Wimbo wa matusi redioni!

Sir Good

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
1,031
406
Muda mfupi uliopita kuna kituo cha redio kimepiga wimbo wa matusi, wimbo huo ni wa bongofleva lakini wa muda kidogo. Kwenye wimbo huo sauti niliyoijuwa ni ya Soggy Doggy, sauti nyingine sikuzitambua. Ni matusi mazito yaliyoelekezwa Mawingu fm!
 
Kiukweli media zetu maadili yameshuka sana .....binafsi nimesikia leo jioni nyimbo ya Joh Makini (pengine bado mpya kabisa) akitaja neno f.u,c:k live na redio Clouds wakaupiga kama ulivyo ......pengine radio wamepitiwa bahati mbaya lakini leo nimemdharau sana Joh Makini kwa kulazimisha kurap kwa kiingereza na kutamka neno hilo ktk verse ambayo angeweza kutamka maneno mengine mengi bila kutukana (tena kwa kurudiarudia) kinyume na maadili yetu.......hata mbele radioni huwaruhusu upuuzi kama huu ....

CC TCRA
 
Last edited by a moderator:
Clauds ndo wamepiga huo wimbo?

Mpaka sasa sijajuwa hii ni redio gani kwani hawaongei zaidi ya kupiga muziki wa bongofleva ya miaka ya nyuma ila naendelea kuisikiliza mpaka niijuwe.
 
Wana Jf,hata vituo vya tv kama TBC wanaonesha picha za matusi kabisa !

REJEA SWALI: ELEZEA TAFSIRI NENO "MATUSI".
 
Je,TCRA wanatafsiri ipi kuhusu picha za matusi na maneno ya matusi kwenye vyombo vya habari ?

CC TCRA shujaa Pasco
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom