Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Sijui niwape tusi gani hawa watu.
Yaani akili zao ni kopo kabisa, mpaka Magufuli aongee jambo ndio huja na maagizo.
 
Hivi kweli hii ni barua au taarifa ya wizara?!? Kama ni kweli inaelekea ndani ya serikali Kuna watu hawajui kabisa lugha kikiwemo hata Kiswahili...shame on them...Hakuna neno swala au maswala kwa maana inayoeleweka kwa barua au taarifa hiii..ila Kuna suala au masuala..
Fahamu kwamba hawa hawa unaowaona huku mitandaoni wanachafua lugha kwa kuandika xx badala ya sisi, amna badala ya hamna, ana badala ya hana.... ndio hao hao wako ofisini. Umakini unakuwa mdogo anapoandika taarifa ya kuja kwenye jamii anadhani anaandika kwenye page yake ya Instagram

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unashangaa hilo wakati Rais katuma ndege Madagascar kuchukua dawa ya kutibu ugonjwa unaoathiri Mafenesi?

Sent using Jamii Forums mobile app
I am sorry kwa nitakayoandika hapa kuhusu comment yako hii....nadhani miongoni mwa watu wa ajabu nchini mwetu na pengine mwenye uelewa mdogo was issues mbalimbali na hata mpotoshaji mkubwa pengine wewe unaweza kuwa mmoja wao...Rais atume ndege kuchukua dawa ya kutibu mafenesi?

Wapi na wapi? Kwa kile alichobainisha leo Rais kilipaswa kukushitua wewe, Mimi na wenzio na wenzetu watanzania kwamba Kuna mchezo au mzaha mkubwa kuhusu ugonjwa Corona...Tunapaswa kuvipongeza vyombo vya dola kuhusu kazi waliyofanya...kwamba wamepeleka maabara samplesi mbalimbali yakiwemo majimaji ya mafenesi, kondoo na kadhalika wakiwemo of course binadamu ili kutest Corona...na yakatokea hayo tuliyoambiwa na Rais ...Hilo ni Jambo zito...Sasa wahusika saa hizi matumbo yao ni Moto...wewe unaleta kejeli na dharau mbaya (insubordination) kwa Rais...sisi sisi watanzania wengine tukoje.

Mimi binafsi nafahamu issue moja iliyotokea miaka ya nyuma kwenye hospitali moja ya binafsi ambapo walitegeshewa sample ya damu ya kuku na vipimo vikaja kwamba Kuna malaria...kilichotokea siwezi kuweka wazi hapa...ila kilichofanyika Sasa kuhusu samples/specimen za Corona ni la kutufumbua macho....maabara zetu zinapaswa kuwa makini....
 
Nitoke nje ya mada.

Hatuwezi kuongozwa na wanasiasa kwenye hiki kipindi kigumu kisha tutarajie kuushinda huu ugonjwa.

Ingekuwepo kamati ya wataalamu wa afya na majanga ingekuwa heri mihemko na hisia zingepungua...
Hii ipo Tanzania tu mwanasiasa anaamua hatma ya wananchi. Nasi pia tumejenga utaratibu wa kuwasikiliza as if wao ni wataalamu wa kila kitu kwenye maisha.

kuna vitu vinatolewa maelekezo na wanasiasa unaona kabisa ni maelekezo ambayo hayana tija kabisa na nafikiria watu watampraise huyo mwanasiasa.

Elimu, elimu, elimu ni janga kubwa ndani ya taifa hili.
 
Fahamu kwamba hawa hawa unaowaona huku mitandaoni wanachafua lugha kwa kuandika xx badala ya sisi, amna badala ya hamna, ana badala ya hana.... ndio hao hao wako ofisini. Umakini unakuwa mdogo anapoandika taarifa ya kuja kwenye jamii anadhani anaandika kwenye page yake ya Instagram

Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks...nimekuelewa...
 
Tatizo liko hapa, hao wataalamu mbona hawawezi kujitokeza na kuwapinga hawa wanasiasa? Nangalia USA kwa mfano, Dr. Anthony Fauci anajibu technical questions daily, wanapredict vifo na cases za COVID 19. Trump anatekeleza bila ubishi wowote. Maseneta wanapokea reports za majimbo toka kwa wanasayansi, nk Daby,

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko ni Marekani ndugu, huku aina ya ushauri unaotekelezwa hujauona? Mmoja kashaapishwa leo, pitia Hansard utaona ushauri alioutoa hivi karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi naipongeza sana serikali na wizara ya afya kwa ujumla, suala la kuzika usiku lilileta taharuki kubwa kwa jamii na si utamaduni wetu ingawa ni kweli kuwa ushauri wa kitaalamu unaweza kutolewa kunusuru hali iliyopo.
 
Hivi kweli hii ni barua au taarifa ya wizara?!? Kama ni kweli inaelekea ndani ya serikali Kuna watu hawajui kabisa lugha kikiwemo hata Kiswahili...shame on them...Hakuna neno swala au maswala kwa maana inayoeleweka kwa barua au taarifa hiii..ila Kuna suala au masuala..
😭😭😭😭😎😎😎😎 ndiyo wataalam wetu wanatumika kuandikia viongozi. Hivi hao viongozi hawafanyi proof reading? Swala ni mnyama tena hana wingi. Eti maswala. Yaani kiingereza shida na Kiswahili shida.
 
Watu kuzikwa kama wanyama usiku wa manane haikubalikik nakupongeza sana mganga mkuu prof. Abel Makubi na wizara kwa ujumla uwezo wako toka ulipokua bugando ulionekana Hongera sana...

Its not over until its over...
emoji769.png


View attachment 1438546

Yaani ndio mnakumbuka leo
 
Wakuu nimesikiliza clip ya mwenye nchi. Ninachoona Siasa na utaalam siyo vitu cha kuchezea. Mfano kuzikwa Marehemu wa Corona kama ilivyo waliofariki na magonjwa mengine ni suala la tahadhari mno. Mwili wa Corona ili uweze kuweka mfano kwa jeneza au mkeka kwa wenzetu madawa yake na PEP siyo mchezo.

Ni nani atagharamia hizo dawa na mavazi ili kuhakikisha ni salama? Hapo ni lazima wenye uwezo ndiyo wataweza. Serikali haiwezi gharama PPE za Marehemu wakati watumishi wa afya hawana. Hivyo wenye uwezo mdogo bado serikali itasimama mazishi. Uzuri ni kwamba maziko yatakuwa mchana ili yashuhudiwe.

Poa wahudhuriaji nafikiri ni Ile maximum 10 au hapo umma umeruhusiwa? Tuwe makini mno na hizi statements. Umakini usipochukuliwa na utaalam kuzingatiwa basi tegemea maajabu ya maambukizi.

Haya ni maoni yangu sipingani na mwanasiasa bali nashauri utaalam usikilizwe pia. Hii ni kwa manufaa mapana ya nchi na raia wake.
 
Hapana Monk wanajeshi hawafai...hapa wangepewa kazi madaktari..

Rais angekuwa anapokea ushauri na taarifa ya watalaam. Sasa kamati iliyoundwa inaongozwa ma yeye na nyingine eti waziri mkuu.

Wanajua nini kuhusu magonjwa! Wanasiasa wangeshughulika na siasa. Sasa hapa kwetu ukishakuwa mwanasiasa basi wewe ni daktari, mchumi, mwalimu, askari, mwanasheria na kila kitu.

Hapa nilipotaja chembe chembe za kijeshi sikumaanisha wajeshi wahusishwe peke yao mkuu, najua na wenyewe wana madaktari wao lakini hiyo timu iwe na nidhamu na weledi kama ilivyo wajeda.
 
Sasa wakati zoezi linaendelea wao walikuwa wapi?..
Ina maana wazikaji walijiamulia Tu kuzika usiku?
Watanzania hawana utamaduni wa kuzika wapenzi wao usiku wa manane ila kwa maagizo toka juu inaonekana Awamu hii iliamua kuchukua jukumu la kuzika wafu usiku kukwepa utamaduni uliokuwapo wa mtu yeyote asiyefika kwenye mazishi hutengwa na akifariki hususiwa kuzikwa. Kuzika usiku ni rahisi kupata watu chini ya 10 wa kumzika kila mfu kama Serkkali ilivyotaka. Kwa uamuzi huu mpya utashuhudia maelfu ya waombolezaji wakishiriki kila mazishi.
 
Back
Top Bottom