Wilfred Lwakatare: Mrejesho kutoka mahabusu Segerea

Hapa ndio umenena kuanzia leo nakukubali wewe ni embe

5: NIMEKUTANA NA SHEIKH PONDA

Milima huwa haikutani lakini binadamu wanakutana. Ndivyo sakata la ugaidi lilivyonifikisha gereza la Segerea na huko nikajikuta nawekwa selo moja na ‘mjukuu wangu’ Issa Ponda mtoto kutoka Kigoma. Issa Ponda ni kiumbe wa mwenyezi Mungu wa aina ya pekee. Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea mtu mithiri ya Ponda si mtu wa kuchukulia mzaa kama ninaouona ukichezwa hapa kwetu. Ni mtu ambaye fikra zake, ubunifu alionao kichwani na katika vitendo, hulka zake, nasaha zake, ushawishi wake, ujengaji hoja zake, uchaji wa Mungu wake, uswalihina wake na vingine vingi ni watu wachache sana unaoweza kukutana nao wakiwa navyo vyote kwa mpigo.

Ponda tofauti na namna mfumo unavyomchukulia, ni mtu ambaye angetumika vyema kwa kusikilizwa sehemu kubwa ya mawazo yake na yakafanyiwa kazi ipasavyo, nina uhakika mambo mengi tunayoyaona yana mitafaruku ya kidini yasingelikuwepo.

Tatizo wakubwa wanamuangalia kwa taswira ya upande mmoja ya kumuona ‘mkorofi, mchochezi’. Sijui na ndio maana nauliza, hivi ni mamlaka gani ya juu na yenye kauli ndani ya nchi hii imewahi kukaa na Ponda kwa karibu katika misingi ya kuheshimiana kwa dhati na kusikilizana ili kujua ana mawazo na mitizamo gani kwa masuala mbalimbali yaliyolalamikiwa na baadhi ya waislamu walio wengi?

Nimeishi naye zaidi ya siku 60 selo moja kwa masaa 24 karibu kila siku na masaa mengi tukiwa wawili tu, mimi na yeye. Ni mdadisi wa kupenda kujua, na ukisha mwelewesha ni mwepesi wa kuelewa na kujenga fikra mpya. Hivyohivyo siyo mchoyo wa kuyabania maarifa aliyonayo na elimu kubwa ya kidini aliyobahatika kuipata.

Alinielewesha kuwa kwenye dini ya kiislamu mtu anapokuwa amefikia kiwango cha kuitwa U-Ustadhi kwa lugha ya haraka inayoeleweka na wengi ni sawa na U-profesa.Hakika Sheikh Ponda ni ‘profesa’.

Nilipata fursa ya kujadiliana naye pia mambo ya msingi yanayolikabili hivi sasa Taifa letu. Moja wapo ni nguvu nyingi zisizo na sababu zinazotumiwa na polisi kushughulika na watu kama sisi ambao hata rungu hatuna. Nguvu kubwa inayotumika ya kumpeleka Ponda au Lwakatare mahakamani ili kesi itajwe tu na kurudi Segerea kulala ni sawa na kumlipa daktari wa muhimbili mishahara mizuri ya miezi miwili. Magari nane na mapikipiki kujazwa mafuta,ving’ora barabarani,askari polisi zaidi ya hamsini kuvunja shughuli nyinginezo kwa siku nzima, barabara kufungwa na mengine kuzuiwa wakati wa kupita n.k Mikwara yote hiyo ya nini?

Mfungwa mmoja aliyesoma kwa kiwango fulani alipoletwa kulala kwenye selo yetu na kuikuta mada hiyo, alichangia hivi, “kawaida ya mtu yeyote anayelazimisha aonekane mbele ya wakubwa zake kwamba anafanya kazi ni lazima atengeneze mazingira yanayomfanya aonekane kweli anafanya kazi”. Kisha kasema hivi “nyie waheshimiwa ili wale waliowafungulia tuhuma za ugaidi na uchochezi lazima watoe taswira ya nje kwa umma kuonesha kuwa ninyi ni watu hatari sana na mkipewa upenyo wowote mnaweza kusababisha maafa makubwa sana wakati wowote kwa taifa. Kwa ufupi wanataka umma uwahukumu kinadharia kwamba mnahusika na tuhuma mlizoshtakiwa nazo hata kama mahakama haijazipitia tuhuma zenyewe kuona zina uzito gani.”

Nilimuelewa vizuri sana na kukubaliana na huyo mfungwa maana vyombo vyetu hivi vya dola wakati mwingine vinapenda kutumia nguvu nyingi sana katika jambo dogo sana kwa sababu tu za kuridhishana na makundi fulani au kulinda nafasi zao za kazi ambazo hawazimudu.

Jambo jingine lililoangukia katika mijadala yetu ni hii migogoro ya makundi ya kijamii na hata mauaji na maumizano yanayojitokeza mara kwa mara. Sheikh Ponda alitoa changamoto moja muhimu ambayo naona ina mashiko sana. Alisema hivi; huko uswazi (mitaani wanakoishi watu wengi kwa kubanana) ambako nyumba moja wanapanga na kuishi zaidi ya watu hamsini, mchanganyiko wa waislamu kwa wakristo, mbona hakuna ugomvi? Mbona akina mama humo ndani waislamu kwa wakristo wanaachiana watoto kwenda sokoni? Mbona wanaazimana vijiko na masufuria? Mbona wanapeana mboga bila kuulizana? Ponda akatumbukiza na utani pia kuwa “mbona humu selo ukileta chakula alichopika mama Frank siulizi na wala wewe chakula anachoniletea mama Mariam naona unabugia tu bila maswali yoyote?

Na mimi nikamwambia mbona ukiamka saa tisa usiku ukaanza swala zako za sunna mpaka alfajiri wakati wa ‘Azanna’ na kisha swala zote tano za ‘faradhi’ za siku nzima na lakhai zake mbilimbili humu humu ndani ya selo havijaingiliana na ibada zangu za ‘Tumwabudu Mungu wetu?’ Selo yetu ndio msikiti wetu na ndilo kanisa letu. Haya mambo chanzo na chimbuko lake ni nini? Hayawezi kuwa yanatengenezwa na kundi maalum la watu kwa malengo maalum?

Swali hili la mwisho likanikumbusha somo moja tulilowahi kufundishwa kipindi fulani nilipokwenda Ujerumani kwa mafunzo ya ‘Strategic Planning’. Katika kipengele kimojawapo cha mafunzo hayo nakumbuka kuna kitu mwalimu alikiita ‘Power Winning and Maintaining Strategy’, kwa tafsiri nyepesi ‘mkakati wa kuupata utawala na kuulinda’.

Katika mkakati huo nakumbuka alitwambia, kuna wakati watawala fulani wanapoelemewa na mambo au jambo wakakosa majibu mbele ya watawaliwa wanaotaka kujua kulikoni ili kuzima mambo hayo aidha ni kutumia nguvu na fursa zilizopo kumshughulikia kinara mmoja anayeonekana kimbelembele kuhoji.

Mkisha mziba mdomo kwa njia zozote zinazowezekana walio nyuma yake wataufyata tu! Njia nyingine ni kuibua au kufanya jambo fulani kubwa bila kujulikana linaloweza kusaidia kuwahamisha watu kifikra toka jambo jingine lililopo ambalo ni hatarishi zaidi kiutawala.
Njia nyingine ni ile iliyotumika tangu ukoloni ya ‘watawanye uwatawale’ (Divide and rule policy).

Ukiwapa nafasi au fursa watawaliwa wakakaa, wakapanga wakaelewana na nyie mpompo tu mkiwaangalia, jua siku watakapozua ajenda ya kushughulika na wewe, ujue umekwenda. Dawa ni kuwafanya siku zote wasielewane kwa kuwagonganisha vichwa wenyewe kwa wenyewe tena kwa mambo madogo yasiyo hitaji gharama kubwa na nguvu nyingi. Tulijadiliana sana na kwa urefu na Sheikh Ponda juu ya mambo haya lakini hatukupata jibu la mwisho na kwa bahati mbaya au nzuri Mungu akawa amezisikia dua zake na sala zake za masaa zaidi ya 18 kila siku akawa amechomolewa Segerea na kuniachia Sello No. 3. Najua Mungu atatukutanisha tena Inshallah! Ila, isiwe tena Segerea au Keko ili tuhitimishe mada hiyo.

Siku moja kabla ya kusomewa hukumu yake na Hakimu Nongwa (9/5/2013) tulijadili sana hukumu yake kwamba inaweza kuwa ya mwelekeo gani na maamuzi yapi. Panga pangua ilishindikana kueleweka mambo yatakuwaje kutokana na mazingira yaliyokuwa yakiizunguka kesi yenyewe. Mawakili wake walikuwa wameifanya kazi yao vyema bila kubakiza punje ya shaka. Lililokuwa likimpa faraja zaidi na kesi yake ni kusikia kwamba huyo hakimu ni mama mlokole, ameokoka. Hiyo ilikua ikimpa moyo sana kwamba atahukumiwa na kupewa haki yake sawa na lile lililozungumzwa na kuwasilishwa mbele ya hakimu Nongwa.

Nilimuuliza endapo hukumu itamuweka katika mazingira ya kumkata makali yake ya kazi ya utetezi anayoifanya na wakati huohuo upande wa pili wa ‘system’ ukamtaka aanze kutoa ‘Ushirikiano’ atafanyaje? Sheikh Ponda aliniambia kuwa haki huwa hainunuliwi wala kuombwa bali hudaiwa. Alisema atakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa yeyote yule anayezungumzia utoaji na upatakanaji haki.Na akasema mdomo na nafsi vilivyodhamiria kuzungumzia na kuitafuta haki huwa havifungiki kwani vikifungika hata hiyo amani haiwezi kuwepo.

Nikiwa ndani ya selo nilimsikia Sheikh Ponda akimwaga mistari yake redioni baada ya kuhukumiwa. Kwa mara nyingine nikazidi kumuaminia Sheikh Ponda kwamba ni mmojawapo ya watu wachache tulio nao hivi sasa nchini wanaoweza kutembea na kuishi ndani ya maneno yao.

Lipo jambo moja muhimu ambalo tulikubaliana na Sheikh Ponda tulijadili na kulifanyia kazi kwa nia ya kuwanusuru watu wanaosota jela bila sababu endapo tungeliachiwa na kuwa huru uraiani. Namtafuta kwenye simu hayuko ‘reachable’. Nikishampata tukashauriana na likaonekana linatekelezeka, nitalitoa hadharani.

6: USHAURI WANGU MDOGO KWA VIONGOZI WETU WA DINI.

Mimi ni mtu mdogo sana na muumini wa kawaida ndani ya dhehebu la KKKT. Lakini natambua kanisa ni waumini na wajibu mkubwa wa kila muumini ni kuhakikisha anatimiza wajibu wake kama kanisa la Mungu linavyoelekezwa kupitia maandiko matakatifu ya Biblia. Wajibu mmojawapo sisi kama waumini ni kuonyana ( Ebr. 10:24 – 25).

Nawaombeni viongozi wetu wa dini zote wakristo kwa waislamu mtimize wajibu wenu mliokabidhiwa na Mungu, Imeandikwa kwa dini zote kwamba kila mmoja bila kujali wadhifa wake atahukumiwa sawa na matendo yake. Nawaomba simamieni na kuuzungumza ukweli(hata kama ni mchungu) mbele ya watawala na hata watawala watarajiwa.Ninyi mmepewa mamlaka na Mungu ya kuonya, kukemea, kuelekeza na kubariki na ndio maana watawala wote wanawaogopa na kuwaheshimu. Wengine huenda ninyi bila ya kuwatambua hutafuta njia za kujikomba kwenu ili wakipate wanachokitafuta.Yasemeni wazi na kuyahoji hata yale machache yanayoonekana au kusikika pasipo kificho.

Muulizeni Mheshimiwa Rais huyo waziri wake anayezungumzwa kila siku kwamba mchana kweupe alisema anao maadui zake wawili ambao ni waandishi wa habari na angewashughulikia, Rais analisemaje hilo? Maadam ni ninyi, nina uhakika Mheshimiwa Rais atajibu na atachukua hatua stahiki.

Binafsi nawaombeni kwa heshima na taadhima muache kuwa vuguvugu (si moto si baridi-Ufunuo wa Yohana 3:15-16) Baadhi yenu acheni kuogopa vivuli vyenu kwa maana ya kuhofia kunyimwa upendeleo au misaada ya serikali (i.e misamaha ya kodi) na baadhi kuutumia mwanya huo vibaya. Kama maandiko yanavyosema JIKANENI WENYEWE.

Lazima mtambue hawa jamaa wakati mwingine huenda wanaitumia fursa hiyo kama chambo cha kuwanasia pindi wanapokua wana taarifa zenu zote za fursa ya misamaha iliyotumika vibaya. “Mnapaswa kushuhudiwa mema na watu walio nje…” (1 Tim 3:2-9)
Binafsi nawaomba msiwalee wala kuwabeba wale wote wenye dhamira chafu na nia mbaya ya kutaka kuyatumia madhehebu yenu kukidhi matakwa binafsi kwani wanachafua taswira zenu nzuri za madhehebu yenu mbele ya waumini wenu na umma kwa ujumla.

Lakini zaidi ya yote ni imani yangu mimi binafsi kwamba madhehebu yenu ni makubwa na yana mtandao mkubwa na wenye nguvu ndani na hata nje ya nchi.Kama inawezekana tumieni mtandao wenu kuisaidia serikali ambayo vyombo vyake vinaelekea kushindwa kuwabaini wahalifu wachache wanaoelekea kuchafua na kuivuruga amani tuliyoizoea ndani ya nchi yetu. Kwa bahati nzuri nimesoma na kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba IGP Mwema amezishauri taasisi za kidini kuanzisha ‘ulinzi shirikishi ndani ya misikiti na makanisa’. Kama mambo serikali ya CCM imeyafikisha hapo, tumieni fursa hiyo kuziomba taasisi makini mnazozifikia nje na ndani ya nchi.

"
 
Pole kamanda...Hii ni shule tosha kwa wanasiasa mahiri waonao chipukia...shule tosha sana hii..
 
Daaah inatia uchungu kwa kweli...

Nilikuwa namuona Lwakatare kama mtu wa kawaida sana, lakini baada ya kuisoma hii makala, nimekubali kuwa huyu jamaa ni kichwa. The guy is genius, CHADEMA mtumieni huyu mtu, atawavusha 2015.

Pia nawapomgeza CCM hasa Mwigulu Nchema kwa kuweza kutambua TISHIO halisi kwa CCM ndani ya CHADEMA ni pamoja na uwezo mkubwa wa kupanga mikakati wa huyu jamaa Lwakatare.
 
" Mrundikano mkubwa magerezani wa wafungwa na mahabusu unasababisha hata huduma ziwe mbovu. Wapo wafungwa hawana sare za gereza wanavaa kitu kinachoitwa ‘nusu mlingoti’, kauka nikuvae, sare zilizochanika kiasi cha kutia aibu.Na kwa kuwa hata sera za uendeshaji magereza nyingi ni zilezile za ‘vichwa vya ki-CCM’ (chama dhaifu,wabunge dhaifu na serikali dhaifu) hakuna akili inayoweza kubuni namna ya kuitumia kiufanisi nguvu kazi kubwa iliyojaa magerezani. Ndani ya gereza kuna kila aina ya fani na vipaji lakini vimelala tu. Kama vile CCM, hawazai na hawana watoto nyumbani, huwezi kuamini watoto lukuki waliorundikwa Segerea bila utaratibu mzuri wa kimalezi na kimakuzi hata kama baadhi yao ni wakorofi na wahalifu. Tutake, tusitake hawa ni taifa la leo na la kesho.Hawa ni nguvu kazi yetu ya nchi ,hawa wanahitaji kukunjwa wangali wabichi. "



Maoni yangu: Wanaotutawala kwa sasa ni kama mzee kikongwe. Akili imegota, imefika mwisho na hakuna jipya HATA KAMA tungewapa miaka mingine 20 ya kututawala. Akili yao iko ktk box ambalo hakuna anayejua namna ya kutoka humo. Si Magereza peke yake lakini ni kila nyanja.

Wapo watu wanasema kikongwe akizeeka sana akili yake inarudi kuwa ya mtoto mdogo!

Pole sana Lwakatare na wote tunaoathirika na mfumo huu.

KIM
 
Ni wakati sasa wa wanasiasa kujifunza jambo katika makala haya, hasa mazungumzo ya Sheikh Ponda na Lwakatare!

Kuna kitu hapo cha kujifunza!
 
Salaam wakuu,

Mheshimiwa Kamanda W. Lwakatare aka PRISON GRADUATE ametoa makala yake ya kwanza iitwayo "MREJESHO KUTOKA MAHABUSU"

He stand a good chance to write a book "Maisha ya Lwakatare gerezani na kesi ya kubambikiwa"
 
‘siasa hazina rafiki wala adui wa kudumu’ bali ni kuangalia nani anawezesha kupenya vikwazo ili kuwezesha kufika salama ninakokwenda (kwa maana ya kuingia Ikulu). Ukishaingia ndani ya mjengo mambo mengine ni akili kichwani, utajua unachemsha vipi kichwa lakini muhimu kuliko yote si tayari umo ndani na unachezea ndani?

Nisingependa kuona kuona zinatumika njia zisizo rasmi ilimradi tu tufike ikulu......zaidi nisingependa kuona tunaingia ikulu bila plan tukitarajia akili kichwani baada ya kuingia, hilo haliwezi kutuvusha ukizingatia changamoto mhimu tulizonazo wananchi. Master Plan ya kuingia ikulu tunatakiwa kuwa nayo sasa na si kujichanga akili mara baada ya kuingia badala ya kuanza kutekeleza majukumu kadri ya sera zilivyouzwa.
 
Ujumbe muhimu toka gerezani according to Rwakatale ambao nami nimeukubali natamani chadema wauweke katika vitendo "Wamenituma niwaeleze, kwa kipindi kilichobaki, ‘chonde! Chonde! acheni kugombana, kurumbana na kufukuzana. Tumieni kipindi hiki kujenga mshikamano utakaowezesha kukisuka kikosi cha ‘Real Madrid’ au ‘Manchester United’ ya siasa za Tanzania ili uchaguzi ujao CCM walazwe chali-mwanguko wa kifo cha mende! Wanasema CCM ni wepesi kama nyama ya maini, wakibanwa kwenye kumi na nane hawana ujanja wataachia tu , tatu bila!!!"
Yafanyieni kazi haya pia

 
Du. Mpaka nimenogewa. Natamani kiwe kitabu, japo kisifanywe biashara bali kiwe chanzo cha maarifa ya kuing'oa ccm...
 
Nakupa pole sana Kamamda, CCM waanaelekea pabaya na wasiopobadilika kitakufa na hakitaweza kufufuka kamwe.Kuhusu kushindwa uchaguzi 2015 kwa wabunge hiyo ni MUST,wasipobadilika Uraisi nao kwa heri.Dhambi zinazofanywa na wabunge wa CCM bungeni hazitasamehaewa kamwe.
CCM wanajiona kuwa wao no wawindaji tu kila siku ,na wananchi wawindwaji. wakumbuke " Wakati muwindaji anapokuwa muwindwaji na muwindwaji anapokuwa muindaji,maisha huwa magumu sana kwa yule muwindwaji
" WHEN THE HUNTER BECOME THE HUNTED ,AND THE HUNTED BECOME THE HUNTER.LIFE BECOME COMPLICATED".
 
Shukrani za pekee zimwendee Mwigulu Nchemba kwa kuanzisha uzushi ambao utalipeleka taifa letu kwenye ukombozi wa kweli kwa kuwatesa watu wa Mungu bila hatia. It is a blessing in disguise lakini tutamuomba Mwigulu hatuonyeshe ushahidi aliotwambia anao hata kama mahakama haitamtaka afanye hivyo maana aliyasema kupitia vyombo vya habari na sasa atumie njia hiyo hiyo. What a shame to our Police forces for accepting silly allegations by Mwigulu. Ingekuwa vizuri kama Mwigulu akishindwa kutoa ushahidi ambao ni sound akajitanguliza mbele ya sheria ili akahukumiwe tofauti na hapo atakutana na nguvu za umma. People's poweeeeer!
 
6: USHAURI WANGU MDOGO KWA VIONGOZI WETU WA DINI.

Mimi ni mtu mdogo sana na muumini wa kawaida ndani ya dhehebu la KKKT. Lakini natambua kanisa ni waumini na wajibu mkubwa wa kila muumini ni kuhakikisha anatimiza wajibu wake kama kanisa la Mungu linavyoelekezwa kupitia maandiko matakatifu ya Biblia. Wajibu mmojawapo sisi kama waumini ni kuonyana ( Ebr. 10:24 – 25).

Nawaombeni viongozi wetu wa dini zote wakristo kwa waislamu mtimize wajibu wenu mliokabidhiwa na Mungu, Imeandikwa kwa dini zote kwamba kila mmoja bila kujali wadhifa wake atahukumiwa sawa na matendo yake. Nawaomba simamieni na kuuzungumza ukweli(hata kama ni mchungu) mbele ya watawala na hata watawala watarajiwa.Ninyi mmepewa mamlaka na Mungu ya kuonya, kukemea, kuelekeza na kubariki na ndio maana watawala wote wanawaogopa na kuwaheshimu. Wengine huenda ninyi bila ya kuwatambua hutafuta njia za kujikomba kwenu ili wakipate wanachokitafuta.Yasemeni wazi na kuyahoji hata yale machache yanayoonekana au kusikika pasipo kificho.

Muulizeni Mheshimiwa Rais huyo waziri wake anayezungumzwa kila siku kwamba mchana kweupe alisema anao maadui zake wawili ambao ni waandishi wa habari na angewashughulikia, Rais analisemaje hilo? Maadam ni ninyi, nina uhakika Mheshimiwa Rais atajibu na atachukua hatua stahiki
.

/Bernad MembeWasaidizi wa Bernad Membe mwambieni ajibu hoja hii ya Lwakatare kwa sababu toka mwanzo uchunguzi wa jukwaa la wahariri walisema membe ahojiwe ana kesi ya kujibu kutokana na matamshi yake na matukio wanayofanyiwa waandshi i.e KIBANDA
 
6: Ushauri wangu mdogo kwa viongozi wetu wa dini.

Mimi ni mtu mdogo sana na muumini wa kawaida ndani ya dhehebu la kkkt. Lakini natambua kanisa ni waumini na wajibu mkubwa wa kila muumini ni kuhakikisha anatimiza wajibu wake kama kanisa la mungu linavyoelekezwa kupitia maandiko matakatifu ya biblia. Wajibu mmojawapo sisi kama waumini ni kuonyana ( ebr. 10:24 – 25).

Nawaombeni viongozi wetu wa dini zote wakristo kwa waislamu mtimize wajibu wenu mliokabidhiwa na mungu, imeandikwa kwa dini zote kwamba kila mmoja bila kujali wadhifa wake atahukumiwa sawa na matendo yake. Nawaomba simamieni na kuuzungumza ukweli(hata kama ni mchungu) mbele ya watawala na hata watawala watarajiwa.ninyi mmepewa mamlaka na mungu ya kuonya, kukemea, kuelekeza na kubariki na ndio maana watawala wote wanawaogopa na kuwaheshimu. Wengine huenda ninyi bila ya kuwatambua hutafuta njia za kujikomba kwenu ili wakipate wanachokitafuta.yasemeni wazi na kuyahoji hata yale machache yanayoonekana au kusikika pasipo kificho.

muulizeni mheshimiwa rais huyo waziri wake anayezungumzwa kila siku kwamba mchana kweupe alisema anao maadui zake wawili ambao ni waandishi wa habari na angewashughulikia, rais analisemaje hilo? Maadam ni ninyi, nina uhakika mheshimiwa rais atajibu na atachukua hatua stahiki

penye red membe apelekwe mahakamani akajibu hizi tuhuma ni nzito na waandshi wa habari wanang'olewa kucha na meno kila sku .i.e kibanda huyu mdmu akajibu hizi tuhuma msiwabambkzie chadema hawauski kabsa
 
This is a very very strong message to the Rulers(Not Leaders) of this country!
Huu ni ujumbe mzito sana kutoka kwa PRISON GRADUATE kwa Watanzania wote.

Mimi huwa ni mgumu sana wa kutoa machozi, lakini ujumbe huu yamenitoka. It's a natural feeling which makes you automatically cry! Sijui kina Mwigulu Mchembe, Nepi Nauye,Steven Wassira wao wameupokeaje ujumbe huu! Ujumbe huu ni chachu kwa Watanzania kuwapeleka mbele zaidi katika kudai Haki na Uhuru wao ambao wamepokonywa na Serikali Dhalimu ya CCM!

Ujumbe huu umenifanya nimkumbuke Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere(RIP) kwamba umoja,upendo na mshikamano aliotuachia Mwalimu,Watawala wa chama cha CCM kwa maksudi wameamua kusambaratisha kila kitu kwa tamaa zao za kundelea kukaa madarakani.

CCM baada ya kuona kwamba kwa sasa hawauziki tena na wameshapoteza mvuto kwa Watanzania wameamua kutumia mbinu za kinazi(Hitler) za kukamata,kutesa,kujeruhi na kuua ili kujiimarisha kwenye madaraka!

Watawala(Rulers not Leaders) wa CCM wamejisahau kabisa na bado wanaota ndoto za mchana za kutaka kuitawala Tanzania milele, jambo ambalo haliwezekani! Labda tuwakumbushe CCM na vibaraka wake kuwa historia huwa haifutiki,bado inaturejesha huko nyuma kwamba walikuwepo watawala kina Hitler, kina Botha,Idd Amin,Bokassa,kina Mobutu,kina Milosevic na madkiteta wengine wa dunia waliowahi kutawala WAKO WAPI???????

Rais Kiwete, Nnepi Nauye,Mwigulu Mchembe, Steven Wassira, IGP Mwema, RPC Kamuhanda, Kinana, Nchimbi na wengineo mlio CCM huu upepo wa mabadiliko hamutaweza kuubadilisha. Tunajua mnajipanga KUCHAKACHUA RASIMU YA KATIBA na hatimaye mje kupata KATIBA YA CCM, you must be wasting your time. Where is USSR you guys? It's no longer there! Imesambaratika na hakuna aliyeweza kuzuia mabadiliko hayo.

Changes are there and must be there. You better accept these changes or else.....................!
 
Hii habari imeniliza machozi ni kweli watu kama Sheikh Ponda ni wakusikilizwa. Ila kumwita Prof nadhani Lwakatare umekwenda mbali.
Hilo ndilo lilonifanya niache kuendelea kusoma hii tamthilia. ngoja kuna picha nizitafute alipofanya press conference huku ana rungu la Polisi, hapa Lwakatare amenitibuwa kabisa, hajui hata waliobahatika kuongea na Osama ni mtu mkarimu sana na anayejuwa kucheza vyema na akili za watu mpaka wengine wanajilipuwa ili waende peponi na mabikira 100.
 
Back
Top Bottom