Wito kwa JK: Jenga Serengeti Highway na Fast speed Rail

Katika kuonesha yuko serious ajenge kabisa na kile kiwanda cha magadi pale lake natron
 
Kumbe welfare ya wanyama ni bora kuliko binaadamu.
TAZARA imepita Selous na Mikumi mpaka leo wanyama wapo!
Ilo la Vyura uko malagalasi limenichosha mbona Kihansi kuna vyura na kuna bwawa.
Issue sio kuacha mradi bali go for both plans to proceed with the project and conserve the environment.KIHANSI tumeweza uko why tushindwe

Mkuu reli ni bora kuliko barabara. Madhara ya uwepo wa reli hifadhini ni madogo kuliko uwepo wa barabara.

Hapo mwisho ni sawa kabisa. Kutengeneza win-win situations kwa maendeleo na mazingira ni muhimu sana. Ila pale inapoonekana upande mmoja utapoteza,basi mradi upewa mapendekezo kwa njia ya shughuli au mradi mbadala wenye kutengeneza win-win situation.
 
Kuna umuhimu hiyo barabara kujengwa , utanyanyua uchumi sana kwa watu wa kanda hiyo sana . Ila wakenya wanawachezea wa tz kama watoto wao . Sijui tiss wapo wapi ? Lowassa angekuwepo huu ujinga usingekuwepo.

Umuhimu kweli upo. Lakini je at the expense of what?!
Mradi ungeendelea kama ulivyokuwa umependekezwa ungeleta madhara makubwa kwenye ecosystem ya Serengeti-Masai Mara. Ecosystem ambayo inachangia pato kubwa kwa taifa kupitia utalii na utafiti. Pia route iliyopendekezwa ilikua haina trickle down effects kama alternative route iliyopendekezwa. Maana ile route kwa sehemu kubwa ilikua ipite mahala pasipo na makazi ya watu,ilhali alternative route ingependa mahala penye makazi ya watu.

Mkuu katika hili tuweke siasa pembeni na tutumie utaalamu na weledi katika kujadili na kufikia muafaka.
 
Mikataba yote ya mazingira inazibana nchi changa ili zisiweze kupiga hatua ya maendeleko. Kuna ule mkataba maarufu wa Kyoto ambao unataka mataifa makubwa yenye viwanda yapunguze emission ya carbon dioxide inayoongeza joto ili kuhifadhi leya ya ozone. Amerika (USA) ambaye ndiye nchi yenye viwanda vingi duniani ilikataa kusaini mkataba wa Kyoto.

Kama leo tunajadili existence ya wanyama na tunataka tu equate na wanadamu kwa vijisababu vya environmental impact, nafikiri tunapoteza mwelekeo. Hata kwenye vitabu vitakatifu hususan biblia tunaona mungu aliumba dunia, akamuumba mwanadamu na akamkabidhi mamlaka juu ya wanyama watambaao, watembeao na waarukao Mwanzo 1:25-28.
 
Kama issue ni wanyama kufa tuweke barabara then tuangalie tufanyeje magari yawe yanaenda kwa mwendo wa kawaida yafikapo hayo maeneo. La sivyo sisi tutabaki ***** mtozeni

Kwa Mikumi hilo naona halijafanikiwa. Mikumi National Park (MINAPA) walijaribu kufanya stakeholders' workshop katika kuelimishana,lakini hawakufanikiwa. Na moja ya sababu ni wao kuwaita wamiliki wa vyombo vya moto vinavyopita pale,na kuwasahau watumiaji halisi wa hiyo njia. Madereva,makondaktana matingo wa malori na mabasi,bila kusahau abiria (nafikiri kuna chama cha wasafiri/abiria hapa TZ) nao walipaswa washirikishwe katika kuelemishana juu ya matumizi angalifu ya eneo la barabara ndani ya hifadhi.

Barabara ilijengwa wakati sheria na kanuni za kuenforce tathmini ya madhara katika mazingiria na jamii (sheria ya mazingira namba 20 ya 2004 na kanuni zake za mwaka 2005) hazijatungwa. Hivyo alternative routes na mapendekezo ya namna ya kuepuka na kupunguza madhara kwa mazingira na wanyamapori yasingeweza kutolewa.

Ila bado kuna nafasi kupitia environmental auditing,ambapo kunaweza kufanyika aina ya tathmini ili kuangalia madhara halisi yanayotokea pale Mikumi na kuweza kutoa mapendekezo ya kupunguza madhara hayo.
 
Mikataba yote ya mazingira inazibana nchi changa ili zisiweze kupiga hatua ya maendeleko. Kuna ule mkataba maarufu wa Kyoto ambao unataka mataifa makubwa yenye viwanda yapunguze emission ya carbon dioxide inayoongeza joto ili kuhifadhi leya ya ozone. Amerika (USA) ambaye ndiye nchi yenye viwanda vingi duniani ilikataa kusaini mkataba wa Kyoto.

Kama leo tunajadili existence ya wanyama na tunataka tu equate na wanadamu kwa vijisababu vya environmental impact.

Mkuu suala la Kyoto Protocol na ujenzi wa barabara yenye madhara katika mazingira havihusiani.

Suala la Kyoto Protocol hakika ni kwamba nchi zinazoendelea zimekosa sauti ya pamoja katika kulitia mkazo. Ndiyo maana nchi kama Marekani na China zinasuasua kujifungua kwa kukubali hiyo protocol.
Juzi pale Joburg katika Conference of Parties (COP),nchi zinazoendelea badala ya kuzishurutisha nchi zinazoendelea zizingatie mkataba wa Kyoto,zenyewe zinapiga kelele kutaka pesa kupitia Climate Funds.

Umaskini wetu ndiyo unatuponza katika utekelezaji wa Kyoto Protocol. Sasa tumeletewa Reducing Emissions from Deforestation and Forest Degradation (REDD);kwa kiswahili Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kupitia Ukataji Miti na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI). Huu ni usanii na unafiki wa kiwango cha juu kutoka kwa nchi zilizoendelea. Kwa sababu utunzaji wa misitu pekee hautasaidia kama nchi hizo zinaendelea kuzalisha hewa ya ukaa (CO2) kwa million of particles.

Kwa hiyo mkuu kufananisha mambo ya Kyoto Protocol na ujenzi wa barabara pale Serengeti si sawa. Kwa kila jambo lanatazamwa na kutekelezwa katika angles tofauti.
 
Nnzi. Naanza kuhisi kuwa mchangiaji hoja anayeitwa Nzi, ni miongoni mwa Watanzania ambao ni mawakala wa Kenya ambao kila uchao wanabwata kuhusu maendeleo ya Tanzania
 
Nnzi. Naanza kuhisi kuwa mchangiaji hoja anayeitwa Nzi, ni miongoni mwa Watanzania ambao ni mawakala wa Kenya ambao kila uchao wanabwata kuhusu maendeleo ya Tanzania

Mkuu hakuna cha uwakala.
Weka siasa pembeni, ili tujadili kitaalamu na kiweledi.
 
Mkuu hakuna cha uwakala.
Weka siasa pembeni, ili tujadili kitaalamu na kiweledi.

Mkuu sijaongea siasa ila wewe ndiyo uko kwenye siasa. Mimi nimeangalia uhalisia in a broad spectrum na kujiuliza je ingekuwa Tanzania ni Japan, UK au USA na inataka kupitisha barabara kwenye mbuga zake, je nani angefungua mdomo wake kuuliza.

Nyie akina NZI nawaona more or less ni vibaraka wa serikali ya Kenya ambao munatumika kwa viji pesa kidogo munavyopewa kwenye NGO zenu. Bahati mbaya mumekosa ajira ya serikali kutokana na ufinyu wa ajira kwa hiyo mumeamua kuwa malaya wa akili zenu. Muko tayari kutumia akili zenu dhidi ya mambo halisi ili kuwaridhisha mabwana zenu wa Kenya.

Kenya wanajenga Airport karibu na Mlima Kilimanjaro upande wao, Kenya wana hoteli zaidi ya 20 za nyota tano kwenye mbuga ya Masai Mara lakini hamna anayeona environmental abuse upande wao. Lakini Tanzania ilipojenga Bilila Lodge Kempiski tukaambiwa tume disturb eco system ya wanyama.

Juzi wamezindua ujenzi wa bandari ya Matrillion ya Shillingi kwenye ukanda wa Lamu ili kuweza kuvuta biashara ya mizigo toka Ethiopia na South Sudan. Wenzetu wanaangalia miaka 100 mbele wakati sisi unarudi nyuma miaka 10.
 
Mbona hawawaambii wachina wasijenge?

Mbona ulaya ma fly over yamejengwa na maroute 69?

sisi tukitishwa na enjioo za ajabu ajabu tunafyata mkia
 
Mbona hawawaambii wachina wasijenge?

Mbona ulaya ma fly over yamejengwa na maroute 69?

sisi tukitishwa na enjioo za ajabu ajabu tunafyata mkia

Tinker mi nakushukuru kuleta mada hiibilibtuwasute hawa wasomi uchwara wanaokaa kwenye vivuli za NGO ili kutetea masilahi ya mabwana zao
 
Hapo ndo nampenda Dr Slaa na Dr Magufuri, ni wazalendo wa kweli wanaojali maslahi ya Tanzania zaidi kuliko sifa toka kwa Wazungu.
 
ninapinga hii barabbara kujengwa hapo serengeti. kuna hiyo pesa kwa nini wasiipeleke kwenye project za kuongeza umeme uwe wa uhakika?
 
Mkuu hapo sio kweli. Kama ungejua madhara wanayopata wanyama wa Mikumi kutokana na uwepo wa hiyo barabara,husingeandika hayo juu. Wanyama wengi wanakufa sana kutokana na uwepo wa barabara hiyo na kutokana na raia kutozingatia sheria na alama za kwenye kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi.

Kwenye suala la wanyama kuzoea au kuadapt mazingira fulani,ni kweli. Ila kumbuka wao pia wana tolerance limit ambayo ikipitwa ndiyo mambo ya extinction au kuwekwa katika Species Red List ya IUCN. Kumbuka wanyama wengi duniani wametoweka baada ya tolerance limits zao kupitwa kwa kiasi kikubwa. Mfano maarufu ni Dinosaurs.

Hapa simaanishi kuwatetea wanyama na kuwasahau wanadamu,la hasha. Ninachokitetea na uwepo wa win-win situation kwa sisi wanadamu na kwa wanyamapori. Kwani kila upande unategemea upande mwingine kwa kiwango kikubwa. Wanyamapori wanatupa mapato na aesthetic values. Nao wanatutegemea sisi kwa survival yao kwa njia ya kuwatunya na kuwajali.

Hivyo ni vyema kufikiria pande zote.

kuna faid ana hasara ya kila kitu...............hatuwezi kuwa kwenye lindi la umasikini kwa kuchelea kitu ambacho kwacho faida yetu ama yetu si sawa na gharama yeke kwetu
 
Mkuu sijaongea siasa ila wewe ndiyo uko kwenye siasa. Mimi nimeangalia uhalisia in a broad spectrum na kujiuliza je ingekuwa Tanzania ni Japan, UK au USA na inataka kupitisha barabara kwenye mbuga zake, je nani angefungua mdomo wake kuuliza.

Nyie akina NZI nawaona more or less ni vibaraka wa serikali ya Kenya ambao munatumika kwa viji pesa kidogo munavyopewa kwenye NGO zenu. Bahati mbaya mumekosa ajira ya serikali kutokana na ufinyu wa ajira kwa hiyo mumeamua kuwa malaya wa akili zenu. Muko tayari kutumia akili zenu dhidi ya mambo halisi ili kuwaridhisha mabwana zenu wa Kenya.

Kenya wanajenga Airport karibu na Mlima Kilimanjaro upande wao, Kenya wana hoteli zaidi ya 20 za nyota tano kwenye mbuga ya Masai Mara lakini hamna anayeona environmental abuse upande wao. Lakini Tanzania ilipojenga Bilila Lodge Kempiski tukaambiwa tume disturb eco system ya wanyama.

Juzi wamezindua ujenzi wa bandari ya Matrillion ya Shillingi kwenye ukanda wa Lamu ili kuweza kuvuta biashara ya mizigo toka Ethiopia na South Sudan. Wenzetu wanaangalia miaka 100 mbele wakati sisi unarudi nyuma miaka 10.

Kwa mtazamo huo I can't reason no more with you!!
 
kuna faid ana hasara ya kila kitu...............hatuwezi kuwa kwenye lindi la umasikini kwa kuchelea kitu ambacho kwa faida yetu ama yetu si sawa na gharama yake kwetu

Umenena vyema. Kwamba kuna faida na hasara ya kila kitu.
Lakini lazima kuwepo na namna ya kuuwianisha faida na hasara hizo; tena kwa upana zaidi ni lazima kuwepo na namna ya kuweka utaratibu wa kuhakikisha hasara hazizidi faida hata siku moja. Sasa kwa tafiti zilizofanyika pale Serengeti zimeonyesha ile barabara kwa kupita katika route iliyokuwa imependekezwa ingekua na hasara zaidi kwa taifa na wanyama kuliko barabara ambayo ingepita kwenye alternative route ambayo ilependekezwa na tathmini ya madhara ya mradi kwenye mazingira na jamii.
 
ndugu zangu, dr JK ametumia busara kuachana na project hiyo.
hivi mradi wa treni unaweza linganisha na serengeti?
mimi naona reli ya kati ambayo inamanufaa zaidi ya hiyo ya serengeti imetushinda. pia tazara imekufa....
serengeti ni mradi mkubwa zaidi ya hiyo miradi ya kenya na kwingineko duniani....
ukiweka treni serengeti hakutakuwa na migration ya wanyama tena, hivyo itakufa.
alternatively treni na barabara zaweza pitishwa katika mkoa mpya wa simiyu na hapo maanake ni faida zaidi.....
bravo jk!!!!!!!!
 
Nani kakudanganya jk yupo kwaajili yakuwaletea nyinyi maendeleo? Isitoshe haji kuwaomba kura zenu tena
 
Serengeti Highway ijengwe, na ukweli ni kwamba tunapoteza muda kusemasema maneno badala ya kupeleka magreda huko! Hakuna mahali popote dunuiani ambapo watu waliona umuhimu wa kiuchumi katika kufanya jambo wakaacha mradi huo eti kulinda nyumbu na mamba. Ukisikilza sana maneno ya watu ipo siku utakuwa hufanyi kitu. Reli na/ama barabara kuunganisha Arusha na Mara ni mpango mzuri kiuchumi. Peleka magreda huko leo. Maneno maneno maneno mpaka lini?

Hivi watanzania tutajifunza lini kuwa maneno maneno yana ukomo wake wa tija? Kwenye soka--maneno maneno maneno nothing doing in the field; haya: Economics--maneno maneno maneno inflation inahit 20%.

Eti Kenya is the strongest economy in East Africa! Kisa? they are taking action wakati sisi , ambao in reality ndio tunatakiwa kuwa strongest economy kwa sababu ya endowments, tunaendelea na maneno maneno maneno. Damn it! Peleka magreda Serengeti leo!

