wikiendi ukweni!...

...umeenda ukweni kuchumbia rasmi, baada ya utambulisho na wenyeji kuwapa muda 'mjisikie mpo nyumbani' , Baba mkwe anakutupia swali la papo kwa papo; ..." eti kijana, iwapo tumepata ajali majini, na uwezo wako kumuoka mtu mmoja tu, utamuokoa nani kati yangu, mama mkwe, mkeo au mwanao?"Ingelikuwa weye ungejibu nini?
huyo baba mkwe lazima ana tu element twa uchawi. Ndio maswali gani hayo ya kumuuliza mgeni? Baba mkwe huyo hana adabu kabisa.
 

...Tulizo,..hili swali limelenga zaidi kwenye kutafuta busara ya mhusika, kulikoni kuangalia Consequences za harakati za kuokoa. Ndio maana nikasema swali hili kila mtu anaweza 'kujikaanga kivyake,' lakini madhali upo ukweli huna budi kujibu vile busara na maamuzi yatavyokuruhusu.

Duh! nimekupata vizuri sana mkuu..Yaani kutokana na mazingira busara yaweza kuzidi ukweli..hivyo kwa wale tunaojifanya tuko'practical' tunaweza kukosa mke ..

Big up mkuu.. Good lesson!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom