Wadau naomba mnisaidie kudadavua hili jambo ninaliliona.
Kuna mgahawa kuanzia kama miaka miwili nyuma hadi hivi leo huwa ninakwenda kila siku kupata chakula cha mchana au mara nyingine kuchukua takeaway.
Kuna DADA ni mmoja wa wahudumu kwenye huo mgahawa ambao ni mkubwa tu katika huu mji ninaokaa. Huyu dada siku za nyuma alikuwa akiniona nimefika, ananichangamkia na kunitania tania mbele ya baadhi ya wafanyakazi wenzake wa kike utani wa kama vile mimi ni "jamaa yake" ila mimi sikuwa na hisia nae zozote wala kumwambia lolote kutokana na utani utani wake, kwasababu nikawa nachukulia anachoifanya ni utani tu na wala sio serious anachofanya!
Sasa siku za karibuni naona huyu dada kabadilika, hataki ukaribu na mimi wala kuongea na mimi tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma.
Mfano, kuna mara mbili nimefika akaja mezani kunisikiliza halafu, oda ya chakula nikaletewa na muhudumu mwenzake, kitu ambacho kikanionesha ni dhahiri kuna kitu kinachoendelea ndani ya nafsi yake huyu dada.
Naomba kujua ndugu zangu, huyu dada anaweza kuwa amebadilika kwasababu gani?
Nauliza tu, ingawa mimi hili jambo haliniumizi kichwa kwasababu hata sina hisia nae zozote. Na hata kama huyu dada ana hisia na mimi, kwenye huo mgahawa sina mazoea wala ukaribu na muhudumu mwingine yeyote wa kike kusema labda amenihisi nina uhusiano nae kisha yeye ndio akaona wivu au kuwa na kama chuki.
Ahsanteni.