Kuna ndugu anajiita Inzi anasema tutaathiri eti tolerance level ya wanyama--kwa hivyo panaweza kuja hatari ya wanyama kutoweka. Wanyama wenye akili wata-adapt, wajinga watatoweka kama dinasour, ndege dodo na wengine. Sisi wenyewe ni wanyama, na ndo tupo katika process ya ku-adapt hivyo. Jenga serengeti tupunguze dhiki kwa watu wa mikoa ya ziwa na kutunisha mapato ya taifa letu kwa ujumla tubaki hai!

Ndugu Inzi (inzi?) hili jina litakuwa si la kweli tu. Anyway, Sijui una habari kuwa Kenya kuna mbuga ya Wanyama inaitwa Tsavo, na kwamba kuna barabara ya lami na reli vinakatiza mbuga ile? Unadhani kwanini Wakenya hawajang'oa ile reli na kubomoa ile barabara vitokavyo Mombasa kwenda Kisumu kama kweli wanajali sana kuhusu hizo tolerance level za wanyama?

Of course lengo la kuunga mkono ujenzi wa barabara za Serengeti si kwa ajili ya kuwakomoa wakenya au kulipa kisasi eti mbona wao wamejenga kupitia Tsavo. Sababu kubwa ni kwamba Tanzania ina maslahi makubwa ya kiuchumi katika hiyo njia ya Serengeti. Basi. Tha't it.

Mkuu hapo sio kweli. Kama ungejua madhara wanayopata wanyama wa Mikumi kutokana na uwepo wa hiyo barabara,husingeandika hayo juu. Wanyama wengi wanakufa sana kutokana na uwepo wa barabara hiyo na kutokana na raia kutozingatia sheria na alama za kwenye kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi.

Kwenye suala la wanyama kuzoea au kuadapt mazingira fulani,ni kweli. Ila kumbuka wao pia wana tolerance limit ambayo ikipitwa ndiyo mambo ya extinction au kuwekwa katika Species Red List ya IUCN. Kumbuka wanyama wengi duniani wametoweka baada ya tolerance limits zao kupitwa kwa kiasi kikubwa. Mfano maarufu ni Dinosaurs.

Hapa simaanishi kuwatetea wanyama na kuwasahau wanadamu,la hasha. Ninachokitetea na uwepo wa win-win situation kwa sisi wanadamu na kwa wanyamapori. Kwani kila upande unategemea upande mwingine kwa kiwango kikubwa. Wanyamapori wanatupa mapato na aesthetic values. Nao wanatutegemea sisi kwa survival yao kwa njia ya kuwatunya na kuwajali.

Hivyo ni vyema kufikiria pande zote.
 
Ni matumaini yangu kuwa JK hupata nafasi kusoma mambo katika JF. Na kwa tumaini hilo naandika sentensi hizi hapa sasa.

Mara ya kwanza kukuona JK ulikuja kumtembelea mtu kwenye gazeti la serikali la Daily News--sometime in the late 1980s. Mimi nilikuwa pale kumtembelea rafiki yangu Reginald Mhango.

First impressions ziliniambia ulikuwa mtu very soft spoken, mpole, charming katika maongezi, and of course very handsome. Hilo kila mtu analijua. Tatizo letu ni kwamba upole wako unatu-cost.

Start taking tough decisions. Jenga barabara ya Serengeti. Achana na hizo environmental hogwash za wakenya. This is our country. We make decisions about what we want to do. Nobody here makes decisions for what is done in Kenya. They make their own decisions. Tushinndwe kuunganisha mikoa productive na bandari through a cost effective route eti kwa sababu nyumbu zitashindwa kwenda Kenya? Nonesense!

This is a ploy to keep our nation second-rate economically, na hizo nyumbu ni kisingizio tu. Wabomoe reli inayotoka Mombasa kwenda Kisumu na kile kipande kinachokuja Moshi kulinda Tsavo tuone, kama kweli mazingira ni muhimu kiasi hicho kwao.
 
Back
Top Bottom