SoC01 Wosia siku ya ndoa yangu kwa mwanamke nitakayemuoa

Stories of Change - 2021 Competition

emmapetertz

Member
Jul 15, 2021
12
28
WOSIA SIKU YA NDOA YANGU KWA MWANAMKE NITAKAYEMUOA

Screenshot_20210716-085203.png

Picha: www.wikipedia.com

Mwandishi: Emmanuel P. Peter Jr.
Mob/WhatsApp: +255 788000273
Email: emmapeter759@gmail.com
Instagram: emmapetertz
Source: -------NIL------

“Maisha yanaenda kwa kasi sana, siku hizi mwanamke mwenye tako anajiamini kuliko mwenye bachelor degree”, simjui ni nani alikuwa mtu wa kwanza kusema hivi lakini ninachokumbuka ni kwamba andiko hili nimeliona mara nyingi sana. Ni kweli, kwa namna moja au nyingine na mimi naunga mguu. Hakuna anayeweza kupinga kuwa katika jicho la kiimani binadamu wote ni sawa na wote ni wazuri, lakini katika kipimo cha kawaida cha kibinadamu wazuri wapo bhana. Tuende mashariki turudi magharibi, tutakachokifanya ni kufanya mazoezi ya kutembea tu, ukweli ndio huu.

Wanazuoni wengine huamini kuwa uzuri wa mtu ni kipimo cha upofu wa macho yako kwahiyo hakuna mzuri kwa wote, umuonaye mzuri wewe wengine kwao ni wa kawaida sana. Pengine, naweza kulibali hili ndio maana; weupe kwa weusi, warefu kwa wafupi na wasomi kwa wasiosoma wanaolewa kila siku. Ila katika jamii yoyote, uzuri wa mwanamke unaamuliwa na wanaume, hili liko wazi kabisa.

Najua hujanielewa, lakini nachomaanisha ni kuwa; ni wanaume tunaoamua jamii iamini kuwa, Anitha ni mzuri kuliko Aisha na Josefina haoni ndani kwa Rahma.

Ni rahisi kusikia neno “Mashallah” (likiwa na maana ya kuusifu na kuutukuza uumbaji wa Mwenyezi Mungu) likitamkwa kwenye kikundi cha masela kila apitapo mwanamke kisura au aliyefungasha vizuri. Lakini ni ngumu mno kwa wanawake kufanya hivyo anapopita gentleman mmoja mwenye muonekano murua mbele yao. Nafikiri ni kwa sababu, Uzuri wa mwanaume haupo katika sura au mwonekano, wanaume hatusifiani wala hatupendi kusifiwa uzuri wa sura.

Kwenye maisha ni kazi bure kupata vitu elfu usivyovihitaji, lakini ni faraja kubwa mno ukipata kitu kimoja tu unachokipenda.

Mke wangu?
1. Ninapokuoa wewe, haimaanishi kuwa wewe ni mzuri kuliko wanawake wote duniani. Nikisema sijawahi kuwaona wanawake wengine wazuri kama wewe, nitaudanganya umma. Amini kwamba kuna wanawake wengi wazuri pengine hata kukuzidi wewe, lakini bahati au mkosi huu umekudondokea wewe. Ijue thamani yako, ninakuoa ili uwe mke wangu sio mke wetu. Moyo wangu mdogo sana na nina wivu mno, nikigundua unanisaliti sitaweza kuvumilia, nitakuacha.

2. Ninachokiamini, moyo mmoja huwezi kupenda watu wawili au zaidi na wewe sidhani kama utaweza kumudu kutumikia mabwana wawili?! Siwezi kukufunga kamba, kukutia kufuli/nywila (password/pattern) au kukufunga CCTV kamera ili kila upitapo nikuone, ila naomba tu unihakikishie kuwa ni mwanaume mmoja tu kuanzia sasa ataona nyeti zako, atafaidi utamu wako na kuhisi joto la kumbato lako ambaye ni mimi mmeo tu.

3. Najua mimi si binadamu wa kwanza kukufahamu kwa sababu sijakutoa pangoni, ulikuwa ukiishi na watu kwahiyo naamini; una ndugu zako, una rafiki zako na wengine tangu udogoni umecheza nao na umekua nao. Hata mashuleni mpaka vyuoni umesoma na watu na wengine ni shoga zako ambao huwa mnajadiliana mambo yenu ya wanawake yanayowahusu ninyi ambayo mimi hutaniuliza.

4. Sitakuzuia kuchangamana na watu wa jinsia yoyote ile, sikuzuii kumiliki wala kutumia simu, sikuvunjii laini ya simu (sim card), sikufutii akaunti ya facebook/Instagram na mitandao mingine ya kijamii kwa sababu wewe ni binadamu uliyekamilika unahitaji furaha na uhuru wako binafsi. Lakini kero zikizidi mitandaoni, waambie kuwa umeolewa na mimi kama mumeo nitakapohitaji kujua mwenendo wako; unawasiliana na nani, rafiki zako ni akina nani kwa sababu najali, nitashika na kutumia simu yako na wewe ruksa kufanya vivyo hivyo.

5. Ninaposema nakupenda; haimaanishi kuwa hakuna kiumbe mwingine ulimwenguni ninayempenda kuliko wewe, la hasha; nina mama yangu, dada zangu na ndugu zangu wengine ambao kipimo cha upendo wangu kwao inategemea na walivyonitendea mpaka sasa. Mimi pia nimelelewa na kupewa support na watu wengi mpaka kufika hapa. Watu wote walio na mchango mkubwa maishani mwangu nawapenda mno. Neno nakupenda wewe yaani I love you lisikupofushe macho na kukulewesha akili ukakengeuka, kwa sababu mara nyingi tumeshuhudia sifa huishia kuponza.

6. Ninaposema nakuhitaji katika maisha yangu haimaanishi siwezi kuishi bila wewe. Naweza sana tu, kwa sababu wewe sio Oksijeni na nilikuwa ninaishi hata kabla ya kukufahamu. Lakini nimekuchagua wewe uwe rafiki yangu wa maisha, ndiyo tena zaidi ya rafiki kwa sababu; nitakula pamoja nawe, nitalala kitanda na kuchangia shuka na wewe. Raha na shida zangu tutazibeba wote, ninakuomba uzistahimili raha na karaha zangu, mazuri na mabaya yangu yanayoweza kuvumilika, ubora na udhaifu wangu uustiri.

7. Tukigombana si lazima jirani ajue, kwa sababu mambo kama hayo hayaepukiki na ndio maana ya ubinadamu. Tushiriki kujenga familia moja, nikileta na wewe unaleta au unatuza kilicholetwa. Ukumbuke kuwa; Mwenyezi Mungu akipenda siku moja tunaweza kuwa na watoto na watatutegemea, kwa hiyo msingi mzuri wa maisha yao unategemea uimara wa ndoa yetu.

8. Inawezekana bado au tayari ulishacheza mechi nyingi tu; za ugenini ama nyumbani, kwahiyo mazingira na maana ya ndoa unaijua sina shaka juu ya hilo. Kwangu mimi, wewe kuwa bikira au kutokuwa bikira hakuna maana yoyote, usijipe stress (msongo wa mawazo) kuwaza juu ya hilo. Ila naungana na Mugabe kukukumbusha kuwa, “Ukiwa mwanamke mzuri na hauna akili zitakazoumia ni sehemu zako za siri”. Wanaume hawataacha kukutongoza eti kisa umeolewa, watakuja tu na ukiruhusu watakugeuza uwanja wa mazoezi.

9. Mwanamke unapata wapi ujasiri wa kutembea barabarani umevaa vizuri na umesitirika halafu kumbe kuna watu zadi ya 10 mtaani wanakujua ulivyo nje ndani hata ukiwa bila nguo, unajisikiaje?!! Anyway, kwangu mimi; ufundi kitandani na majonjo wenyewe mnaita mahaba niue, ni ziada sana usihangaike nayo ingawa napenda uwe romantic. Ukinipikia, ukinifulia, ukitunza ndugu zangu, ukalea watoto wangu kwa ustadi, ukasaidia ndoto zangu kukamilika itafaa zaidi kuliko kunilisha vitu vya ajabu kutoka kwa sangoma ili nikupende.

10. Uzuri wa kudumu ni inborn, mtu anazaliwa nao: na mimi nilikupenda ulivyo since day 1 nilivyokuona; sipendi upake mikorogo, uvae mawigi, na marembo mengine mengi ya bandia kama; kucha, kope, rasta, makeup, sindano za kubusti hips na makalio. Yaani, kiufupi sipendi ujidanganye mwenyewe na udanganye watu wengine kwa vitu vya kubandika ambavyo unajua kabisa si vyako na ukibandua unarudi kama ulivyozaliwa.

11. Ridhika na ulivyoumbwa, usimkosoe Mungu kwa kujibadilisha ama kujiongezea maumbile ambayo hajakuumbia ni machukizo mbele zake na mbele zangu mumeo. Sio lazima usifiwe na wanaume wengi upitapo barabarani, nikikusifu mimi mumeo itatosha sana. Hata wasipokusifu; mvua zitaendelea kunyesha na jua halitaacha kuchomoza mashariki wala kuzama magharibi.

12. Hongera kwa majitoleo yako, asante kwa kuwa tayari kuniheshimisha nasikia mwanaume aliyeoa anaheshimiwa kuliko bachela; nipe ushirikiano tuijenge familia yetu. Naomba nisiwachoshe wasikilizaji na watazamaji katika siku yetu muhimu, nawasilisha.

Asante....
 
WOSIA SIKU YA NDOA YANGU KWA MWANAMKE NITAKAYEMUOA

View attachment 1856753

Mkuu hii kitu ni fasihi ya hali ya juu, umetuliza kichwa sema nondo zinadondokeaga kwa wauza chuma na tatizo linaanziaga hapo mtoa nondo kuwa mtaji wa muuza siso
 
Umeongea real fact kuhusu wanawake wanavyokua na negative mind kwny vichwa vyao.. But uzi wako umetujenga wote.. Hongera sanaa! Endelea kutujuza vitu vya maana kam ivii
 
Back
Top Bottom