Yah: Ombi la kufundisha Jangwani High School

Jamani,kama hata utaratibu tu wa KUOMBA uhamisho hujui,unaandika jf,tena mwl.wa Kiswahili,ndiyo watoto wetu huko jangwani si utawa Felisha?
 
YAH: OMBI LA KUHAMISHIWA JANGWANI HIGH SCHOOL.
Mimi ni Sadick francis Masilu,(BAED) ninaomba mamlaka zinazohusika na uhamisho na uteuzi mnipeleke nikafundishe JANGWANI HIGH SCHOOL sababu nina uzoefu wa kutosha na mbinu za kisasa za ufundishaji. Naahidi kua katika masomo yangu (History,Kiswahili) nusu ya darasa au zaidi wasipopata alama A mamlaka husika inifute kazi. Kwa sasa ninafanya kazi mkoani Tabora kama mwalimu mwajiliwa wa serikali. Sihitaji gharama za kuhamishwa sababu nina wito wa kurudisha jina la JANGWANI. nawahakikishia nitaipaisha Jangwani.

MWL SADICK F. MASILU
0652583409
Si uende kwa dada yako Ndalichangu?
 
Zipo za kutosha, natamua Jangwani ni shule.kubwa haiwezo kuaibishwa namna ile. Mimi niko commited, na kwa kujiamin kabisa ndo maana nimesema nusu ya darasa au zaidi wasipopata A kwenye masomo yangu mamlaka husika zinifute kazi kabisa na siyo kunihamisha tena. Mimi nimebobea kufundisha kwa ustadi wa hali ya juu wenye kumuhamasisha mwanafunzi kuelewa bila kutumia nguvu kubwa. Kwahiyo hapa sijifurahishi bali nimeamua kuisaidia serikali na wananchi kwa kuwafundisha kwa weredi watoto hadi wapate matokeo mazuri.
Ulichojibu sicho ulichoulizwa, na ulichoulizwa hujakijibu. Unaposema zipo za kutosha ndio ngapi hizo?
 
Hata Mimi natamani kufanya kazi sehemu iliyoboreshwa miundombinu kama hapo jangwani ila mungu ndo hupanga. Sumbawanga kusiwe pa mwisho ila shule ya dar penye kila kitu. Hata Mimi wanipe nafas nifundishe kiingereza waone mziki wangu, haiwezekani MTU aliyefaulu olevel kwa akili take halafu advance ndo akushinde. Ni uzembe usiovumilika.
 
Lete CV yako inayoambatana na matokeo ya kidato cha sita ya Necta[/QUOTE
NENDA GOOGLE SEARCH SADICK MASILU
ITAKULETEA MATOKEO YA MWAKALELI HIGH SCHOOL MWAKA 2010 ANGALIA JINA LA SADICK MASILU UTAONA MATOKEO YANGU MAANA KIPINDI HICHO MATOKEO YALIKUA YANATOKA KWA MAJINA.
 
Ulichojibu sicho ulichoulizwa, na ulichoulizwa hujakijibu. Unaposema zipo za kutosha ndio ngapi hizo?
Mamlaka zinazohusika wataona CV YANGU labda na wewe ni miongoni mwa walimu wa Jangwani waliofelisha watoto wetu. Haiwezekana mtoto afaulu vizuri akiwa O LEVEL halafu ADVANCE ASHINDWE wakati shuoe ina kika kitu miolundombinu bora. Nakuambia ndani ya mwaka mmoja tu nikiwepi Jangwani kila mwanafunzi atatamani kuja kusoma Jangwani maana itatisha kwa ufaulu wa juu
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WADAU WOTE WA ELIMU
Ndugu wanahabari wote,kwanza nimshukuru Mungu kwa uhai na afya njema aliyonijalia hadi siku ya leo.

Ndugu zangu kwanza kabisa niwapongeze wanafunzi wote wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani yao. Hongereni sana.

Ndugu zangu, jana nilijaribu tu kuelezea azma yangu ya kutaka kuirudisha SHULE YA JANGWANI KATIKA HADHI YAKE, lakina nimepokea maoni mbalimbali wengi wakinitia moyo na wengine wakinibeza kwa kua na mawazo hasi. Lakini niseme tu sikukurupuka juu ya hilo.

KWANINI NIMEAMUA KUOMBA NIPELEKWE JANGWANI HIGH SCHOOL NA NINA NINI CHA PEKEE?

Ndugu zangu, mimi ni mwalimu kwa taaluma na siyo wito. Mtu anaweza kua na wito wa ualimu lakini asiwe na maarifa ya kutimiza majukumu ipasavyo,naomba niweke wazi kua nakwenda JANGWANI HIGH SCHOOL KAMA MWALIMU MWENYE WEREDI KAMILI NINAYEJUA JINSI YA KUPUNGUZA KIWANGO CHA UJINGA NA KUONGEZA KIWANGO MAARIFA KWA WANAFUNZI.

Ndugu zangu, rekodi zangu tangu nikiwa shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu ninapenda kusoma na kujifunza njia bora za kufundishia na kujifunzia. Kilichotokea JANGWANI ndicho kinatokea kwenye shule nyingi za binafsi na serikali maana walimu wengi mbali na kutofundisha kwa weledi pia hawana utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali pamoja na majarida mbalimbali yanayohusu ulimwengu wa elimu na namna bora ya kumfundisha mwanafunzi. Mwalimu bora ni yule anayesoma vitabu mara kwa mara na tena vitabu vya waandishi mbalimbali na kujiimarisha kimaarifa.

Mwalimu bora ni yule anayewapenda wanafunzi wake kwa namna ya kuwafanya walipende somo lake na kipindi chake.

Mwalimu bora ni yule anayewatambua wanafunzi kwa majina na uwezo wao wa darasani ili aandae mbinu bora za kuwawezesha kuelewa somo lake kila mwanafunzi kulingana na uwezo wake.

Mwalimu bora ni yule anayewapatia mazoezi,majaribio na mitihani ya kutosha wanafunzi wake na kusahihisha ili kubaini ufaulu na mabadiliko ya wanafunzi kitaaluma na kujua jinsi ya kuwasaidia zaidi.

Mwalimu bora ni yule anayetoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri na kuwatia moyo wanafunz wale waliopata alama hafifu katika majaribio na mitihani.

Mwalimu bora ni yule anayefanya vikao na mazungumzo mara kwa mara na wanafunzi wake ili apokee maoni na mapendekezo yao kwa lengo la kuwasaidia zaidi.

Mwalimu bora ni yule anayebaini tabia na nidhamu ya wanafunzi wake ili aweze kuwasaidia maana nidhamu bora ndoyo inayozaa matunda bora kitaaluma.

Mwalimu bora ni yule anayewapa muda wanafunzi wake kucheza michezo mbalimbali ili aweze kuwasaidia wanafunzi kupumzisja akili na kujenga afya bora.

Mwalimu bora ni yule anayewapa miongizo mbalimbali wanafunzi wake ili iwasaidie katika masomo yao na maisha yao.

Nugu zangu, nitareje ten ILA NAOMBA NIPELEKWA JANGWANI HIGH SCHOOL NAWAHAKIKISHIA SHULE ITAUSHANGAZA ULIMWENGU KWA KUFANYA VUZURI KITAALUMA.

Na MWL SADICK F MASILU

Hii ilifaa iwe thread
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom