WPFD DAY 2: Mei 2, 2024, Media AI and Emerging technologies, mjadala wa JamiiForums

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,878
12,133
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa Mwaka 2024 yanafanyika Mei 1-3 Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, leo Mei 2, 2024 ni siku ya pili ya maadhimisho hayo.

photo_2024-05-02_09-32-00.jpg

Wadau watajadili mambo mbalimbali, pia kuangazia mchango wa Uandishi wa Habari na Uhuru wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabianchi Duniani.

Kauli Mbiu ya Mwaka 2024: Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi

Baadhi ya wanaotarajia kuzungumza kwa leo ni:
- Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson
- Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rose Senyamule Staki
- Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Zlatan Milisic
- Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo
- Mwakilishi wa UNESCO (Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa), Michel Toto
- Muhtasari wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Usalama wa Wanahabari,
- Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya
- Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye

Session ya JamiiForums ina heading ya Media, AI and Emerging Technologies
Session hii inakuwa moderated na Asha D Abidallah

Wazungumzaji ni
Neema Lugangira,
Nuzulaki Dausen
Harlod Sungusia

Session hii ilihudhuriwa na watu zaidi ya 100, ambapo ishirini kati yao walikuwa ni wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mzungumzaji Nuzulak Dausen
AI imekuwa ikitumika kwa muda mrefu, zaidi ya muongo mmoja uliopita, imekuwa ni sehemu ya maisha yetu. Mashine zimekuwa na uwezo mkubwa ya kutufahamu. Kabla ya chatGPT kulikuwa na ile hali ya kwenda kuangalia video youtube na kesho unakuta inakupa video sawa na zile ulizoangalia, na kuna ile unatafuta gari unakuta gari lipo kwenye kila social media page yako.

Swali lilikuwa anatumia tools gani kwenye kampuni yake ya Nukta Afrika.
Jibu ni lake: AI inatumika kwenye kila hatua ya kukusanya habari, kuanzia kukusanya habari. Ametolea mfano zamani kutaka kujua habari za barabarani tulikuwa tunatuma waandishi barabarani, lakini kwa sasa ukiwasha GPS yako unaweza kujua wapi kuna foleni nk. Hii ni kwenye kukusanya habari.

Hatua nyingine ni kwenye kuhariri, hata kwenye kutengeneza habari. Kwasasa sisi wamiliki wa vyombo vya habari ni kwenye kuchapisha habari ambapo ni Automation. Yaani saa mbili unaona habari inatoka lakini mimi niko huku naongea, hii pia ni AI.

Kwa tools inategemea na unayotaka kutumia. Tools ziko nyingi sana, unaweza jua hii kesho ukakuta imebadilika.

Mzungumzaji mwingine, Neema Lugangira
Amezungumzia athari za AI kwenye kusambaza misinformation and disiformation kwa kutumia sauti au picha za watu. Mbali na changamoto zilizopo, baadhi ya nchi amesema Neema kuwa zimeshatunga sheria kwa ajili ya AI, ikiwemo Nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani. Nchi zinazoendelea zimekuwa nyuma kwenye kutengeneza suala hilo. Neema amezungumzia suala la tech accountability ambapo amesema kwa nchi zenye sheria, kampuni hufuata sheria za nchi, lakini kwa nchi zinazoendelea kampuni hufanya wanavyojisikia.

Neema amezungumzia suala la kufuata maadili. Ametolea mfano wa chombo kumchapisha kiongozi wa kike, ambapo watu wengi huja kukoment mambo ambayo hayaendani na post bali kumbagaza kiongozi husika na wanaomiliki page husika hawafuti zile comment ambazo zinamdhalilisha mwanamke. Amesema kwa kufuta hizo coments za matusi inaonesha kuwa hata watu wa media wanawajibika.

Jambo lingine ni misinformation na disinformation ambapo kila mmoja anatamani kupeleka habari kwa haraka bila hata kufanya verification ya taarifa. Ambapo vyombo vimebaki kuomba radhi na kuendelea.

Neema ametoa wito wa kuwa na training za kiteknolojia kwa wanahabari hasa wa mikoani, ili kuimarisha habari na media Tanzania.

Mzungumzaji, Harlod Sungusia
Katika mabadiliko ya kiteknolojia ndio kunakuwa na mabadiliko ya sheria na sera. Changamoto ambazo ziko kwenye AI katika sera na Sheria ni pamoja na zifuatazo. Kwanza sera ni kile ambacho serikali imeamua kufanya au kutofanya.

1. Nature ya technolojia. Kwanza inategemea sana uwepo wa miundombinu, umeme na internet. Lakini sisi hadi sasa tunahangaika na umeme. Maendeleo ya teknolojia inaathiri maendeleo mengine yote. Hivyo tunahitaji sasa sera inayoenda kuathiri miundombinu na maeneo mengine.

2. Ufahamu, kwa walaji na wazalishaji. Hapa kuna shida kubwa, upande wa skills mfano kwa wasimamizi wa sheria hakuna wataalamu wa kuweza kushindana na wataalamu walio nje ya nchi ambao wanapingana na kile tunachokiongea. Mfano kwa sasa ujambazi upo mkubwa zaidi kwenye mtandao badala ya kuvamia benki kama ilivyokuwa zamani. 2015 nikiwa LHRC tulikamatwa na polisi ambapo walitaka vifaa vyetu lakini hawakuwa wanajua cloud ni nini.

3. Usimamizi katika upande wa kitaifa kwenye Data sovereignity. Tunasimamiaje taarifa. Baadhi ya nchi zimetaka kuwepo kwa protocal dhidi ya threats za kimtandao kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa. Suala hili linataka global efforts, kwa kuwa kuna makampuni ambayo hayapo nchini kwako lakini yanatoa huduma.

4. Kingine ni usimamizi wa data. Hii ni kwa sababu kampuni zimejiwekeza sana kwenye big data. Lakini hatuna muongozo wa kuwa na data centers za kutosha. Wengine wana data centres za kutosha, kwa tanzania data centres hazizidi tatu, ambapo inapora ile data sovereignity. Uwepo wa humanoids zinaathiri kila kitu kwa kuwa zinaenda kuchukua nafasi za watu, kwa kuwa zinatumika hata kufanya utangazaji, kwa hiyo sheria inabidi iseme Muandishi wa habari ni nani? Uwepo wa robot ambazo unaweza kuoa, na kwasasa kuna robot ambazo unaweza kuzioa kwa hiyo sheria ya ndoa ibadili tafsiri ya ndoa ni nini. Kwa kuwa sasa mtu anaweza kununua robot na akawa mkewe badala ya kutoa mahari nk.

Tukitunga sera au sheria ya AI lazima tuwe makini, Uingereza waliwahi kutunga sheria ya farasi walikuwa wakipambana na farasi mwenyewe. Hivyo hata sasa, tunahaja ya kuangalia kuhusu teknolojia, mfano kwa sasa watu wengi wanawaza kama kompyuta ni adui au sio adui.

Sera na sheria pia inabidi ione namna ya kudecolonize data.

Maangalizo kutoka kwa Nuzulack
News Room zisiruhusu habari kupelekwa kiakili mnemba bila kuwa na mtu aliyehakiki suala husika. Hii ni muhimu sana.

Pia ni muhimu kuzingatia faragha kwa kuwa nyuma ya mifumo ya AI kuna watu wanaohakiki kila kinachowekwa kwa hiyo kikiwa ni kitu cha kiuchunguzi unaweza kuta umezuiwa kabla hata ya stori yako kutoka.
 
Back
Top Bottom