Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?

Nasikia Ephraim Mafuru aliyekuwa Vodacom amehamia TTCL kama Mkurugenzi Mkuu,
Je ni kweli na anaweza kuleta mabadiliko chanya na kuifufua TTCL?
From Kishongo's and Gis posts, not a chance.., tatizo sio CEO au TTCL, tatizo ni mfumo mzima wa nchi yetu ambayo imekosa DIRA
 
Mimi ni mtumiaji mzuri wa TTCL mobile na Landline. Siku moja niliwauliza wafanyakazi wake mbona huduma zenu ni nzuri na rahisi sana na hamjitangazi zaidi ya vipeperushi ambavyo huonekana tu unapoingia katika ofisi zenu????? Sikupata jibu ila niliambulia nyuso za wafanyakazi waliokata tamaa!!!

Kwa zote thread nilizosoma ninachoweza kusema ni MAYOOOO!!! MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!:A S 20::A S 20::A S 20::A S 20:
 
Rostam Aziz na Lowasa siyo shareholders wa Airtel ( Celtel, Zain) ila wako VODACOM na Rostam Aziz alikuwa major shareholder ila sasa nasikia kapunguza share kwa kuwauzia Vodafone

Thanx Mr. boma2000 for a point of correction.

Ni kweli RA na EL wana shares Vodacom na si Zain/Airtel.
Hata hivo bado wako upande uleule wa adui wa KUIANGAMIZA TTCL.

Thanks.
 
Thanx Mr. boma2000 for a point of correction.

Ni kweli RA na EL wana shares Vodacom na si Zain/Airtel.
Hata hivo bado wako upande uleule wa adui wa KUIANGAMIZA TTCL.
Thanks.

ni kweli kabisa ni waangamizaji nwa ttcl na nchi kwa ujumla
 
Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,

  • Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
  • Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
  • Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
  • Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)
  • Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
  • Baadaye TTCL ikanyang'anywa shea zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina shea na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha
  • Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.
  • Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.
  • Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.
  • Mwaka 2007, serikali ikaleta menejinti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.
  • Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.
  • Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)
  • Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzani, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndo wenye mali serikali ni msimamizi tu.
  • Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.
  • TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.
  • Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!
Ala kumbe! Mchawi wa TTCL ni serikali yenyewe! Sasa nimeanza kuuelewa utamu wa kubinafsisha makampuni na mashirika ya serikali yaliyoasisiwa katika awamu ya kwanza na Hayati Baba wa Taifa. Kama ni kweli basi tumekwisha. Sasa sishangai kwa nini Precision ya Mramba inashamiri wakati ATCL iko mbendembende, kumbe siri ni umafia wa wamiliki - ndiyo serikali. Ama kweli tunamkumbuka Nyerere na Azimio lake la Arusha ambalo pamoja na mambo mengine liliwazuia viongozi kufanya Biashara au kumiliki mali kubwakubwa!
maelezo haya yanadokeza kwa nini Tanzania bado tuko maili nyingi nyuma ya wenzetu tuliokuwa sawa au mbele yao kimaendeleo wakati nchi hii inapata uhuru. Hali hii pia inajibu kwa nini sasa miaka 50 tangu tujitawale tumekuwa taifa la mazezeta tuishio kwenye giza totoro kwa kukosekana nishati ya umeme (Uliokuwa tele enzi za Nyerere)huku viongozi wakipiga kelele kuwa uchumi wetu unapaa! Ufisadi ndani ya serikali ya CCM umetuletea shida na matatizo mengi mno, inatisha. Hebu ona , nchi iliyozunguukwa na mito isiyokauka lukuki, upepo, gesi,makaa ya mawe n.k. imeshindwa kabisa kuzalisha umeme wa kutosha kiasi cha kuwakatisha tamaa wawekezaji wa kweli ambao wangeuokoa uchumi wetu? Tunasubiri nini kufanya yale yanayotokea Tunisia, Misri na kwingineko? Watanzania tutabaki punda wa kuwabeba wahuni hawa hadi lini na wapi?
Down with CCM, Down with its entire Leadership. Long live Tanzania's opposition. A luta Continua.
 
