Wizara ya Mifugo na Uvuvi wekeni utaratibu rahisi katika kutoa vibali vya kusafilisha vitu nje ya nchi

Kipapuro

Member
Aug 12, 2012
32
14
Baada ya kurejea nchini, matumaini yangu na nguvu ya kuitumikia Tanzania yalikua makubwa kweli, Nilijaribu tafuta ajira kwa kipindi cha mwaka mmoja bila mafanikio, nikaamua kuanza kujiongeza kwa kutumia uzoefu wangu wa nje hasa katika e-commerce huku nikilenga kushirikiana na wajasiliamali wa ndani, ni sehemu ya kuinuana unajua ee? ILA NIMEANGUSHWA SANA na system now nimebakia mifupa, mda mwingine natamani kukimbia tena ila sio rahisi ukiwa ushafulia zaidi ya mack muga inabidi kuendeleza mapambano tu.

Sasa basi, moja ya fursa ya haraka niliyoiona na nikaiendea ni kuuza art and craft nje ya nchi, nikahangaika kweli kupata wateja, mteja wangu wa kwanza akakubali kujaribu kuuza bidhaa za tanzania (art and craft) katika duka lake, nimeingia cost zote kuandaa mzigo. Nilipoupeleka mzigo wangu wa kwanza posta wakagundua mzigo wangu una bidhaa moja (sea Shells) ambayo inahitaji kibali maalum, hilo sio tatizo kama nchi hatutakiwi wananchi kufanya mambo kiholela tu. Hivi vidubwana unavikuta beach vimetapakaa, niliviokota na kutengeneza necklaces mteja wangu akazipenda.

Hapa nikagundua kua tuna tatizo la information kwa wajasiliamali, wakaguzi wa posta wakanielekeza wizara ya maliasili, maliasili wakanambia sio wao ni wizara ya Mifugo na uvuvi. Nikaenda uvuvi naambiwa andika barua utajibiwa, Ubongo wangu ukaanza ongea wenyewe "Huyo mteja uliembembeleza, akajitahidi kukuamini ukampa expectation ya lini utatuma anakusubiri wewe" sikulisema nje kwa yule afisi alieendelea kunena " Kuna jamaa mmoja aliwahigi andika barua akajibiwa " nikasema tena ubongoni ee kumbe ni probability" na sio system ambayo ipo on place" tena sikuongea nje, busara inahitajika hii nchi uropokaji hausaidii nikawa nishagundua kua itachukua mda mpaka wizara ijibu barua yangu, nikaondoka zangu huku nikimsikia afisa anasema " anaogopa andika barua" lahasha it wasn't necessary unless kama itajibiwa katika mda mfupi but we both know how long it will take.

Basi kiunyonge nikaenda nikatuma bidhaa zingine chache tu zisizohitaji kibali, nikasema hizi nitatuma next time kama hizi zingine zikiuza, ila nilitumia mda kweli kuvitengeneza. Pale wizara ya maliasili wao wako very efficienty unaandaa invoice na copy ya kitambulisho, wanakadilia value unalipa fee unapata kibali unasafilisha kakifurushi kako, very well established system. Wizara ya uvuvi WE CAN DO BETTER mmeniangusha mtanzania tena duni sana, najaribu tu jenga nchi, hizi bidhaa tena hata sio illegal ni zinahitaji kibali tu, basi kuweni more efficient why haya mambo ya barua na kusubilia wakati it can be that simple? haya ndo maoni yangu.

Wadau mwenye uzoefu wowote on how to go about this nitashukuru sana. Sasa kichekesho ni kwamba vipo vidude kama hivi vinauzwa kariakoo, vimeingizwa kutoka china najiuliza nikivitumia hivyo kutengeneza bado watanidai kibali au utaratibu upoje?

uvuvi.jpeg
 
Kusoma nje ndio kumekufanya usijue lugha yako ya taifa?..
Matumizi ya r na l...
Matumizi ya herufi kubwa...

Kuwa mzalendo ndugu mtanzania
 
Kusoma nje ndio kumekufanya usijue lugha yako ya taifa?..
Matumizi ya r na l...
Matumizi ya herufi kubwa...

Kuwa mzalendo ndugu mtanzania
Asante sana kwa mchango wako mzuri, nimejaribu kufanya marekebisho kadhaa, kwa mchango wako post itasomeka vizuri kweli. Sio kusoma nje mkuu nadhani ni mapungufu yangu kwenye kiswahili nitajitadi kujifunza zaidi na kuwa mzalendo zaidi. Mchango mzuri sana, unajua nawezaje edit kichwa cha habari cha post?
 
Wababaishaji sana pale mapokezi, hata ukitaka kumuona bosi wao wanasema hayupo andika barua
 

VIBALI VYA UVUVI​

Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) inatoa vibali vya kuruhusu usafirishaji wa samaki na mazao ya uvuvi. Kabla ya kupata vibali, mwombaji anatakiwa kutimiza vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye sheria, kanuni na miongozo ya uvuvi.

Source: Mwanzo | Wizara ya Mifugo na Uvuvi
 
Back
Top Bottom