Wizi unaofanywa usiku Dar kwa kukata nyavu za madirisha

Mar 15, 2018
26
36
Wadau ukipita sehemu nyingi Dar es salaam yani kwenye mitaa na makazi ya watu unakuta madirisha mengi ambapo nyavu au wavu ukiwa umechanwa ukionesha kuwa kuna wizi ulishawahi tokea

Wezi hao hutumia usiku wa manane kuwa ni nyakati ambazo wananchi wengi wamekuwa wamelala, hutumia dawa kama spray za kumfanya mtu alale au apoteze fahamu kwa mda fulani na kuanza kuchana nyavu za dirisha kisha kuanza kuiba sanasana wanaibaga simu, laptop na vifaa vinavyoweza pitika dirishani.

Japokuwa mitaa ya jiji la Dar es salaam lina ulinzi shirikishi na sungusungu lakini baado linaendelea kuwa changamoto ambapo wananchi wanaendelea kuathirikia, wadau tuchukue tahadhari nyingi mfano kutuacha simu na vifaa vingeni eneo la wazi wakati wa usiku, kulala kwa uangalifu pia kutoa taarifa ili wahajibishwe wahalifu.
 
Back
Top Bottom