Thanx Mr. boma2000 for a point of correction.

Ni kweli RA na EL wana shares Vodacom na si Zain/Airtel.
Hata hivo bado wako upande uleule wa adui wa KUIANGAMIZA TTCL.

Thanks.

Hapo TTCL haiwezitendewa haki hata kidogo
 
hapa shida siyo ttcl mi nadhani shida ni hujuma za viongozi wenye hisa kwenye makampuni mengine ya simu, hawa jamaa wanajua kabisa ttcl ikiacha itawale soko ni nini kitatokea kwa makampuni yao. Mi nafkiri tukipata viongozi wanaojua wajibu wao kwa taifa basi shilika hili litakuwa ni moja ya mashirika wanayojivunia watz.

ttcl wawajibike tu kwanza na simu za mezani nchini, phonebootH .......na kuhangaika na mambo ya internet, hizo ndio kazi za kampuni kama ttcl duniani kote........mambo ya celula makampuni ni mengi popote duniani, usa,japan,uk wote wapo kwenye mfumo nao kueleza............. Na kila mtu yupo huru na hilo hata the great thinkers mnaweza kuanzisha ya kwenu...
 
Strategy, mission and vision of TTCL Tanzania still relies on the old model of business unlike other MPSP who work to ensure they co-exist with the modern environment in case of marketing and stiff competition from outside. TTCL can advance from the old model of service providing to the contemporary way only if the company`s public relations officer would work to adapt with changing environment and from there they can be the leading in providing good services as other companies do.

Jipe nafasi ya kusoma kabla hujabwatuka.

Yaani wewe kwa akili yako unadhani mafanikio ya kampuni yako vested 100% kwa PR Officer bila kujali mipango mkakati ya kampuni husika.
Hizi shule za uandishi wa habari za mtaani ndio zinawafanya kudhani PR ni jambo pekee tunalohitaji for a successful company.

Kuna wadau wameshusha nondo hapo juu, ni asiye mtanzania tu ndio anaweza kuwashutumu TTCL
 
Thanx Mr. boma2000 for a point of correction.

Ni kweli RA na EL wana shares Vodacom na si Zain/Airtel.
Hata hivo bado wako upande uleule wa adui wa KUIANGAMIZA TTCL.

Thanks.
Pole sana TTCL
EL
RA
Serikali
Ukiwa na maadui kama hapo juu, na wako upande mmoja kukuandama suala la kufa is a matter of time.
Muulizeni TANESCO
 
Nasikia Ephraim Mafuru aliyekuwa Vodacom amehamia TTCL kama Mkurugenzi Mkuu,
Je ni kweli na anaweza kuleta mabadiliko chanya na kuifufua TTCL?

Hii hali ya Watanzania wengi kupenda watu wanaojitokeza sana kwenye vyombo vya habari na kudhani ni watendaji wazuri ni kati ya kansa za hatari sana ndani ya nchi hii, na kiukweli hadi sasa inatuangamiza sana. Watendaji wengi wazuri wasiojionyesha sana kwenye vyombo vya habari wanadharauriwa, wale wanaojifanya kujitokeza sana ndio wanaheshimiwa, hii hali ndio inafanya hata kuchagua watu magalasha watuongoze pasipo kupima uwezo binafsi wa utendaji bali kwa kupima porojo zao.

Huyu jamaa watanzania wengi hapa mnamuona ni best just kwa sababu alikuwa anajitokeza sana kwenye vyombo vya habari, kwa taarifa yenu ni kuwa huyu jamaa alitimuliwa kimya kimya Vodacom kwa sababu ya ufisadi mkubwa alioufanya. Huwezi fikiria nani anaweza kuhama vodacom kwenda TTCL kampuni bibi kizee iliyokwishajichokea ? Huyu jamaa aliwekwa kando kimya kimya Vodacom, ndio akasepa TTCL.
 
