Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

Status
Not open for further replies.
Abunuwasi kwa taarifa yako, huyo dhaifu anawajua wauza unga, majina anayo likiwemo la mwanae, ndio maana kakaa kimya hataki kuwashughulikia.

Dr Slaa ni kati ya watu ambao hasemi kitu bila kukifanyia utafiti, najua kama kweli kasema haya ushahidi anao, mpelekeni mahakamani muone mtakavyoumbuka.

Ikulu sasa imekuwa pango la wahuni na wauza madawa ya kulevya, hakuna heshima tena, shame on you Abunuwasi and your father Mr/dr Dhaifu.
 
Abunuwasi.... u mean it uko ka abunuwasi...

Umeandika KIUDAKU ZAIDI.... not a professional way... too low ... Even ungekuwa na points u mixed up urself...

--- UANDISHI.... 1% ...
 
Hebu pitia hii vizuri tena.

Rais Jakaya Kikwete aiweka nchi rehani kumuokoa mwanae asinyongwe China.

September 7, 2012

Ningumu kuamini lakini ni UKWELI

Taarifa za upelelezi makosa ya jinai nchini China zinasema tarehe 01/7/2012, vijana wawili wenye asili ya kiafrika walikamatwa katika uwanja wa ndege wa Hong Kong usiku, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi za Tanzania Bilioni nne, mkuu wa kitengo chakuzuia mihadarati cha uwanja wa Hong Kong Yiu-Kwong anawataja kuwa ni Ridhiwani Jakaya Kikwete na Abdalah Aman Mohamed

Mnamo tarehe 2/7/2012 majira ya saa nne (4:13) za usiku hapa Tanzania, rais Jakaya Kikwete alipokea simu kutoka kwa mtanzania mmoja aitwae Philip Malmo ambae ni balozi wa Tanzania nchini China, Taarifa muhimu baada ya salamu ilikuwa ni Ridhiwani amekamatwa uwanja wa ndege wa Hong Kong na madawa ya KULEVYA,

Kwa haraka, rais akamuuliza vipi suala hili limeshafika hapo ubalozini? Akajibiwa hapana ni mimi na kaimu wangu tu ndie tumepata taarifa hii mda huu, bado hatujaliifanya lakiofisi, tunasubiri ushauri wako mheshimiwa.

Rais alikata simu huku hali yake usoni ikibadilika gafla, ilichukua kama dakika 20 hivi rais akiwa kimya hata kutikisa macho tu hatikisi, baadae akainua simu na kumpigia rais Hu Jintao wa China, Waliongea kwa mda mrefu yapata dakika 40 hivi, na walikonekana kama hawakubaliana kitu fulani katika mazungumzo yao. Baadae simu ikakatwa,

Akampigia simu Malmo nakumwambia suala hili walifanye kwa siri kubwa asijue mtu yeyote, naaweke maandalizi yawe tayari yeye anajiandaa kuja kulimaliza, kasha akampigia tena simu Hu Jintao na walitumia dakika 16 tu akainuka nakusema, vijana, mwambie SD53 aandae ndege haraka kwa safari ya China,

Gari ya kirai namba T 435 CDR aina ya Landcruiser nyeusi iliingia nakuwabeba watu watatu akiwemo rais Jakaya kuelekea airport, kama dakika 13 ikafika airport, tayari ndege ilishaandaliwa na palikuwa na maafisa watatu, wote tuliingia katika ndege ile isipokuwa yule dereva wa gari ambae aligeza mjini, hiyo ilikwa sasa ni saa 7:43 za usiku.

Tarehe 3, majira ya saa nane za usiku kwa china, tulifika China, hakukuwa na aina ya mapokezi yoyote ya kiserikali, na baada ya kushuka tulimkuta Malmo na msaidizi wake wakitusubiri, Malmo alikuwa tayari ameshaandaa hoteli lakini kulingana na tukio lilivyo tulikubaliana tusilale na tukammwambia mheshimiwa rais amwambie Hu Jintao kuwa ameshafika. Rais alitekeleza hilo na baada ya dakika 15 maafisa watatu wa china walifika nakujitambulisha kuwa wenyeji wetu, wakatuchukua hadi alipo Hu Jintao katika moja ya ikulu ya Hong Kong,

Kikao chao kilichukua masaa manne, na jambo kuu walilokuwa wanakubaliana ni mashariti ya kumuachia, Hu Jintao alihitaji jambo moja tu, kwamba nini serikali ya china itapata kwakumwachia huru Ridhiwani? Kilichomvutia Hu Jintao naakamua muachia Ridhwani ni ahadi ya makubaliano ya Rais Kikwete kuwa ataipa China fursa ya uwekezaji wakudumu kusini mwa Tanzania ambako kumegunduliwa mafuta, gesi, na makaa ya mawe.

Kwakuwa sera ya china kwa sasa ni "Now we are going to Africa", ilisaidia sana kukubali ombi hilo la jk.

Majira ya saa 11 alfajiri kwa saa za china, Ridhiwani aliletwa akiwa katika gari dogo, nakupokelewa na jk huku wakikumbatiana wote WAKILIA. Jk na Jintao wote kwapamoja wakamuonya sana nakumwambia ameliaibisha taifa la Tanzania, lakini kwakujitetea akasema sio yeye, ila inawezekana yule kijana waliyesafiri wote kutoka Ethiopia ndie mwenye mzigo huo.

Majira ya saa 12 za asubuhi tukaondoka kurudi Tz.

Taarifa hii ni yakweli mimi nilikuwemo kwenye msafara huo,
Hutaki unaacha, hulazimishwi kuamini.
Source ni mimi mwenyewe.
Jason Bourne
 
Yan una kanusha kitotoooo tuhuma nzito kama hizi! Kweli wewe umepanic sana!

Umeshindwa hata kuthibitisha kuwa ni uongo! Yani umeongea kwa kupanic tu na matusi wala hayajasaidia kufuta tuhuma za huyo ndugu yako!
 
Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.

Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:

Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.

Hakuna anaeweza kukushangaa na maelezo yako ya mke anamtetea mumewe maana hizo ndo story zako abunuasi.. Jina lako linajieleza.. waambie waliokutuma wajipange upya na JF si mahali pakutafuta kujisafisha. Kama wamehisi kuchafuliwa na/au yalosemwa ni uzushi wanajua pakutafuta ukweli... kama hawajui ni wapi inazidi kudhihirisha uwezo wa dhaifu, familia yake na nyumba ndogo zake.
 
Karibu Riziwani bora umekuja kujisafisha!!! Dubai si unakwenda kwa sababu kuna yale mambo yetu umenunua kule a.k.a vitega uchumi!!!? Hata upayuke vipi Dr. Salaa humuwezi!!! Mmefungua kesi, hola, mmesema vile hola!!! Bisha yale magari, PUMA, hotels na yale mengine namezea!!! Wewe uu msafi?
 
Kama Dr Slaa ni muongo kwaniniNape alitisha kumshitaki kwa kusema ccm imeleta kontena la silaa, na akataka alipwe Bilioni 3 na shilingi 1. ila baada ya Chadema kusema wameshafungua mashtaka dhidi yake juu ya kauli aliyosema kuwa chadema inachangisha pesa huku ina pesa nyingi kutaka kwa wafadhili wa nchi za nje, Nape akaghairi kufungua kesi na kusema amemsamehe.
 
Abunuwasi nakuona upo hewani!!! Jibu maswali unayoulizwa!!! Kumbe wamekutuma leo!!! Watahangaika ila cha moto Dr. anawaonesha!!! Mkimsikia unapata matumbo ya mwendo kasi tu!! Ha ha ha ha!!
 
Tunashukuru sana Dr.Slaa hakumtaja lakini naona unajitokeza na kusema siyo mimi ,siyo yeye. Kwani Ridhiwani ndo mtoto pekee wa vigogo hapa nchini? Mwisho wa mwezi
 
Hii habari ya mtoto wa mkuu kukamatwa na madawa nami nlisikia kitambo ila nkapuuza
alipoibuka dr Slaa na kusema sina shaka kuna ukweli ndani yake
Dr slaa alisbaibuka na ishu ya ufisadi akatukanwa na kusemwa sana na hata press release zikatolewa kupinga
leo hii tumeshaona mafisadi kibao aliowataja na hata skendo ya EPA nk
kwa hili ukweli utajulikana soon.
 
Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.

Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:

Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.

Hizo ni tuhuma nzito, si dhani kama ingekuwa kweli Riz1 ama ndugu yake hajafanya kitu wangekuwa wameshatinga mahakani mara moja au kuomba akanushe na kuomba msamaha mbele ya umma. Kwa misingi hiyo kwa asilimia kubwa yawezekana aliyoyasema Dr. Slaa ni yakweli.
 
AIBU KUU,yani umejiunga jana kwa ajili ya kuja kukanusha ukweli?

  • A%20S%20angry.gif
    • :eek:hwell:
      • :bowl:

umeniuzi,umenikela,umenitia hasira,umeniboa na umenitia kichefuchefu na kinyaa
:angry: :mimba:
  • :shut-mouth:
    • :eek:hwell:

:dance:

A%20S%2027.gif

:grouphug:

A%20S%20103.gif
 
Jamani huruma haka ka form one, si munaona kanatetemeka kujibu hata thread. Enzi zangu tukiwa shule angekuwa ashaenda kunifulia nguo na jion angenibembeleza mpaka mawazo ya kutoswa na demu wa tbr gelos iishe. Sh.....wa.iiiiin. Mswaki
 
kanusha kuhusu yale masaa na namba za gari zilizotajwa.hata EPA slaa alisema uongo!

sasa kama alipatia EPA,ndo kila kitu anachosema ukiamini?..si wewe greatthinker bana.
THINK,REASON,ANALYSE THEN COME TO YOUR OWN CONCLUSION.
 
raise issue,huna adabu umekosa malezi,huwezi kumtukana mtu WA heshima,kama uwongo fungueni mashtaka,halafu we si msemaji wa rIZONE.MODS NAMCHANA JAMAA NIKO TAYARI KWA BANN ,KWA MARA NYINGINE,HUYU JAMAA ANATUMIA MAVI BADALA YA UBONGO,HE CAN NOT UNDERSTAND BEYOND THE VISIBLE MEANING.

You have been banned for 2 weeks. Reason: the ban you searched for. The ban will be lifted on 12th November at 22:00hrs
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom