Xiaomi Redmi Pad: Tablet bora zaidi kwa bei ya chini ya laki tano

Reuben Challe

JF-Expert Member
Dec 10, 2021
2,761
5,039
Mwaka 2022 Xiaomi walizindua tablet ambayo inakwenda kwa jina rahisi tu "Redmi Pad" ... yaani Xiaomi Redmi Pad. Ambayo bei yake ni kama shilingi laki nne hivi za kitanzania.
Screenshot_20230105-161838.jpg

Tablet hii inakioo cha inchi 10.61 ambacho ni LCD screen, kulingana na bei yake.
Screenshot_20230105-164220.jpg
Screenshot_20230105-162007.jpg

Kioo chake kina refresh rate ya 90Hz na brightness inafikia hadi 400nits. Hili ni jambo la kufurahisha kwa tablet ya bei hii. Kuangalia muvi kwenye kioo hiki cha 90Hz ni miongoni mwa utamu unaopatikana kwenye tablet hii
Screenshot_20230105-161931.jpg

Specifications zake ni kubwa kuliko bei yake
Screenshot_20230105-163432.jpg

Betri lake ni kubwa sana 8000mAh sio utani aisee. Yaani shida ya chaji utaisikia kwa jirani tu.
Screenshot_20230105-164207.jpg
Screenshot_20230105-162120.jpg

Inasupport 18W fast charger, lakini kwenye boksi unakuta 22.5W charger, what a suprise
Screenshot_20230105-161906.jpg

Screenshot_20230105-162155.jpg

Hii tablet ni ya shilingi laki nne tu lakini ina muonekano premium sana. Apple hutumia muonekano wa aina hii kwenye tablet zake za mamilioni
Screenshot_20230105-164239.jpg
Screenshot_20230105-162028.jpg

Xiaomi Redmi Pad inafaa kabisa kwa kuchezea magemu. Shukrani zote ziende kwa MediaTek Helio G99 ambayo ni chipset kubwa sana kwa bei hii
Screenshot_20230105-164149.jpg

Pia inakuja katika matoleo ya aina tatu ambayo ni (3GB RAM 64GB ROM), (4GB RAM 128GB) na (6GB RAM 128GB)
Screenshot_20230105-162902.jpg

Redmi Pad inakuja na Android 12 na MIUI 13.1 na pia tablet hii itapata software updates za miaka miwili yaani itapata Android 14 na MIUI 15 respecively.
Software ya MIUI 13 kwenye Redmi Pad inavutia sana. Angalia muonekano wake hapo chini.
Hii ni home screen
Screenshot_20230105-162534.jpg

Hii hapa chini ni App drawer (optional)
Screenshot_20230105-162511.jpg

Hiyo hapo chini ni Mi Control Centre
Screenshot_20230105-162622.jpg

Na hii ni Notification bar
Screenshot_20230105-162646.jpg

Angalia pia hapo chini namna MIUI 13 inavyomeremeta kwenye Xiaomi Redmi Pad
Hii ni settings
Screenshot_20230105-163021.jpg

Hii ni application ya kuandaa na kutunza notes zako
Screenshot_20230105-163048.jpg

Hii ni file manager ya Xiaomi
Screenshot_20230105-163109.jpg

Hii ni feature ya Split screen
Screenshot_20230105-163213.jpg
Screenshot_20230105-163330.jpg
Screenshot_20230105-172658.jpg

Hizi ni floating windows
Screenshot_20230105-163310.jpg
Screenshot_20230105-163246.jpg

Kiufupi MIUI 13 ina styles na features nyingi sana, siwezi kuzitaja zote
Bila kusahau Xiaomi Redmi Pad inatumia stereo speakers kwa hiyo ina sauti kubwa na nzuri sana kwa kusikiliza muziki, sauti nzuri ukiwa unaangalia movie na kadhalika.
Screenshot_20230105-162340.jpg

Ingawa kamera sio kipaumbele sana kwenye tablet, lakini Xiaomi hawajaamua kuliacha suala hili nyuma. Bado wameweka kamera nzuri sana ambayo hutoipata kwenye tablet nyingine za bei hii
Screenshot_20230105-162728.jpg

Kamera ya nyuma ina 8MP na ya mbele nayo ina 8MP
Picha zinazopigwa na kamera ya nyuma ni nzuri sana katika tablet.
Screenshot_20230105-162748.jpg
Picha zake zimebalance rangi na hutoka kali zaidi kukiwa na mwanga. Inafaa kwa matumizi ya kila siku
Screenshot_20230105-162807.jpg

Kwa sasa Xiaomi Redmi Pad zinapatikana AliExpress kuanzia TSh 390,000/= hadi laki tano kulingana na storage na RAM utakayochagua
Screenshot_20230105-164417.jpg
 
Kwenye ram na rom umesema zipo za 3Gb/64gb, zipo za 4gb/128gb na mwisho 6gb kwa 128gb.

Tayari bei zitakuwa tofauti. Tupe bei ya chini, kati na juu.
 
