Wife hanichangamkii, nimepoteza mzuka naye kabisa

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Ama kweli kuishi na mke kunahitaji uvumilivu Sana

Nimekuwa na mwanamke huyu almost miaka 8, tuna watoto wawili.

Mke wangu ni muajiriwa na analipwa vizuri tu,siku za nyuma tulikuwa tunaishi kwa furaha Sana japo ni mikoa tofauti ila ni ya jirani

Kwa miaka 7 tumeishi bila ndoa Hadi tulipoamua kufunga ndoa ya bomani mwaka huu.

Mke wangu huyu ni mtu mwenye wivu kupindukia na ana asili ya kukaa na kinyongo moyoni Hali inayopelekea tuwe na migogoro ya hapa na pale.

Sasa miezi kadhaa nyuma alikuja mkoa ninaoishi ,akakutana na majirani akapewa umbea kwamba kuna binti wa nyumba ya jirani namla,basi Yeye na majirani wakaweka mtego,wife akaniaga anarudi kwake na hapo tayari tulishagombana,nikamwambia poa kumbe kajificha Ili amkamate yule binti

Sasa nilimpigia simu binti aniletee mboga kutoka sokoni,ile anaingia tu ndani wife nae kaingia kaanza kumpiga yule binti ,bahati nzuri binti akakimbia.

Hali ya mgogoro na wife ikawa mbaya zaidi,nikamwita rafiki angu tukaongea na wife na nikamwomba samahani, tukayamaliza akaondoka.

Sasa tangu wakati huo mawasiliano yamekuwa finyu Sana,nimejaribu Sana kumwomba msamaha lakini naona mwenzangu hataki suluhisho,sina mchepuko na nimeachana kabisa na mipango ya kando.

Hivi karibuni nimekuja kumtembelea wife na kuwaona watoto naona mwenzangu hana time na Mimi na ana tabia ya kukumbushia mambo yaliyopita miezi zaidi ya 5 sasa, hatuna amani,tangu nije hakuna mazungumzo yoyote, hata unyumba sijapewa na nimekosa kabisa mzuka nae.

Nikiri hata yeye na ndugu zake akiwemo mama yake walinikosea Sana ila mi nilisamehe na maisha yakaendelea.

Sasa nashindwa kuelewa huyu mwenzangu anataka nini hasa kama msamaha nilimwomba ila naona bado ana kinyongo miezi zaidi ya 5 sasa hadi furaha na mzuka wa kuwa nae umeniisha kabisa yani tunaishi Ili mradi tu.

Naombeni ushauri nifanyaje Ili huyu mwanamke aache kisirani chache na kuninunia!? Manake nimemvumilia Hadi nimechoka sioni sababu ya yeye kuendelea kununa na kuwa na mawasiliano hafifu na Mimi kana kwamba yeye hajawahi nikosea na nikamsamehe.

Sometimes najiuliza au kazi na mshahara mzuri alio nao ndo unampa kiburi Hadi anione mi mkosaji na kila siku akumbushe makosa yangu..!!?

Ushauri tafadhali.
 
Sikiliza bradha.

Inaonekana wewe ndiye unampenda sana kuliko anavokupenda wewe.

Kama sivyo.
Basi rudi kazini halafu nawe kula kimya kwa muda hata wa miezi mitatu. Uone kama hajakutafuta.

Wana kawaida ya kutikisa kibiriti hasa akiona kuna sehemu kakukamata.

Nina miaka mitano kasoro kwenye ndoa. Kidogo nina ka uzoefu


ASANTE.
Na pole kwa yote, lakini ni mambo ya kupita tuuu mkuu


 
Ndoa nyingi zikishaingia kwenye ishu za kukamatana kwenye uzinifu zinapitia hali hiyo.

USHAURI: Jaribu kumvumilia huku ukionyesha mapenzi kwa watoto na kuwa mstaarabu kwake. Kuwa smart sana, vaa vizuri upendeze na kama una kauwezo badili gari unayotembelea.
 
Kuwa busy na kazi kwa miezi mitatu hivi utaona matokeo.
Kumaliza ugomvi na mtu aliyefanya kosa si kazi, Ila kumaliza ugomvi na mtu aliyefanya kosa kisha kudanganya ni kazi ngumu.

Anachotakiwa kufanya ni kuomba msamaha kwa kumdanganya mke wake. Pia atuombe msamaha sisi kwa kutudanganya pia

Kama ni kweli hakufanya kosa kama alivyo andika hapo aliomba msamaha wa nini? Hua wanasema ukiwa muongo uwe mtunzaji wa kumbukumbu.
 
Yaani hapo Ndugu yangu hata mkeo akikusamehe not this lazima akulipizie Tena visasi vyao huwa Ni vile vya kuliwa na watu wako wa karibu anaweza kuwa Ndugu au rafiki au jirani ..so jipange ki saikolojia mapema ..yaani lazima uchapiwe 😁😁😁
 
Back
Top Bottom