SoC01 Wosia: Jambo la Muhimu Linalosahaulika/Kupuuzwa na Wengi

Stories of Change - 2021 Competition

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
23,779
71,315
Wosia ni kauli ya hiari inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake ikionyesha mgawanyiko wa mali/mirathi pamoja na muongozo wa familia yake baada ya kifo chake. (tafsiri ya kisheria)

Katika jamii ya Kitanzania, kumekua na mitazamo mbalimbali juu ya kuandika wosia na wenegi wamekua wakihusisha na imani potofu au mtazamo hasi kama vile kujitabiria kifo n.k.

Katika siku za karibuni tumeshuhudia wajane na watoto wa marehemu wakipoteza haki zao kwa sababu ya kufiwa na waume/baba zao pasipo kuacha wosia au andiko lolote linalotambulika kisheria linaloweza kulinda mali zao au mirathi iliyopo.

Hata hivyo kuna badhi ya familia zinaachiwa wosia lakini zemekua hazina elimu ya kutosha ya namna ya kuhifadhi wosia au mahala salama pa kuhifadhi wosia na matokeo yake wanapoteza au kupokonywa haki zao.

Baadhi ya manufaa ya kuhifadhi wosia ni pamoja na kuepusha familia kunyang’anywa mali, kuepusha mifarakano katika familia, kuepusha kesi za mirathi ambazo huchukua muda mrefu, kuepusha migogoro wakati wa kuzika au kugombania maiti.

Aina za Wosia

1. Wosia wa maandishi - Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika. Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.

Wosia wa maamdishi unapaswa kuwa na tarehe, uandikwe kwa kalamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja. (Kutoka tovuti ya RITA)

Mtoa wosia asiye jua kusoma ua kuandika awe na mashuhuda wa nne wanao jua kusoma na kuandika, mhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia, mashuhuda hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye wosia kwa wakati mmoja.

2. Wosia wa mdomo - Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda wasiopungua wanne, wawili kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia. Wosia huu hutolewa na mtu asiyejua kusoma na kuandika.

Kupata ufafanuzi zaidi rejea: Kuhusu Wosia

Mambo ya kuzingatia wakati wa kuandika wosia

• Mtoa wosia lazima awe na umri wa miaka 18 na kuendelea, awe na akili timamu.
• Wosia lazima uonyeshe tarehe, mwezi na mwaka ulioandikwa.
• Wosia lazima uonyeshe majina ya warithi, hii itasaidia kuondoa utata na malumbano dhidi ya nani atarithi nini na kwa silimia ngapi.
• Wosia lazima uandikwe kwa kalamu isiyofutika (wino) au uchapishwe na uwe na nakala.
• Mashahidi waliokuwepo wataweka saini zao kwa pamoja.
• Wosia pia ni lazima utaje mali ya mwandishi bila kuhusisha mali ya mtu mwingine.
• Wosia unapaswa kuwa siri na wanufaika hawapaswi kujua.

Iwapo mwosia anajua kuandika,Wosia ni lazime uwe na mashahidi wawili, inapobidi mmoja wapo awe ni mwana familia au mwana ukoo, iwapo mwosia hajui kusoma na kuandika, mashahidi wanne wanahitajika, wawili kati yao lazima wawe wana ukoo.

Namna ya Kuhifadhi Wosia.

Kutokana na tamaa za wanafamilia au ndugu, mara nyingi hutokea watu ambao hujipanga kudhulumu mali ya marehemu na wengine wapo tayari kughushi wosia na kudai kuwa uliandaliwa na marehemu wakati akiwa hai.

Wengine wakipata nafasi, hufanya mabadiliko katika wosia ulioachwa na marehemu. Hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kutunza wosia mahali palipo salama. Sehemu hizi zinaweza kutumika katika kutunza wosia kwakuwa ni nyaraka muhimu sana ambayo hubeba kauli ya mtu baada ya kufariki.

I. Ndugu au rafiki ambaye mwosia anamwamini.
II. Nyumba ya ibada ya mwosia.
III. Mwanasheria wa familia.
IV. Mahakama.
V. Wakala wa Usajili (RITA).
VI. Benki.

Rejea: Maeneo ya Kutunza Wosia

Mapendekezo.

Tujenge tabia ya kuandika wosia baada tu ya kufikisha umri wa miaka kumi na nane ili litakapo tokea jambo lolote (hasa kifo) tusiache sintofahamu katika familia zetu ikiwemo upotevu wa mali (mfano pesa zilizopo benki, madeni kwa watu). Pia kuepusha migogoro na mifarakano kati ya ndugu.

Elimu itolewe kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuandika wosia na namna ya kuhifadhi pamoja na mahala pakupata msaada wa kisheria pale maagizo ya wosia yanapokiukwa.

Serikali isimamie na kuthiniti gharama zinazotozwa katika kuhifadhi wosia kwenye mabenki au mahakamani ili kuwezesha wananchi kuhifadhi wosia mahali salama.

Serikali iangalie namna ya kuendesha kesi za mirathi kwa muda mfupi ili kuepuka usumbufu wanaoupata familia ya marehemu baada ya kufiwa.

Angalia videos ujifunze

Kweli mkuu, wosia ni muhimu sana. Watu wengi huwa wanapoteza mali zao walizowekeza mfano biashara za ubia, pesa benki n.k kwa kutokuacha wosia.

Hata kama mali zake nyingine zisipoleta mgogoro lakini zile ambazo hazikuwa zinajulikana na wanafamilia huishia kuliwa na watu wengine kiulaini tu.
 
Ni kweli kabisa, jamii nyingi zina imani.potofu kuhusu wosia lakini umuhimu wake ni mkubwa na ni kitu ambacho kimepuuzwa kwa kiasi kikubwa pamoja na mdahara mengi yanayotokea baada ya misiba
 
Elimu ni muhimu kutolewa juu ya umuhimu wa jambo hili. Ni jambo ambalo kwa mtizamo wangu nadhani sio la hiyari sana bali ni la msingi (lazima).
 
Back
Top Bottom