Hakuna bei constant lakini, AliExpress sehemu nyingi bei zinacheza hivi
3GB/64GB...... Around TSh 387,000/=
4GB/128GB.....Around TSh 440,000/=
6GB/128GB.....Around TSh 520,000/=
 
Tatizo unachopata kwenye pad ndo hicho unapata kwenye simu, so umuhimu wa pad hamna
1. Experience ya mtu anayeangalia muvi kwenye tablet, si sawa na ile ya kuangalia muvi kwenye simu. Mtu kama mimi, ninapenda sana muvi na napenda kuangalia kwenye tablet kuliko hata kwenye TV. Kwangu mimi, tablet ni muhimu.
2. Magemu kama PUBG, Call of Duty, Asphalt 9, Free fire, Fortnite na mengine mengi yanakosha zaidi ukicheza kwenye tablet kuliko kwenye simu. Si unajua mkuu, wengine ni mobile gamers na hawana time na games za kwenye PC, hivyo wanapenda magemu ya kwenye simu lakini pia wanatamani nao wacheze kwenye screen kubwa, kwa hiyo tablet zikatengenezwa kwa ajili yao.
3. Pia tablet nyingi huwa hawapunji specifications hususani kwenye suala la battery. Mfano hiyo Redmi Pad ina 8000mAh, nyingine huko zina 12000mAh, hii inaonekana kabisa iliwalenga watu wanaopenda kuangalia muvi na kucheza online games kwa masaa marefu zaidi.
4. Kuna watu wanapenda kusoma vitabu mitandaoni. Kusoma vitabu kwenye simu sio funny kama kusoma kwenye tablet. Kwa hiyo tablet zilitengenezwa kwa ajili ya watu kama hao pia, wapenzi wa vitabu.
5. Kingine kuingia kwenye streaming apps kama Netflix, Disney plus, Youtube na kadhalika, inaonekana kuvutia watu wengi ukitumia tablet kwa sababu items nyingi zinaonekana kwa wakati mmoja na katika size kubwakubwa, tofauti na simu ambayo huonesha items chache katika size ndogondogo.
6. Pia kwenye mambo ya biashara za mitandaoni, bidhaa huonekana vizuri zaidi ukiziangalia kwenye tablet kuliko kwenye simu. Hata ukiingia AliExpress, eBay, na sehemu nyingine kuangalia bidhaa, experience utakayoipata kwenye tablet ni tofauti na ile utakayoipata kwenye simu.
7. Pia kuhusu kuandaa documents au notes labda, au mambo mengi ya kimasomo au ya kiofisi basi tablet ni friendly zaidi ukiachana na PC. Ukifuatilia vizuri hata waandishi wa habari hutumia tablets.
8. Features nyingi za kwenye software mfano floating windows, split screen, etc huvutia zaidi zinavyoonekana kwenye tablet kuliko zinavyoonekana kwenye simu.
9. Kwa watu wanaopenda zile apps za kuchorachora, kuandikaandika ushubwada, hii ni hususani kwa watoto au watu wenye vipaji vya kuchora, tablet ni rafiki kuliko simu. Simu ina kioo kidogo hivyo huwa hakiwatoshi kwa matumizi yao. Suala hili la kuchora mara nyingi kufanikishwa na smart pen, ambayo inakosha zaidi kuitumia kwenye tablet kuliko simu. Kwenye simu kioo kiko limited sana (in terms of size) kutumia pen.
10. Tablet pia ina advantage nyingine nyingi kuliko simu huku advantage hizo zikitokana na ukubwa wa display, betri kubwa, chipset nzuri za kuchezea magemu na kadhalika.
Tablet zilitengenezwa pia kwa ajili ya watu ambao hawakuridhika na size ya simu, waliona size ndogo ya simu haikutosheleza mahitaji yao, kwa hiyo miongoni mwa walengwa wa matumizi ya tablet pengine haupo mkuu, maana wewe simu tayari imeshatosheleza mahitaji yako.
Naweza kusema TABLETS ARE NOT FOR EVERYONE
 
Kibiashara its either laptop or smartphone, hiyo ya middle soko ni dogo sana, na ndo maana smartphone na pc zinatoka nyingi kuliko pad
 
Sawa, ila pointi kubwa zaidi ni namba 1 na namba 2
Tablet zinatoka chache kwa sababu kwa watu wengi hawachukulii kama ni compulsory kuwa na tablet, simu kwa sasa imekuwa kama ni compulsory need.. Tablet ni kama tu inakupa extra luxury ambayo huipati kwenye simu, mfano rudia kusoma hapo nilipoandika faida za tablet utaona sababu nyingi zinahusu extra-luxury ambayo huipati kwenye simu
 
