chuwaalbert
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 3,598
- 2,115
Inaonekana alionywa siku ya ufunguzi wa mradi wa Maji Nyamazugo...Kwani walisema arejeshe? Au serikali imezidai
Inaonekana alionywa siku ya ufunguzi wa mradi wa Maji Nyamazugo...Kwani walisema arejeshe? Au serikali imezidai
Yes of course...akiwemo Mwigulu Nchemba aliyeidhinisha fedha hizo zikatwe kodi huku akijua fika kwamba zilikuwa fedha za wizi.Itakuwa vizuri na wale walio idhinisha haya malipo washughulikiwe...
Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Nani ambaye ameshafungwa?MTOA RUSHWA NA MPOKEAJI RUSHWA WOTE WANAHATIA HIVYO NAYE AFUNGWE KAMA WENZIE
Mkuu macho huwa makavu huku mdomo wa chini na juu ikipishana.Halafu Polepole akiulizwa kama CCM ndiyo iliharibu nchi anajiuma uma.
Habari wanaJF,
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja amerejesha rasmi Serikalini fedha alizozipokea kutoka kwa James Rugemalira mnamo tarehe 12/2/2014 katika mgao wa Escrow ambazo ni kiasi cha Shilingi Milioni 40.4 ili kukwepa kuendelea kuandamwa na kashfa hiyo.
Ngeleja amesema kuwa ''Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo'' Ngeleja.
'Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi.
Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW nimeamua kuchukua hatua.
Kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuna harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.
Nimerudisha fedha hizi ili kulinda maslahi ya nchi yangu na heshima ya chama changu, Serikali, wanasengerema, familia yangu na heshima yangu.
Nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha kiasi cha Milioni 40.4 serikalini.
KWANI HIZO FEDHA NI ZA TRA.Chonde chonde TRA, mpigieni hesabu ya riba.