Wizara ya elimu isikurupuke katika maamuzi mashoga wako mitaani

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
MAKALA

WIZARA YA ELIMU ISIKURUPUKE KATIKA ,MAAMUZI MASHOGA WAKO MITAANI

Hivi karibuni serikali kupitia wizara ya elimu ilitoa waraka unazuia wanafunzi wa kuanzia darasa la awali hadi la nne katika shule za msingi kusoma kwenye shule za bweni, Waraka huo ulitolewa baada ya kuripotiwa kwa uchache matukio ya watoto wadogo kuhamasishwa kushiriki vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Waraka huo ulitoka huku serikali ikiwa imetuma timu yake ya kitaalamu kuchunguza uwepo wa madai hali hiyo katika baadhi ya shule mkoani Kilimanjaro.Kabla hata timu hiyo haijamaliza muda wake na matokeo kutangazwa bayana kwa watanzania wote serikali ikatoa tangazo la kusitisha watoto wadogo hao kusoma shule za bweni.

Baadaye serikali imetoa taarifa kupitia vyombo vya habari ikikariri waraka huo na mara hii ikiweka mkazo mpya kuwa wamiliki wa shule hasa za binafsi kuomba kibali maalumu kutoka kwa kamishna wa elimu ili kupata ruhusa ya kuwa na huduma za bweni kwa watoto wa chini ya darasa la tano.

Kwa mtazamo wangu serikali imefanya jambo jema ingawa naona kama imekurupuka kama ilivyokurupuka wakati wa serikali ya awamu ya tatu ilipofuta michezo mashuleni.

Naelewa nia njema ya serikali ni kudhibiti wimbi baya la watoto wetu kufundishwa tabia mbaya za ushoga zinazohamaishwa na mataifa ya magharibi.Lakini nia hii pia isigeuzwe kuwa tishio kwa uhai wa wawekezaji wa kitanzania waliowekeza katika miundombinu ya mashule.

Serikali imesema shule binafsi za bweni zianze kuchukua watoto kuanzia darasa la tano hadi la saba kwa shule za msingi.Kwa maana nyingine ni kuwa kama shule ilikuwa na mabweni 5 kwa ajili ya watoto 200 mathalani italazimika kutumia labda mabweni 2 tu na mengine yatabaki kuwa tupu.

Ikumbukwe kuwa mabweni haya yamejengwa kwa fedha nyingi,yana vitanda na pia magodoro na wakati mwingine mashuka.Serikali ndo iliruhusu uwekezaji huo kufanyika na miundombinu hiyo kujengwa kwa mamilioni ya fedha.

Si ajabu kukuta baadhi ya shule zetu za bweni wawekezaji wengi wana mikopo benki na wanatarajia kufanya marejesho ya mikopo yao mikubwa kwa kuwa tunajua ujenzi wa mabweni huchukua fedha nyingi na kwa muda mrefu.

Kuondolewa kwa huduma za bweni kwa watoto chini ya darasa la tano kutazifanya shule kukosa wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali na badala yake watalazimika kugombania wanafunzi walewale wa kutwa kutoka kwenye maeneo yao huku maelfu ya wanafunzi wakianza kuhaha kutafuta shule mpya za kutwa.HUU NI MKANGANYIKO MKUBWA.

Ukaguzi wa miundombinu ya mabweni umekuwa ukifanyika kuhakikisha usalama kwa watoto na hivyo serikali ilijiridhisha kwa kuwa na shule za bweni kwa watoto na ndio maana serikali kwa miaka yote imekaa kimya kuhusu taratibu za usajili wa shule za bweni lakini ghafla imekuja tu na waraka ambao unazuia watoto wadogo chini ya darasa la tano kusoma shule za bweni.

Maswali ni mengi hapo !je serikali imebaini kuwa shule za bweni ndio uhamasishaji wa ushoga na ulawiti unafanyika?na kama ndivyo kuna shule gani zimechukuliwa hatua hata ikibidi kufungwa?kuna walimu wowote waliobainika kushiriki au kuhamasisha vitendo hivyo na wamechukuliwa hatua gani?

Hivi karibuni gazeti moja liliripoti shule moja ya msingi ya serikali katika eneo la Marangu wilaya ya Moshi kijana mmoja alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kulawiti watoto 9 na hawa wanasoma shule na kurudi majumbani.Je hatari ya ushoga inawanyemelea wanafunzi wa kutwa pia?

Na kama ndivyo kuna shule gani ziko kwenye hiyo hatari?na kama sivyo kuna uchunguzi gani unafanyika kuwaondoa watoto wanaotembea umbali mrefu kurejea majumbani kuepuka mkono wa wabakaji ,walawiti na makubeli wa mifumo ya kishoga?

Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa kama serikali inatafuta sulushisho la kudumu la kukabiliana na wanaohamasisha ushoga na ulawiti mashuleni.Mashoga wamejaa mitaani sio mashuleni.Hivi karibuni kondakta na dereva walituhumiwa kumfanyia vitendo vibaya mtoto ambaye anasoma kutwa,je hii ina usalama kwa watoto ambao wanasafirshwa kwenye magari ya shule na ambayo wakati mwingine hayana usimamizi?

Wazazi wanaoondoka alafajiri kwenda kazini anamwachia nani kumwandaa mtoto kwenda shule?sio ndio tunaacha watoto kwenye hatari?na mzazi akirudi usiku anakuta mtoto amelala wala hajui kinachaoendelea kwa mtoto.

Lakini pia kuna wazazi wa wanafunzi ambao kwa asili ya kazi zao au mihangaiko ya maisha wanalazimika kuamka alfajiri na kwenda kutafuta riziki au hata ajira wameamua kujitwika mzigo wa kutafuta ada kwa kazi hizo huku watoto wakiwa shule za bweni .wazazi hawa watalazimika kuacha shughuli zao hizo na kuanza kulea watoto tu ili wafike darasa la tano ndio waendelee na shughuli nyingine?je hili ni jambo linalowezekana kwa hali ya maisha ya sasa?

Nionanvyo mimi nyumbani ni hatari kuliko bwenini hasa kwa wazazi ambao wana shuguli za kufanya nje ya makazi yao,wakati mwingine nyumbani watoto wanabaki majumbani wanatazama TV chanel za ngono ,na wakati mwingine watoto wanaweza kuwa wametoka nje ya nyumba zao na kwenda kuzurura huko na kule na ambako wanaweza kufundishwa mambo mabaya.

Je serikali inaliona hili?

Mosi ,kubadili mifumo na taratibu za kikanuni kwa shule za bweni kuchukua wanafunzi kuanzia darasa la tano sio tu kuwa ni hasara kwa wawekezaji hawa wa ndani bali pia sio njia pekee kumaliza tatizo la ushoga usagaji na ulawiti.

Tatizo liko kwenye jamii yetu.Serikali hasa wizara ya utamaduni imekaa kimya kana kwamba haina majukumu ya msingi,imeacha tamaduni zetu zikimomonyolewa na tamaduni za kimagharibi bila kuchukua hatua.vijana wanavuta bangi hazarani,vijana wanavaa mavazi ya aibu mafupi kupita kiasi kwa wasichana na mengine yakiwaonyesha hadi sehemu za siri. wizara ya utamaduni iko kimya tu ilihali ikijua huo sio utamaduni wetu.

vijana wa kiume wanavaa milegezo ,wanatoa matusi kwa watu wazima bila karipio lolote kutoka kwa jamii au serikali .kwa ujuma maadili yameyumba.Lakini maadili yetu yanayumba wakati nchi kama India,Korea,Japan na hata uchina hazijabadilisha au kuiga tamaduni nyingine mbaya kutoka mataifa mengine.Sisi tumeiga na tukanyamaza kimya,watoto wetu wanaharibika mno.

Pili,huwezi kutatua taizo kwa kutengeneza tatizo jingine.Kwa kinachoonekana hapa ni kuwa serikali itatengeneza tatizo jingine wakati ikijaribu kutatua tatizo la awali la vitendo vya ushoga,usagaji au ulawiti mashuleni.

Nifahamuvyo mimi ni kuwa ,wazazi wanapeleka watoto katika shule wanazoziamini na ni baada ya kujiridhisha kuwa shule husika zinalea watoto wao vyema kwa hiyo serikali hasa wizara ya elimu ifanye uchunguzi wa shule ambazo zina mifumo dhaifu ya malezi na ambazo zinadaiwa kufundisha maadili mabaya na zisiruhusiwe kutoa huduma za bweni au zifungiwe kabisa kuliko kujumishashule zote nzuri na mbovu kwenye kapu moja.

Kwa nini serikali isiimarishe mifumo ya usimamizi wa maadili na malezi na taaluma kwa watoto wa bweni kuliko kuwarejesha majumbani ambako watakutana na wajomba,wapwa na hata ndugu wengine ambao pia wanaweza kuwa hatari kwao?

Serikali iweke vigezo muhimu vya kusimamia maadili mashuleni na sio kukurupuka kusitisha huduma ambazo kwa miaka nenda rudi zilikuwepo na kama wanaona kuna haja hiyo basi watoe muda kwa shule na wazazi kujipanga kufuata mabadiliko hayo.Lakini pia ni vyema tujifunze nchi nyingine za kiafrika zinafanya hatua zipi kukabiliana na tishio la ushoga na ulawaiti mashuleni .hili ni janga la kimataifa tubuni mbinu sahihi na endelevu za kulikabili tukikurupuka tutaleta changamoto kubwa Zaidi katika mfumo wetu wa elimu na hatimaye katika maisha yetu.

Kuna watoto wanatoka katika maeneo ambayo hakuna shule za English medium kwa tangazo la serikali watoto hawa tarejea makwao na kuanza kusoma shule zamichepuo ya Kiswahili je hiisio hatari?haitayumisha mfumo wa elimu?

Wizara itulie kisha ishrikishe wadau watafakari kwa pamoja hatua muhimu za kuchukua zisizo na madhara kwenye elimu yetu,tamaduni zetu na desturi zetu za kimaisha.TUSIFANYE MZAHA NA HILI JAMBO.
 
Back
Top Bottom