Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Kataskopos,

Mal upo sahihi kabisa maamuzi ya mwisho ya nini kifanyike katika majanga kama haya yapo kwa wenye dhamana ya ambao ni wanasiasa tuliowapa hiyo dhamana.

Lakini kuwa na dhamana inatosha wewe kutoa maamuzi? Jibu litakuwa hapana.

Hapo ndipo tunahitaji wataalamu kusikilizwa kuliko yeyote yule. Mtaalamu kazi yake sio kutoa maamuzi. Hapana, ila atuambie tufanye nini na tusifanye nini. Na tukishafanya nini kitatokea na nini hakitatokea.

Nisiingie ndani zaidi ila tuna mifano tumeona ulimwenguni.

Mtaalamu anakuwepo pembeni kiongozi wa kisiasa anapo ongelea chochote kuhusu korona. Kiongozi wa kisiasa makini yeye kazi yake anasikiliza wataalamu wanasemaje. Kisha anapima je anachosema mtaalamu kisheria/kimamlaka kitaendana? Mwisho maamuzi sahihi yanafanyika.

Kinachofanyika hapa kwetu mizani unayoizungumzia haipo.... wanasiasa wamehodhi maamuzi yote yawe ya kitalaam na ya kisiasa.
 
Tatizo liko hapa, hao wataalamu mbona hawawezi kujitokeza na kuwapinga hawa wanasiasa? Nangalia USA kwa mfano, Dr. Anthony Fauci anajibu technical questions daily, wanapredict vifo na cases za COVID 19. Trump anatekeleza bila ubishi wowote. Maseneta wanapokea reports za majimbo toka kwa wanasayansi, nk

Sent using Jamii Forums mobile app

Wataalamu kisheria hawana mamlaka ya kuongelea lolote litokealo. Unajua fika ukiongelea umevunja sheria na unajua mifumo yetu ya kiuongozi. Utakamatwa.


Lililotakiwa kuwepo mizania ya utaalamu na siasa. Kwa kipindi hiki tungependa kuona utaalamu unapewa kiupaumbele zaidi ya siku zingine.

Wanasiasa wapokee emperical data kutoka kwa madaktari wabobezi. Wakae nao meza moja wapime dos na donts za korona. Kisha waje kwenye vyombo vya habari tupewe way foward.

Mimi ningekuwa serikali hata pale bungeni wakati wanajadili ugonjwa Daktari angekuwepo sio kila mmoja kujifanya ni daktari.
 
Daby,
Uko sawa kabisa kiongozi, ndiyo maana nikasema lazima tuweke uwiano mzuri (strike a balance) kati ya maamuzi ya kisiasa na yale ya kitaalamu. Ukisoma vizuri kwenye bandiko langu nimesema kabisa ilitakiwa iwe hivyo kwamba wataalamu wafanye kazi mkono kwa mkono na wanasiasa lakini haiko hivyo kwasababu siasa zimetawala nchi. Ila hata kama wakianza kufanya hivyo sasa bado hawataaminika kwasababu utawala huu umeshapoteza imani kwa wanananchi walio wengi hasa linapokuja suala la kushughulikia majanga makubwa kama haya.
 
Master Mind,
pengne walijianzia 2 kuzika uck ndo sasa mmegu2ka kuwashauri. Hii ni vita ye2 sote 2simwachie rais pekeake, tarehe 2 may 2020 mweshmiwa rais alitoa hotuba ilifumbua mamb meng, wizara ya afya mmefeli kwa kias kikubwa xana mambo mazito mbka ayagundue rais! kah? Mmezidi. Na nyie maprofesa, lecturers kutoka vyuo mbalimbali mnashndwa kufanya tafiti juu ya covid19? Kah? MWone aibu.

NA haya yote yanatokea kwasababu ya mfumo wa elimu 2lionao. Ndalichako umetulia 2 kama haupo vile husemi hata ki2 lakin sio shida kaa ivo ivo kmya ataongea mweshmiwa rais au waziri mkuu. Niwatie moyo wananchi wenzangu kuwa tanzania ha2na wanasiasa wazalendo wapinzani.

2lionao ni wabwabwaji wanadhani kuwa bado watanzania ni wajinga. mWisho dua nyingi zimwendee mweshmiwa rais wa jamhuri ya muungano ya tanzania, waziri mkuu mhe. kassim majaliwa na matabibu mnaowashughulikia ndugu zetu. amen
 
Hivi kweli hii ni barua au taarifa ya wizara?!? Kama ni kweli inaelekea ndani ya serikali Kuna watu hawajui kabisa lugha kikiwemo hata Kiswahili...shame on them...Hakuna neno swala au maswala kwa maana inayoeleweka kwa barua au taarifa hiii..ila Kuna suala au masuala..
Kifimbo cheza
Vipi kazi zinaendaje hapo BAKITA?

Au modds mnasemaje?
 
Back
Top Bottom