1. Experience ya mtu anayeangalia muvi kwenye tablet, si sawa na ile ya kuangalia muvi kwenye simu. Mtu kama mimi, ninapenda sana muvi na napenda kuangalia kwenye tablet kuliko hata kwenye TV. Kwangu mimi, tablet ni muhimu.
2. Magemu kama PUBG, Call of Duty, Asphalt 9, Free fire, Fortnite na mengine mengi yanakosha zaidi ukicheza kwenye tablet kuliko kwenye simu. Si unajua mkuu, wengine ni mobile gamers na hawana time na games za kwenye PC, hivyo wanapenda magemu ya kwenye simu lakini pia wanatamani nao wacheze kwenye screen kubwa, kwa hiyo tablet zikatengenezwa kwa ajili yao.
3. Pia tablet nyingi huwa hawapunji specifications hususani kwenye suala la battery. Mfano hiyo Redmi Pad ina 8000mAh, nyingine huko zina 12000mAh, hii inaonekana kabisa iliwalenga watu wanaopenda kuangalia muvi na kucheza online games kwa masaa marefu zaidi.
4. Kuna watu wanapenda kusoma vitabu mitandaoni. Kusoma vitabu kwenye simu sio funny kama kusoma kwenye tablet. Kwa hiyo tablet zilitengenezwa kwa ajili ya watu kama hao pia, wapenzi wa vitabu.
5. Kingine kuingia kwenye streaming apps kama Netflix, Disney plus, Youtube na kadhalika, inaonekana kuvutia watu wengi ukitumia tablet kwa sababu items nyingi zinaonekana kwa wakati mmoja na katika size kubwakubwa, tofauti na simu ambayo huonesha items chache katika size ndogondogo.
6. Pia kwenye mambo ya biashara za mitandaoni, bidhaa huonekana vizuri zaidi ukiziangalia kwenye tablet kuliko kwenye simu. Hata ukiingia AliExpress, eBay, na sehemu nyingine kuangalia bidhaa, experience utakayoipata kwenye tablet ni tofauti na ile utakayoipata kwenye simu.
7. Pia kuhusu kuandaa documents au notes labda, au mambo mengi ya kimasomo au ya kiofisi basi tablet ni friendly zaidi ukiachana na PC. Ukifuatilia vizuri hata waandishi wa habari hutumia tablets.
8. Features nyingi za kwenye software mfano floating windows, split screen, etc huvutia zaidi zinavyoonekana kwenye tablet kuliko zinavyoonekana kwenye simu.
9. Kwa watu wanaopenda zile apps za kuchorachora, kuandikaandika ushubwada, hii ni hususani kwa watoto au watu wenye vipaji vya kuchora, tablet ni rafiki kuliko simu. Simu ina kioo kidogo hivyo huwa hakiwatoshi kwa matumizi yao. Suala hili la kuchora mara nyingi kufanikishwa na smart pen, ambayo inakosha zaidi kuitumia kwenye tablet kuliko simu. Kwenye simu kioo kiko limited sana (in terms of size) kutumia pen.
10. Tablet pia ina advantage nyingine nyingi kuliko simu huku advantage hizo zikitokana na ukubwa wa display, betri kubwa, chipset nzuri za kuchezea magemu na kadhalika.
Tablet zilitengenezwa pia kwa ajili ya watu ambao hawakuridhika na size ya simu, waliona size ndogo ya simu haikutosheleza mahitaji yao, kwa hiyo miongoni mwa walengwa wa matumizi ya tablet pengine haupo mkuu, maana wewe simu tayari imeshatosheleza mahitaji yako.
Naweza kusema TABLETS ARE NOT FOR EVERYONE
Kwenye battery huwa Smartphone zinakaa zaidi na charge sababu vioo ni vidogo havili sana charge

Issue kubwa ni kusomea hasa kama unasoma Manga/manhua/manhwa ambazo sio webtoon, unahitaji kifaa chenye inch 10 ili kudisplay karatasi ya A4 kama ilivyo.
 
Mbona hiyo tablet gsmarena wanasema bei yake ni €130?
Hiyo bei $70 ni ya wapi?
Vitu vya amazon mara kwa mara vinakuwa kwenye sale mkuu.

$75

$25

Vizia tu deals zao mara kwa mara unapata, mi nilinunua yangu $35, plus usafiri na kodi inakuja around 150-170K
 
Sawa mkuu sema deals zimeshaexpire
Lakini kuna swali lingine naomba unisaidie kujibu, hivi kati ya Xiaomi 13 Pro na Google Pixel 7 Pro, ipi ni simu nzuri? Hilo tu
 
pixel hazijawahi kuwa simu nzuri all around, ni simu ambazo zina target matumizi fulani specific kama camera na stock android, vitu vingine kama matumizi heavy kucheza games, ama kurun app nzito nzito, ukaaji chaji etc hutavipata kwenye pixel.

na hio tablet na vifaa vyote vya amazon kwa ujumla vinakua kwenye sale mara kwa mara, January haiishi hii unapata tena bei hizo hizo
 
Asante mkuu, nitaendelea kuvizia deals ila tu nasikia Amazon shipping ni bei ghali
Kwani Amazon inatumia method zipi za payments na shipping
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom