Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,886
- 41,996
CHADEMA imedhihirisha kuwa inachukia matendo maovu, na kwenye uovu wamedhihirisha hawana subira wala simile, hawaangalii anayefanya hilo ni wa chama chao au mtu wa nje.
CHADEMA imejitofautisha sana CCM, chama ambacho siku zote kimekumbatia majizi, mafisadi, wala rushwa, wakwepa kodi, alimradi tu mwovu huyo awe ni miongoni mwao. Kama ni kada, kiongozi wa chama, haguswi.
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, mpigania haki, mtu aliyenyoka kwa matendo na kauli, mtu jasiri na mkweli wa nafsi, ndugu Tundu Lisu, hivi karibuni ametoa kauli ya kukemea uovu wa kutumia pesa kuupata uongozi ndani ya chama chake. Mambo hayo huwezi kuyasikia ndani ya Serikali ya CCM wala ndani ya CCM yenyewe, japo inafahamika wazi namna baadhi ya mawaziri wanavyowahonga wanaofanya vetting, ili tu waendelee kuteuliwa na Mh. Rais. Huwezi kuisikia kauli kali ya kukemea uovu kutoka Serikali ya CCM wala CCM yenyewe dhidi ya viongozi na maafisa wa serikali wanaofanya ufisadi, rejea ripoti za CAG. Huwezi kusikia kauli kama ya Lisu kutoka CCM wakati wa kura za maoni, japo tunafahamu jinsi rushwa inavyotembea kwa wajumbe wakati wa kura za maoni.
Tunafahamu kuwa hakuwezi kutokea serikali au chama chochote cha siasa chenye watu watakatifu wote, chama cha hivyo hakipo. Lakini tunatofautisha ubora wa vyama na Serikali kwa kuangalia serikali au chama kinachukua hatua gani dhidi ya waovu.
Hongera Lisu. Umeonesha njia.