Wizara ya elimu someni haya.

malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,860
2,638
Wana JF,
Kwa ujumla mimi sikupenda kujiusisha na mjadala wa kwa nini Wanafunzi wa kidato cha nne wamefeli sana na nini tatizo. Lakini baada ya kukaa kimya nimepata jawabu la kuwasaidia hawa vijana wetu badala y akuwaacha wakawa Majambazi na kujiunga na tabia zisizofaa.

Nini cha kufanya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi ni, Kuwasajili wanafunzi wote wanaotaka kurudia mtihani kama private candidate na vilevile kuondoa masharti yote magumu yanayowabana private candidateyaani utungaji wa mitihani na ugawanyaji wa marks uwe kama wa school candidates. Hawa private candidate wawe na mtihani wao na school candidate wawe na mitihani yao. wizara iache mtundo wakutunga mitihani kwa kukomoa wanafunzi unaju walimu wengi mitihani hii ya form four wanashindwa kuijibu hata kwa %60, mitihani inakuwa migumu na inamitego ya kijinga kijinga, mithani iwe wazi kwa kuwapima watoto sio kuwakomoa, unajua mtihani wa kidato cha nne ni mgumu mara 10 wa Chuo kikuu. Elimu bora sio kutunga mitihani migumu. hapo hapo wengine wanawalimu wengi, wengine wanawalimu wachache, madawati, majengo nk.

Asanteni nawasilisha.
 
SIDHANI KAMA KWELI KUFELI KWA WANAFUNZI HAWA NI MITIHANI MIGUMU INAYO TUNGWA NA WALIMU WETU.KILA MMOJA KUANZIA MWANAFUNZI MWENYEWE , WAZAZI , WALIMU NA SERIKALI WANAHUSIKA KWA ASILIMIA SAWA.WANAFUNZI HAWASOMI KABISA , WAZAZI HAWAWAJIBIKI KIMALEZI YA WATOTO WAO WAMEWAKABIDHI WALIMU KAMA MA-HOUSEGIRL NA HOUSEBOYS WA WATOTO WAO WAZAZI KUPIGA WALIMU ETI KAMWADHIBU KIJANA WAKE SHULENI.WALIMU NAO WAMECHOKA KUONA JAMII HAIWAJALI WALA SERKALI HAITAMBUI MCHANGO WAO MAJIBU YA KAJELI NA DHARAU. SERIKALI HAIJUI KAMA INA SHULE ILA KINADHARIA INADANGANYA WANANCHI KUWA INAWAJIBIKA.HIVYO NDUGU SWALA SIYO MITIHANI MIGUMU SIJUI WEWE UMESOMA LINI .miaka ya kuishia 1999 ndo ilikuwa na mitihani migumu leo mwanafunzi anatungiwa maswali anayoyajua kwani tayari EXAMINATION RUBRIC zipo mashuleni na walimu wanazitumia .MCHAWI NI HAO MAADUI WANNE TAFUTENI UFUMBUZI WATOTO WATAFAULU.
 
kama watarudia kwa mtindo huo warudi miaka 3 nyuma toka 2009 wizara walipo anza kuchezea elimu.
 
Una uhakika mitihani ya kidato cha nne ni migumu kuliko ya chuo kikuu aisee?
 
"unajua mitahani ya kidato cha nne ni miguu kuliko ya chuo kikuu "
Hahaaaa usichekeshe chuo gani ulisoma?
 
Naomba tuangalie tatizo la kufeli kwa mapana yake shule za Kikatoriki zote wamepasua anga , Mary Goreti, Marian Boys na Girls nk wamepass DIV 1-2...!
Walikuwa na mitihani yao peke yao?
Tufunguke na tuwe wakweli , lack of discipline na kuwekeza ktk elimu.
Huwezi kuvuna bila kupanda na kupalilia
Tutaunda sana time za kuchunguza wakati ukweli uko wazi. Anza kuandaa mitaala.
 
Mtoa hoja unaonekana hijapita higher learning, huifahamu vizuri elimu. Mitihani ya kidato cha nne ni rahisi sana kwa mwanafunzi aliyesoma akaelewa vizuri. Utungaji wa mitihani uendelee kuwa uleule kwa watoto wanaojua wajibu wao watafaulu tu.
 
Wana JF,
Kwa ujumla mimi sikupenda kujiusisha na mjadala wa kwa nini Wanafunzi wa kidato cha nne wamefeli sana na nini tatizo. Lakini baada ya kukaa kimya nimepata jawabu la kuwasaidia hawa vijana wetu badala y akuwaacha wakawa Majambazi na kujiunga na tabia zisizofaa.

Nini cha kufanya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi ni, Kuwasajili wanafunzi wote wanaotaka kurudia mtihani kama private candidate na vilevile kuondoa masharti yote magumu yanayowabana private candidateyaani utungaji wa mitihani na ugawanyaji wa marks uwe kama wa school candidates. Hawa private candidate wawe na mtihani wao na school candidate wawe na mitihani yao. wizara iache mtundo wakutunga mitihani kwa kukomoa wanafunzi unaju walimu wengi mitihani hii ya form four wanashindwa kuijibu hata kwa %60, mitihani inakuwa migumu na inamitego ya kijinga kijinga, mithani iwe wazi kwa kuwapima watoto sio kuwakomoa, unajua mtihani wa kidato cha nne ni mgumu mara 10 wa Chuo kikuu. Elimu bora sio kutunga mitihani migumu. hapo hapo wengine wanawalimu wengi, wengine wanawalimu wachache, madawati, majengo nk.

Asanteni nawasilisha.

Matokeo ya Mitihani yataendelea kuwa mabaya tu mpaka JOYCE NDALICHAKO aondoke kwenye nafasi hiyo, yeye ndio anashindwa ku-manage wafanyakazi wake.
 
Back
Top Bottom