Wito: Hoja za Kisheria za TLS, Prof. Shivji na wengine wote kupinga IGA, zisijibiwe Kisiasa kwa maneno matupu!, zijibiwe Kisheria kwa Vifungu!

Ivi ni nani alikuwa na HAKI KISHERIA kuandaa BOQ ya mkataba wa BANDARI?. Ktk normal tendering mtoa kazi (TANZANIA) ndio alipaswa kuandaa sifa za mbia (DP WORLD) anaetaka kumpa bandari na mbia alikuwa na jukumu la kuridhia matakwa ya mtoa kazi.

Ktk mazingira hayo mtoa kazi (TANZANIA) hatukutegemea aanze kuukana umiliki wa bandari zake Kwa (1) Kukabidhi majukumu yote ya Bandari zake Kwa mbia (2) kumpa bandari Kwa muda usio na ukomo (3) kulazimika kubadili sheria zake za ulinzi wa RASILIMALI za Taifa na kuweka zile anazotaka mbia (DP WORLD) (4) Kuondoa hadhi ya Mahakama zako kutatua migogoro ya mkataba huo na kuhamishia nchi za nje na (5) Kujiondolea haki yako kama TAIFA HURU (SOUVERAIN STATE) kufanya chochote ktk ardhi yako mpaka mbia (DP WORLD) aridhie.

Mambo hayo hapo yamenirudisha kutafakari MILA NA DESTURI ZETU wa TANZANIA na hata WAAFRIKA wengine linapokuja swala la familia A inapoombwa kuozesha bint Yao Kwa familia B. Katika hatua hii ni familia ipi Huwa na jukumu la kuandaa matakwa (masharti) ya kumtoa bint kwenda familia B??

Nijuavyo mm familia yenye Binti (TANZANIA) ndio huweka orodha ya mahitaji ambayo kama yatatimizwa na familia ya waposaji (DP WORLD) ndipo bint hutolewa na kuolewa na waposaji (DP WORLD). Kwa nn ktk MKATABA huu kadiri tunavyo somewa vipengele vyake vyote vinaonesha sisi TANZANIA ndio tuna COMPLY ktk matakwa ya DP WORLD wakati Mali ni yetu sisi?

HOJA YANGU NI JE?? MKATABA HUU TULIANDAA SISI WENYE MALI AU ULIANDALIWA NA WATAKA MALI KISHA SISI WAKATULETEA TU TUSAINI?

Kama ni ivo inaleta mashaka makubwa sana juu ya UADILIFU NA UWAJIBIKAJI wa WATAALAM wetu ktk kuandaa mkataba huu kiasi imekuja kugundulika hata power of attorney aliyotoa Mh Rais Kwa Waziri Mbarawa kusaini mkataba huu pia ilikuwa batili. Ni AIBU KUBWA kwetu kama NCHI (TANZANIA).
 
Ipo wazi namna Issa Shivji professa wa Sharia za kilatini alivyoeleza namna huu mkataba ulivyo na mapungufu makubwa.

Naona WanaCCM wametapakaa nchi nzima kueleza juu ya nama Rais Samia tangu arithi urais baada ya hayati JPM kufariki kuliko ubovu wa huu mkataba.

Kwa nini hawajikiti juu ya mkataba badala yake wapo busy juu ya uwekezaji na kupamba mafanikio ya Rais Samia?
 
Sasa utamjibu prof mchovu kama Issa ambaye amekubali kulitumiikia kanisa na CHADEMA!
 
Wanabodi,
Mjadala wa IGA ya DPW kupewa Bandari yetu ya Dar es Salaam, unazidi kushika kasi.

Jana asubuhi nilipandisha bandiko hili Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do kuhusu hiyo IGA.

Jana hiyo hiyo ikatokea coincidentally Jukwaa la Wahariri likawaita wahusika wakuu kwenye mkutano na Wahariri, na kujibu maswali ya Wahariri.

Kwanza niwapongeze TEF kwa initiative hiyo, mkutano huo uliotangazwa live na media zetu mainstream na social media, umelisaidia sana taifa katika uelimishaji umma kuhusu jambo hili.

Tangu sakata hili lianze, serikali yetu haijawahi kuwa proactive hata mara moja kwa kujitokeza kuelimisha umma, siku zote, ni inakuwa reactive kujitokeza kujibu hoja.

Miongoni mwa wajibu hoja huo mkutano wa jana ni Wanasheria, kiongozi wa Jopo la Wanasheria, Hamza Johari na Mwanasheria wa Wizara.

Bandiko hili ni wito kwa serikali yetu tukufu na Sikivu, IGA imepingwa kwenye fronts kuu mbili, hoja za Kisiasa, na hoja za Kisheria.

Kwenye hoja za kisiasa ni watu mbalimbali wameibuka ama kuunga mkono ama kuipinga kwa hoja za kisiasa, hoja hizi zikijibiwa kisiasa ni sawa.

Lakini kuna hoja very solid za kisheria zilizotolewa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS, na hoja nyingine nyingi za kisheria zilizoibuliwa na wanasheria mbalimbali, akiwemo Prof. Shivji, Rugemeleza Nshala, Mwambukusi na mawakili wengine wengi.

Hoja hizi za kisheria zimetolewa kwa maandishi zikiandamana na vifungu vya kisheria. Jana nimesikia zikijibiwa kwa kauli nyepesi nyepesi za kisiasa za maneno matupu bila vifungu vya kisheria to back up majibu hayo.

Natoa wito kwa serikali yetu Sikivu, hoja zote za kisheria kuuipinga IGA zilizotolewa kwa maandishi zikiwemo hoja za TLS, Prof. Shivji na Wengine wote Kupinga IGA, zisijibiwe kisiasa kwa kauli tuu nyepesi nyepesi za maneno maneno matupu!, hoja hizi nzito za kisheria, zijibiwe kisheria kwa maandishi zikiambatana na vifungu!.

Kufuatia IGA hii, katika kuiunga mkono, kumejitokeza wanasheria chawa wanaofanya uchawa wa kisheria kuitetea hii IGA.

Na mimi kwa vile ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nami nilitoa hoja zangu kuhusu hii IGA Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! ambazo baadhi mpaka sasa bado hazijajibiwa popote!.
Kwa vile IGA ni utangulizi wa HGA, naomba kuendelea kuwapa matumaini Watanzania kuwa kwa kelele hizi, HGA, itakuwa nzuri.

Serikali Ijibu Hoja.
Paskali
Wakati mwingine kwa jinsi tunavyojadili hoja huwa nadhani hatuwezi mijadala. Wewe ni shahidi ambavyo unakuta umetoa hoja ya kusaidia na wengine wanaleta mambo ambayo ni unrelated kabisa! Hata katika mjadala huu baadhi ya watu wanaibuka na mambo tofauti kabisa hata wakati mwingine huwa najiuliza hivi debates shuleni siku hizi hamna? Angalau enzi zetu karibu kila weekend kulikuwa na debate: mfano, kuwa na baiskeli ni bora kuliko redio, jadili. Au kulima ni bora kuliko kufanya biashara, jadili. Na kutokana na debates hizi watu walijenga skills za majadiliano. Lakini leo hii, ovyo kabisa! Shida ni elimu? Shida ni kuwa na maslahi na upande fulani? Shida ni nini? No wonder wakati wa hapo nyuma vyuo vyetu vilishiriki kwenye maswali ya papo kwa hapo na vyuo vingine na sisi wanafunzi wetu walikuwa wakishika mkia. Labda shida ilianza zamani? Shida nyingine ni kwamba X anaweza kuwa na maoni chanya kuhusu Y na Z akawa na maoni hasi kuhusu Y. Sasa machoni pa watu tutaona X ni muungwana na mzalendo na Z ni mtu mbaya, mchonganishi na hawatakii mema watu wengine. Lakini palipo na watu wengi ni alamost always kwamba baadhi ya watu watakuwa positive kuhusu jambo fulani na wengine negative kuhusu jambo hilohilo, lakini kwa nini tunadhani wale ambao ni positive ni watu wema na wale negative ni wabaya? Sielwei kabisa! Mwisho kama kawaida umetoa points zilizoenda shule. Hongera sana wakili msomi!
 
