_ BABA _
JF-Expert Member
- Nov 23, 2009
- 203
- 19
Jamani wana jamii ninaombeni sana msaada wenu..jana jioni siku ya Jumapili maeneo ya Metropolitan karibu na Green heart restaurant kwa wale wanaofahamu Arusha nikiwa kwenye pikipiki nilivamiwa na kundi la Vijana zaidi ya 50 waliokua wanaandamana wakaninyang'anya hand bag yangu kwa kuivuta kwa nguvu hadi ikakatika mkanda, nikashuka kuwafatilia wakatoa visu pamoja na sime wakanambia kama nataka kufa niwafate watu waliokuwepo around walinisihi nisiwafate maana wale jamaa ni watu wabaya na waweza hata niua,mie bado mgeni hapa Arusha, then wakatokomea nayo kuelekea maeneo ya Unga limited...kwenye hand bag yangu kulikua na IPAD aina ya APPLE 32GB pamoja na vitu vingine vidogo vidogo...nilifika kuripoti kituo cha police cha Unga limited askari nilimkuta akitiririka jasho kanambia ndiyo tu kwanza katoka kukimbizana na jamaa hao hao walimu-attack jamaa moja na kumchania suruali yake wakachukua pesa pamoja na walet yake pia huko njiani walikua wakipiga watu na kuwanyang'anya vitu kama handbags kwa akina mama?dada...Ombi langu kwa wana Jamii wa Arusha PLease ukiona mtu anauza IPOD mtaani au anataka kukuuzia or umepata fununu inauzwa sehemu naomba uni-PM or toa taarifa kituo cha polisi.......Nimefungua file pale Central na nina RB.....ninahitaji sana msaada wenu ndugu zangu maana hiyo IPOD ndiyo ilikua inanisadia kufanyia kazi zangu zote hata ku-browse hapa jamvini......natanguliza shukrani zangu kwenu nyote...