#COVID19 Wizara ya Afya itafutiwe Waziri mwingine

Tumbu

Senior Member
May 27, 2021
109
96
Nimeona mtandaoni namna ambavyo Waziri wa Afya ndugu Dorothy Gwajima alipokua anajibu hoja za Askofu Gwajima wa kanisa la ufufuo na uzima na mbunge wa Kawe.

Zaidi ya mipasho hakukua na majibu ya moja kwa moja ya kuwashawishi wananchi wakapatiwe chanjo ya UVIKO_19. Kwamaelezo ya waziri inaonekana wizara imeshashindwa kutoa elimu ya ushawishi kwa wale ambao hawajaona umuhimu wa kuchanjwa kwa sababu mbalimbali.

Waziri wa afya ameshindwa kushambulia hoja badala yake anashambulia mtoa hoja,hii ni aibu kwa chama na serikali. Anachofanya nikuliomba jeshi la polisi na TAKUKURU wamuwajibishe askofu Gwajima. Kwa maelezo ya Dorothy Gwajima,wenye mashaka juu ya chanjo hawajapata ushawishi bado.

Bora Joti, Masanja, Mkojani, Waigizaji wa Futuhi na Mizengwe wangepewa kazi ya kutoa elimu na waziri huyo akaambiwa asiseme chochote kuhusu UVIKO_19.

Mh. Rais tafuta mtu mweledi ambaye anaelewa dhamira yako ya kufanya uruhusu chanjo. Huyu Dorothy inawezekana anaelewa dhamira yako bali hawezi kutuelewesha hicho alichoelewa kutoka kwako. Hapa kwa mbaaaaaali namuona Kigwangala akipanda chati
Mh. Rais tafuta waziri wa afya anayeweza kujibu maswali ya wanaopinga chanjo huyo aliyepo anazidi kukuhujumu na yupo kimipasho zaidi.
 
Huwezi kusema mimi ni mwanaume wakati huo huo ni mwanamke lazima uchague moja kusuka au kunyoa.

Hawa mawaziri mtawalaumu bure ndio maana kiustaarabu ilitakiwa baraza livunjwe.

Jaman mwaka mmoja tu ulisema Corona haipo na chanjo No. baadae kidogo useme ipo na chanjo ni lazima inahitaji uwe na kipaji kikubwa cha "Bsc. in Arts of backwardness"
 
Huyu mama hafai kushika wizara nyeti Kama hiyo,akiimaliza hii awamu akiwa waziri wa afya ashukuru Mungu,sioni future nzuri kwa huyu mama tangu enzi za Magufuli,asipobadilika huyu mama ataishia pabaya.

Huyu mama naona Kama hawaendani na mama Samia.
 
Huyu mama kazi imemshinda. Angepatikana mtu sahihi wa kupinga hoja za askofu kwa weledi na ushahidi wa wazi(kama upo), watu wengi sana wangechanja.

Maana kule kusema askofu akamatwe, kumeimarisha na kuwapa ujasiri zaidi wa kutochanja wanaoamini kauli zake.
 
Sio vizuri kulaumu sana muda wote hasa kwa mtu aliyetangulia mbele za haki, lakini ile awamu tuliambiwa anawahitaji vichaa vichaa, tukaona aina ya mawaziri vituko akiwepo huyu Mama.

Kwanini bado yupo hadi sasa ndio swali kubwa linalokosa majibu. Nchi ipo kwenye mapito yanayohitaji mtu makini na mweledi kuendesha hiyo wizara. Kwa unyeti wake haihitaji msanii pale.

Na sio lazima uwe msomi sana au daktari bingwa kung'amua kwamba yule Mama iko namna vitu havijajipanga ipasavyo kichwani. Vinginevyo, anajitoa ufaham ambayo nayo bado ni tatizo.
 
Waziri anakosa washauri kuwasikiliza. Kama umeshakua udhaifu wako ni bora wataalamu wangekuwa wanamsaidia cha kuongea
 
Shida ni kuwa hamjaelewa kitu kimoja ni kweli kuwa nchi za wazungu wanatoa mapesa mengi hasa kwa nchi kama Tanzania ili kupambana na janga la corona.....na mojawapo ya malengo ya pesa hizo ni utoaji wa elimu kwa jamii inayohusu kujikinga na mambo mengine kama chanjo....SHIDA NI KUWA HIZO PESA ZINAPIGWA NA WAJANJA WANAZITUMIA KWENYE MAMBO YAO NA KINACHOFANYIKA KWA SASA NI USANII TU...
 
Na hizo pesa wanazotoa wanakupenda saana au wanaipenda nchi yako saana tu kwa mazuri ikiwa huko huko nchi za kwao na wao wana majanga tena makubwa?

Wao wanakupa kwa malengo yao nyeti hautaambiwa raia wa kawaida kama wewe na mimi.Wanaojua ni viongozi wetu tu.Na walivyo wanafiki ukienda kinyume na matakwa yao ni wepesi tu kukuondoa kwa kutumia propaganda na ikiahindikana watatumia military(mara nyingi hii military ni suluhisho ambalo hutumiwa mwishoni yakishindikana yoote).

Kuhusu chanjo nayo Sisi nchi zetu nazo zimezidi kila kitu zisaidiwe tuongelee tu ya Covid-19 hakuna nchi hata moja kusini mashariki kaskazini wala magharibi imetoa mchango wa pesa au wa wataalam au mawazo kufanya utafiti wa chanjo ikapatikana.Tutapata wapi jeuri ya kusema chanjo haifai? Au ukisema inafaa wewe ulikuwepo maabara wakati wanaigundua?

Ifike kipindi tuwe tunatizama tu haya maigizo siyo wote lazima tuwe wasanii.Ila nimependa hapo mambo ya upigaji pesa huo upo hata nchi za wenzetu japo wenzetu wanapiga na vitu vinaonekana kwa raia hata kama siyo nusu ya yale ambayo walitarajia.Hapa kwetu kama tanzania unapigwa bila chenga na utahoji mitandaoni tu kama hivi live ni ngumu.Safari bado ni ndefu kwa kweli.
 
Acha wivu, muache Dorothy atakeleze majukumu yake
IMG_20210818_150417.jpg
 
Huyu mama hafai kushika wizara nyeti Kama hiyo,akiimaliza hii awamu akiwa waziri wa afya ashukuru Mungu,sioni future nzuri kwa huyu mama tangu enzi za Magufuli,asipobadilika huyu mama ataishia pabaya.

Huyu mama naona Kama hawaendani na mama Samia,
Naona kama amebebeshwa mzigo mzito sana
 
Tatizo ni mfumo wa Sasa wa Nchi yetu!Kuingiza wataalamu katika Mambo ya siasa!
Dk Dorothy siyo mwanasiasa hivyo Serikali ilipaswa kumwacha aendelee kuhudumia wagonjwa pale Muhimbuli au hospitali yo yote ya Serikali! Nikimwangalia zaidi kwa anayofanya ni kama alikuwa daktari katika Psychiatric Ward!
 
Huyu alipewa nafasi kwa kuwa na "usukuma" ila hana uwezo kwa kweli !!! Magu aliharibu sana hili taifa!!!
 
Nimeona mtandaoni namna ambavyo Waziri wa Afya ndugu Dorothy Gwajima alipokua anajibu hoja za Askofu Gwajima wa kanisa la ufufuo na uzima na mbunge wa Kawe.

Zaidi ya mipasho hakukua na majibu ya moja kwa moja ya kuwashawishi wananchi wakapatiwe chanjo ya UVIKO_19. Kwamaelezo ya waziri inaonekana wizara imeshashindwa kutoa elimu ya ushawishi kwa wale ambao hawajaona umuhimu wa kuchanjwa kwa sababu mbalimbali.

Waziri wa afya ameshindwa kushambulia hoja badala yake anashambulia mtoa hoja,hii ni aibu kwa chama na serikali. Anachofanya nikuliomba jeshi la polisi na TAKUKURU wamuwajibishe askofu Gwajima. Kwa maelezo ya Dorothy Gwajima,wenye mashaka juu ya chanjo hawajapata ushawishi bado.

Bora Joti, Masanja, Mkojani, Waigizaji wa Futuhi na Mizengwe wangepewa kazi ya kutoa elimu na waziri huyo akaambiwa asiseme chochote kuhusu UVIKO_19.

Mh. Rais tafuta mtu mweledi ambaye anaelewa dhamira yako ya kufanya uruhusu chanjo. Huyu Dorothy inawezekana anaelewa dhamira yako bali hawezi kutuelewesha hicho alichoelewa kutoka kwako. Hapa kwa mbaaaaaali namuona Kigwangala akipanda chati
Mh. Rais tafuta waziri wa afya anayeweza kujibu maswali ya wanaopinga chanjo huyo aliyepo anazidi kukuhujumu na yupo kimipasho zaidi.
Dr. Z.Chaula will fit for the post.
 
Back
Top Bottom