Wanabodi,
.
Na mimi kwa vile ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nami nilitoa hoja zangu kuhusu hii IGA Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! ambazo baadhi mpaka sasa bado hazijajibiwa popote!.
Kwa vile IGA ni utangulizi wa HGA, naomba kuendelea kuwapa matumaini Watanzania kuwa kwa kelele hizi, HGA, itakuwa nzuri.

Serikali Ijibu Hoja.
Paskali
Hapa nilishauri tuu na sijabahatika kuona popote hoja za kisheria zilizoibuliwa na wanasheria na viongozi mbalimbali zikijibiwa, hivyo nikaelekeza matumaini kwenye HGA, Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA
P
 
Wanabodi,

Lakini kuna hoja very solid za kisheria zilizotolewa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS, na hoja nyingine nyingi za kisheria zilizoibuliwa na wanasheria mbalimbali, akiwemo Prof. Shivji, Rugemeleza Nshala, Mwambukusi na mawakili wengine wengi.

Hoja hizi za kisheria zimetolewa kwa maandishi zikiandamana na vifungu vya kisheria. Jana nimesikia zikijibiwa kwa kauli nyepesi nyepesi za kisiasa za maneno matupu bila vifungu vya kisheria to back up majibu hayo.

Natoa wito kwa serikali yetu Sikivu, hoja zote za kisheria kuuipinga IGA zilizotolewa kwa maandishi zikiwemo hoja za TLS, Prof. Shivji na Wengine wote Kupinga IGA, zisijibiwe kisiasa kwa kauli tuu nyepesi nyepesi za maneno maneno matupu!, hoja hizi nzito za kisheria, zijibiwe kisheria kwa maandishi zikiambatana na vifungu!

Serikali Ijibu Hoja.
Paskali
Ukiacha kutetea DP world tutakuunga mkono
Mkuu JakiDubai, kuna watu wanaandika jf ili waungwe mkono?, utaniunga mkono ili iweje?.
Anyway karibu, hili ni moja ya mabandiko yangu kuunga mkono IGA ya DPW na Bandari zetu, angalia tuu tarehe ya bandiko hili ili ulinganishe na wengine, na ikitokea una uwezo wa kusoma contents, soma contents uone jinsi ninavyoisupport DPW na Bandari zetu!.

Karibu

P
 
Wanabodi,
Mjadala wa IGA ya DPW kupewa Bandari yetu ya Dar es Salaam, unazidi kushika kasi.

Jana asubuhi nilipandisha bandiko hili Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do kuhusu hiyo IGA.

Jana hiyo hiyo ikatokea coincidentally Jukwaa la Wahariri likawaita wahusika wakuu kwenye mkutano na Wahariri, na kujibu maswali ya Wahariri.

Kwanza niwapongeze TEF kwa initiative hiyo, mkutano huo uliotangazwa live na media zetu mainstream na social media, umelisaidia sana taifa katika uelimishaji umma kuhusu jambo hili.

Tangu sakata hili lianze, serikali yetu haijawahi kuwa proactive hata mara moja kwa kujitokeza kuelimisha umma, siku zote, ni inakuwa reactive kujitokeza kujibu hoja.

Miongoni mwa wajibu hoja huo mkutano wa jana ni Wanasheria, kiongozi wa Jopo la Wanasheria, Hamza Johari na Mwanasheria wa Wizara.

Bandiko hili ni wito kwa serikali yetu tukufu na Sikivu, IGA imepingwa kwenye fronts kuu mbili, hoja za Kisiasa, na hoja za Kisheria.

Kwenye hoja za kisiasa ni watu mbalimbali wameibuka ama kuunga mkono ama kuipinga kwa hoja za kisiasa, hoja hizi zikijibiwa kisiasa ni sawa.

Lakini kuna hoja very solid za kisheria zilizotolewa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS, na hoja nyingine nyingi za kisheria zilizoibuliwa na wanasheria mbalimbali, akiwemo Prof. Shivji, Rugemeleza Nshala, Mwambukusi na mawakili wengine wengi.

Hoja hizi za kisheria zimetolewa kwa maandishi zikiandamana na vifungu vya kisheria. Jana nimesikia zikijibiwa kwa kauli nyepesi nyepesi za kisiasa za maneno matupu bila vifungu vya kisheria to back up majibu hayo.

Natoa wito kwa serikali yetu Sikivu, hoja zote za kisheria kuuipinga IGA zilizotolewa kwa maandishi zikiwemo hoja za TLS, Prof. Shivji na Wengine wote Kupinga IGA, zisijibiwe kisiasa kwa kauli tuu nyepesi nyepesi za maneno maneno matupu!, hoja hizi nzito za kisheria, zijibiwe kisheria kwa maandishi zikiambatana na vifungu!.

Kufuatia IGA hii, katika kuiunga mkono, kumejitokeza wanasheria chawa wanaofanya uchawa wa kisheria kuitetea hii IGA.

Na mimi kwa vile ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nami nilitoa hoja zangu kuhusu hii IGA Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! ambazo baadhi mpaka sasa bado hazijajibiwa popote!.
Kwa vile IGA ni utangulizi wa HGA, naomba kuendelea kuwapa matumaini Watanzania kuwa kwa kelele hizi, HGA, itakuwa nzuri.

Serikali Ijibu Hoja.
Paskali
Unategemea majibu gani kutoka kwa
Msukuma
Kibajaji
Jah People
 
Unategemea majibu gani kutoka kwa
Msukuma
Kibajaji
Jah People
Kwa vile DPW ina hoja za kisheria na za kisiasa, hao wawili, Msukuma na Kibajaji ni wazuri sana.
Anza na Kibajaji Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.
Msukuma nae sii haba Msikilizeni Msukuma Star TV ana historia ya kusikitisha sana pia nilimzungumza hapa GEITA: Msukuma amshusha cheo mkuu wa shule kwa kukataa Magufuli club kufanyia mahafali shuleni!
P
 
Wanabodi,
Mjadala wa IGA ya DPW kupewa Bandari yetu ya Dar es Salaam, unazidi kushika kasi.

Jana asubuhi nilipandisha bandiko hili Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do kuhusu hiyo IGA.

Jana hiyo hiyo ikatokea coincidentally Jukwaa la Wahariri likawaita wahusika wakuu kwenye mkutano na Wahariri, na kujibu maswali ya Wahariri.

Kwanza niwapongeze TEF kwa initiative hiyo, mkutano huo uliotangazwa live na media zetu mainstream na social media, umelisaidia sana taifa katika uelimishaji umma kuhusu jambo hili.

Tangu sakata hili lianze, serikali yetu haijawahi kuwa proactive hata mara moja kwa kujitokeza kuelimisha umma, siku zote, ni inakuwa reactive kujitokeza kujibu hoja.

Miongoni mwa wajibu hoja huo mkutano wa jana ni Wanasheria, kiongozi wa Jopo la Wanasheria, Hamza Johari na Mwanasheria wa Wizara.

Bandiko hili ni wito kwa serikali yetu tukufu na Sikivu, IGA imepingwa kwenye fronts kuu mbili, hoja za Kisiasa, na hoja za Kisheria.

Kwenye hoja za kisiasa ni watu mbalimbali wameibuka ama kuunga mkono ama kuipinga kwa hoja za kisiasa, hoja hizi zikijibiwa kisiasa ni sawa.

Lakini kuna hoja very solid za kisheria zilizotolewa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS, na hoja nyingine nyingi za kisheria zilizoibuliwa na wanasheria mbalimbali, akiwemo Prof. Shivji, Rugemeleza Nshala, Mwambukusi na mawakili wengine wengi.

Hoja hizi za kisheria zimetolewa kwa maandishi zikiandamana na vifungu vya kisheria. Jana nimesikia zikijibiwa kwa kauli nyepesi nyepesi za kisiasa za maneno matupu bila vifungu vya kisheria to back up majibu hayo.

Natoa wito kwa serikali yetu Sikivu, hoja zote za kisheria kuuipinga IGA zilizotolewa kwa maandishi zikiwemo hoja za TLS, Prof. Shivji na Wengine wote Kupinga IGA, zisijibiwe kisiasa kwa kauli tuu nyepesi nyepesi za maneno maneno matupu!, hoja hizi nzito za kisheria, zijibiwe kisheria kwa maandishi zikiambatana na vifungu!.

Kufuatia IGA hii, katika kuiunga mkono, kumejitokeza wanasheria chawa wanaofanya uchawa wa kisheria kuitetea hii IGA.

Na mimi kwa vile ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nami nilitoa hoja zangu kuhusu hii IGA Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! ambazo baadhi mpaka sasa bado hazijajibiwa popote!.
Kwa vile IGA ni utangulizi wa HGA, naomba kuendelea kuwapa matumaini Watanzania kuwa kwa kelele hizi, HGA, itakuwa nzuri.

Serikali Ijibu Hoja.
Paskali
Mjumbe usisahau kuwa Waraka sasa uko kwenye Ilani ya CHADEMA, mbowe anawauliza Rombo na Peramiho kama wanamuunga mkono Samiaaaaa au wanaunga mkono Maaskofu? Of course watasema Maaskofu. Hii ndiyo ilikuwa nia ya Pd Charles Kitima kada wa CHADEMA, amefaulu.

Shivji ni Marxist, 100% totally against private capital. Si ni sawa na kuwaomba ng'ombe machinjioni wampigie kura mchinjaji?

TLS hawana msimamo hawajui kama wanakuja au wanakwenda. Laana iliwakamata tangu pale walipochagua Wasalito kama fatmakarume na tundulissu kuwa Rais wao. Kumbuka Rais wa sasa ni Mwanasheria rasmi wa CHADEMA, yeye na Mtobesya aliyemshinda jamaa
HS walikuwa na tegeme
kote kote.

Bado Dr Slaa na Dr Kitima, hawa ni PhD wa Canon Law na Sacred Theology, respectively, zote ni strong on Family Law huku kwa Walei, hawajui uwekezaji. Slaa washamtimua wao wenyewe maadili. Dr Kitima ni kada wa CHADEMA kama nilivyoeleza hapo juu.

If you remember, Fr Kitima ni kijiji kimoja Singida na tundulissu Wanyaturu hawawi jirani na asiye ndugu). Fr Kitima alikuwa invited Main Speaker wa
Mkutano wa Temeke Bulwagi lakini hakuja, raia wa kawaida nao hawakuja. Ilikuwa wawe laki moja kama alivyotangaza Slaa (na kuiombea hela Diaspora na kuipewa hela tosha) badala yake wakaja watu 800 watoto wa kindimu na Wasukuma (ni eneo lao, wengi wala hawajui Kiswahili).
 
Mjumbe ngoja nikusaidie kufuta tongotongo zako zimekukubika rindi.

1. Iko kwenye article 28 kila mmoja anategemea cha mwenzie, siyo cha kwake. Dubai wanataka waone kuwa huyu anayesaini kwa TZ ana kibali cha kusaini huu mkataba, hawajui ana mikataba gani mingine.

2 hadi 6 kamwulize mtu kama Slaa au tundulissu anayatafutactumehuru aende Dibai aombe tumehuru. Dubai yote ninmali ya Sultani, hata DPW ni yake. Sisi ni Jamhurivya Muungano wa Tanzania, wao siyo. Again, it is none of our business under Article 28. By the way, hata sisi hawakuweka jina la shahidi wa Mbarawa, nao Dibai hawatolalamika kwa vile wanalindwa na Art.28.

Swali la 5 landrights amgalia kwenye definitions.

Swali la 6 kuhusu Shivji huyu ni mwanaharakati wa Karl Marx, Nihilist, yaani Mkomunisti. Mosi, hajui asemalo kwa vile si fani yake (Professor Asad alifafanua), lakini muhimu zaidi ni kwamba hapendi uwekezaji kwa ujumla, hevis a Marxist. Sawa ni Profesa, lakini ni Profesa wa nini? Ushamuona Kortini hata siku moja? Unajua kitabu chochote "cha Kiprofesa" alichotunga? PhD yake aliandika kitabu "The Class Struggle in Tanzania", wapi na wapi?

