauzo ya nyumba hizo ni kati ya asilimia 10 hadi 15.
Alisema tatizo si gharama kubwa ya nyumba hizo bali ni kipato cha Watanzania ambapo asilimia 90 wanalipwa mishahara chini ya Sh. 800,000.
“Issue (suala), ni kwamba tunamnyanyua vipi mtu huyu wa chini aweze kumudu kununua nyumba hizi,”alisema.
Alisema miongoni mwa changamoto zinazolikabili shirika hilo ni ukubwa wa kodi mbalimbali zinazotozwa hadi nyumba inapomfikia mteja.
Alitoa mfano wakati wa ujenzi NHC inatozwa kodi na ujenzi unapokamilika, serikali inatoza kodi ya nyumba, hivyo kuwa chanzo cha kupanda kwa gharama ya uuzaji.
Alitoa mfano kuwa nyumba za NHC katika eneo la Kibada zimegharimu Shilingi milioni 23, lakini kodi zinazotozwa zinasababisha bei yake kufikia Shilingi milioni 41.
Awali, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Godluck Medeye, alisema
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imeelekeza kujenga nyumba za makazi kwa wananchi ambapo NHC inatarajiwa kufanikisha azma hiyo. Alisema lengo ni kujenga nyumba 15,000 katika kipindi cha miaka mitatu.
Alisema Februari, mwaka huu, wabunge waliielekeza wizara yake kuangalia namna ya udhibiti wa sekta ndogo ya nyumba.
Alisema rasimu ya sekta ya nyumba imekamilika na kwamba wanategemea kufikisha serikalini.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, alisema wamepata ujuzi kutoka kwa Shirika la Nyumba la Uturuki ambalo limekuwa likijenga nyumba 100,000 kwa mwaka.
Aliwataka wabunge kuliunga mkono shirika hilo na wasikubali kuyumbishwa kwa mambo yasiyo na ukweli.
Alisema ifikapo Agosti mwaka huu, NHC itakuwa imeanzisha kitengo cha kushughulikia kero za wateja, kikifanya kazi hadi saa 4.00 usiku.
Imeandaliwa na Sharon Sauwa, Mashaka Mgeta na Jacqueline Massano, Dodoma

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  • Thanks
Reactions: PPM
wabunge wa ccm tangu lini wakatetea wananchi?ni kuwa hawajapata deal mle ndani ya nhc ndio maana wanaumia weka pesa nunua nyumba sio weka card ya ccm uwekewe nyumba poleni sana
8th July 2012

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

headline_bullet.jpg
Wasema inajikita kuwasaidia mafisadi, Waasia
headline_bullet.jpg
Mkurugenzi ang`aka, alalamikia utitiri wa kodi

Nehemia%20MchechuNHC(3).jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Nehemiah Mchechu

Wabunge wamelishukia Shirika la Nyumba (NHC) kwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha kisicholingana na uwezo wa wananchi wenye kipato cha chini kununua nyumba zake.
Wamesema bei za nyumba zinazotarajiwa kujengwa na NHC kwenye maeneo tofauti ya nchi, zinaweza kulipwa na watu wenye kipato kinachotokana na njia zisizo halali kama ufisadi na wafanyabiashara wakubwa hasa wenye asili ya Kiasia.
Hali hiyo imejitokeza jana mjini hapa kwenye warsha iliyoandaliwa na NHC kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi, Hawa Ghasia, alisema katika hali ya kawaida, gharama ya Sh. milioni 41 inayotozwa haimlengi mwananchi wa kawaida.
Alitoa mfano kuwa, alimtuma ndugu yake kwenda kuulizia nyumba katika eneo la Mchikichi jijini Dar es Salaam, ambapo aliambiwa inauzwa Sh. milioni 168 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratius Ntukumazina, alikosoa hatua ya NHC kuwatuma wataalamu wake kwenda Uturuki kujifunza namna bora ya kuboresha utekelezaji wa mradi huo.
"Kwa nini walikwenda kujifunza Uturuki nchi ambayo kipato cha wananchi wake ni kikubwa kuliko nchini," alihoji.
Mbunge wa Urambo Magharibi, (CCM), Profesa Juma Kapuya, alihoji kama shirika hilo lina mlengo wa fikra za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kuwatumikia wananchi wa kawaida.
Alisema gharama ya nyumba za NHC zina utata ikiwa ni pamoja na zile zilizopo mkoani Dodoma penye upungufu wa miundombinu kuuzwa kwa Sh. milioni 100 wakati zilizopo Dar es Salaam zinatozwa Sh. milioni 198.
Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Rukia Kassim Mohamed, alisema shirika hilo haliwasaidii watu wa chini kwa kutoza kodi kubwa ya pango.
Alisema kodi katika nyumba za NHC ni kati ya Sh. 200,000 hadi Sh. 500,000, hafikirii kwamba wanalenga kumsaidia mtu wa chini.
"Shirika hili lipo zaidi kibiashara kuliko uzalendo, wanasema sababu kubwa hakuna maji wala umeme, gharama za nyumba hizi na VAT zinafikia hadi Sh. milioni 198, hivi kweli unamsaidia Mtanzania wa kawaida?" alihoji.
Alisema mazingira ya utozaji gharama za nyumba hizo yanakuwa rafiki wa mafisadi na raia wenye asili ya kiasia.
Mbunge wa Bukombe (Chadema), Profesa Kulikoyela Kahgi, alitaka shirika hilo kuwashirikisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na (Takukuru), katika kuhakikisha hati za nyumba ambazo ni mali ya NHC zisizoonekana, zinapatikana.
Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, alitaka fidia kwa wale wanaondolewa katika nyumba ambazo NHC imezibomoa na kujenga nyumba za ghorofa.
Alitaka NHC wapunguze faida wanayoipata ili kuwawezesha watu wenye kipato cha chini kumudu gharama za kununua nyumba zinazojengwa.
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema ramani na thamani ya nyumba za NHC, havionyeshi kutoa fursa kwa raia wa kawaida kumudu kuzinunua.
"Tumeona hapo kuna sehemu ya magari, siamini kwamba mnazungumzia kumkomboa mtu wa chini, ninawaomba NHC wawe wazi, watuambie wanawahudumia watu wa kipato cha kawaida ama lah?" alihoji.
Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, alihoji kama waliwashirikisha wapangaji katika kupanga kodi za nyumba zao.
Mbunge wa Nkenge (CCM), Assumpter Mshama, alisema hakuna mtu mwenye kipato cha kawaida ambaye anaweza kununua nyumba za NHC.
"Hamjafanya kumsaidia Mtanzania wa kawaida, mimi nilikuwa nakaa katikati ya mji, mimi peke yangu ndiye nilikuwa Mtanzania mweusi, nilikuwa nakaa na hao hao Wahindi watupu ambao tulikuwa tunalipa Sh. 100,000," alisema.
Mbunge wa Mbulu (Chadema), Mustapha Akunaay, alisema bei kubwa ya nyumba za NHC ni matokeo ya sera na mfumo mbovu wa kodi uliopo nchini.
"Tulalamikie mfumo wa kodi zetu, tuzungumzie kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi, sisi tuzungumze na TRA na Wizara ya Fedha ili waiondoe," alisema.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Mariam Msabaha, alihoji ni kwa nini NHC wasianze mradi huo kwa watu wa vijijini, badala ya kuwekeza mjini.
Alisema ujenzi wa nyumba za NHC unapaswa kuwaelekea wahitaji kama wazee wasiokuwa na uwezo, yatima na wajane badala ya mafisadi na raia wenye asili ya Kiasia.
Mbunge Hilda Ngoye alitaka muswada kwa ajili ya kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi wa nyumba za watu masikini.
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM), Dk. Lucy Nkya, alitaka mtindo wa watu kushikilia nyumba za shirika na baadaye kukodisha kwa watu wengine ukomeshwe.
Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Ibrahim Sanya, aliitaka NHC kwenda kujifunza nchini Morocco ambapo ghorofa moja huuzwa kwa bei pungufu ya dola za kimarekani 50,000.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM) Ally Kessy, alisema mshahara wa kima cha chini kwa watumishi wa umma ni Sh. 170,000 ambazo haziwawezeshi kumudu ununuzi wa nyumba hizo, hivyo akaihoji NHC inataka wakaishi wapi. Akijibu hoja hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Nehemiah Mchechu, alisema suala la bei ya nyumba zinazojengwa na shirika hilo wataliangalia.
Hata hivyo, alisema faida wanayoipata katika mauzo ya nyumba hizo ni kati ya asilimia 10 hadi 15.
Alisema tatizo si gharama kubwa ya nyumba hizo bali ni kipato cha Watanzania ambapo asilimia 90 wanalipwa mishahara chini ya Sh. 800,000.
"Issue (suala), ni kwamba tunamnyanyua vipi mtu huyu wa chini aweze kumudu kununua nyumba hizi,"alisema.

Back
Top Bottom