Nikupe jibu umpe Shivji: naam, DPW wana haki ya kupewa ardhi na kila watakachoomba ili mradi ufanikiwe, sisi tuna wajibu wa kuwapa.

Lakini nao wana wajibu wa kuwekeza $500m ambazo hatuna na kuleta computer systems ambazo sisi hatuna, na kutafuta biashara Kongo na Rwandaburundi ili mwisho wake bandari ilete shs 2.6b/= badala ya 600m/=. Atafupisha meli kukaa ili igeuze kesho yake badala ya kugeuza wiki ijayo kama ilivyo sasa. Hayo ni majukumu makubwa, ni wajibu wao kutupa, sisi tunasubiri bulungutu, mwambie hilo Shivji au la sivyo akugee $500m kama anazo.

Aidha, SGR na Mwendokasi watapata biashara nzuri Kongo na Rwandaburundi. Huku nako TANESCO atapata biashara nzuri kwa SGR; na hilo mwambie Shivji.

Kuhusu sheria ipi itumike mie mikuulize swali. Tuna bomba la mafuta toka Uganda kwenda Tanga: mafuta ni yao bomba ni la Wafaransa sisi tumetoa njia tu. Mafuta yanaenda China, ndiye atayelipa. Hii ni rasilimali ya nani? Tutumie sheria yetu au ya Uganda au ya China au ua Ufaransa? Wacha ubinafsi, biashara za kimataifa lazima ziwe win-win mufaidi wote, kwa nini wewe huwaoni wengine?

La mwisho ni swali la kitoto. Kwani, Man U walipomnunua Ronaldo je uliona tangazo lao huku wskitsfuta tenda ili James Ng'ombeyapi mshambuliaji wa Mwadui FC ili naye atoe ushindani? Au, kama Sekali ikiamua tununua ndege ya Boeing, utataka tutangaze kimataifa hadi Burundi na Ukraine, wakati mtengeneza Boeing ni mmoja tu yuko USA? Si unaenda kwake moja kwa moja kama maniyu walivyomfuata Ronaldo moja kwa moja?
 
Hili jambo halikupangika vyema. Ndio maana hawawezi kuwa na majibu hayo ya kisheria.

Tuanza na makosa tu ktk hiyo nyaraka;
1. Ile power of attorney ya mh. Rais, inavyosomeka ni kwamba inampa Waziri Mbarawa kusaini kwa niaba ya Tz na Dubei. Sasa hilo wanajibuje? Kwamba ilikosewa?
2. Hiyo IGA, wahusika wote wa upande wa Dubei, hawaeleweki, majina, vyeo, kuna saini tu. Ni kina nani?
3. IGA ni kati nchi na nchi, Sisi Rais kaonekana kwenye nyaraka, Waziri, kaonekana, na kuna sehemu PS wa wizara kaonekana, wao yupo mkurugenzi wa bandari (DP WORLD), hii ni kampuni tu. Wa Dubei wako wapi?! Unajibuje hilo ..
4. Power of Attorney upande ule alopewe huyo Mkurugenzi wa bandari Dubei, kapewa na nani?! Ukiisoma unaona juu tu, stamp ya Government of Dubei. Ni nani katika serikali ya Dubai, kampa hiyo nguvu,? Cheo na majina na signature, havipo? Mbona sisi Mh Samia kaonekana. Unajibu hili?
5. Zile hoja za huyu mwekezaji kupewa Land Rights na sheria za ufidiaji kinyume na sheria zetu za Ardhi, unazijibuje?!
6. Alisema Prof. Shivji, wao DP World wamepewa haki zote za mkataba, sisi Tanzania tumechukua wajibu wote wa mkataba. Yeye haonekani ktk kipengele chochote akiwa na wajibu. Ni nini hiki?!
7. Wanasema wakienda usuluhishi huko S. Afrika , sheria inayotumika ni "Laws of England". Hii inakinzana na sheria zetu zote. Unajibuje hilo?!
8. Mchakato wa tender ulitangazwa kwa tangazo lipi? Waweke wazi,

Mambo ni mengi sana.

Hili jambo ni zito.

Comprehensive Points
 
Back
Top Bottom