Shingo kaeleza uzuri sana on the above subject. Hii inaonesha jinsi serikali hii ya CCM ilivyosheheni walafi na wasiokuwa wazalendo, wanataka kuua kila kitu kwa kujinufaisha wao. Ndo maana hata serikali ya Malkia haiwaamini tena, maan wanaijua. Chenji waloiba kupitia Rada Waingereza hawataki kuirudisha kupitia Serikali ya CCM, maana wanajua ikipitia huko washenzi hawa wataila tu!!!???
 
Nilishawahi kufanya kazi TTCL zaidi ya miaka kumi iliyopita chini ya utawala wa Mapunda. Kwa wakati huo tuliamini kuwa ufumbuzi wa matatizo yetu ulikuwa chini yetu wenyewe.

Nimekuwa nikiongea na wafanyakazi wa TTCL wa sasa, wao wanaamini kuwa chimbuko la matatizo ni serikali kupendelea makampuni binafsi. Nikiwauliza ni upendeleo gani? Wanashindwa kujibu. Kimsingi TTCL wanaogoja kivuli chao wenyewe.

Naamini tatizo kubwa ni la uongozi, mzee Said na wenzie wameshindwa kuiongoza TTCL.


Pole sana na endelea kufikiria hivyo.
 
Hi Great thinkers,

I am back again as I promised.

As I have already said ealier and I say it again,the KILLERS of TTCL is the CCM government under leadership of KIWETE and his henchmen. Most of government leaders are either SHARE HOLDERS or CHAIRMAN/CHAIRPERSON/BOARD MEMBERS in Foreign MOBILE operators.We have live examples:
  1. Pius Msekwa,the former Speaker of Tanzania Parliament was Chairman Board of Directors Vodacom Tanzania.
  2. Salim Ahmed Salim,the former AU Secretary General,PM and Minister is ZAIN/AIRTEL shareholder and Board Member.
  3. Joseph Sinde Warioba,the former PM and Minister is ZAIN/AIRTEL shareholder and Board Member.
  4. Rostam Aziz,the MP for Igunga Constituency is Vodacom shareholder and Board Member.
  5. Basil Pesambil Mramba is Board member and shareholder in Zain/Airtel.
This is just a list of some few Government leaders who are fully engaged in Mobile operators business and therefore making all possible means to make SURE that TTCL is no longer there.
About 2 years ago 2009/10 a secret letter from ZAIN to the Deputy Minister(by then Doctor Maua Daftari) was revealed at the Ministry of Science and Technlogy headquarters STATING A STRATEGIC PLAN TO STOP TTCL FROM OPERATING AND EXPAND THEIR TTCL MOBILE PHONES as it will adversely affect other Mobile operators!

The strategic plan was to make sure that TTCL MOBILE network be controlled and limited! In this plan TCRA wa involved in such a way that TTCL can not expand its Mobile phones without the TCRA authority. TTCL was allowed under special LICENCE to expand its network ONLY by 100,000 customers per year! While other Mobile operators are talking of a Customer base of 4m to 6m like Vodacom TTCL have to expand by 100,000 per year. That means, by just simple arithmetic TTCL can achieve a 1m customer base after 10 years!!!.

This can be proved by poor coverage of TTCL MOBILE. There is only one BTS(a Microwave system which connect mobile customers) in most Regions or Districts to cater for TTCL mobile customers. I know one region where there is ONLY ONE BTS!!!!!! Other companies like Vodacom,Tigo,Zain/Airtel have 30-50 BTS systems approximately in the same region.

The cost of 1 BTS ranges between 200-300m Tshs. which TTCL can afford.

I shall come later on more stories about TTCL.

Baasi Mkuu unanitoa machozi! Hivi watanzania tuna laana gani jamani? Yani viongoz wetu wanashiriki kutuhujumu,kuhujumu mali ya umma!
 
ala kumbe! Mchawi wa ttcl ni serikali yenyewe! Sasa nimeanza kuuelewa utamu wa kubinafsisha makampuni na mashirika ya serikali yaliyoasisiwa katika awamu ya kwanza na hayati baba wa taifa. Kama ni kweli basi tumekwisha. Sasa sishangai kwa nini precision ya mramba inashamiri wakati atcl iko mbendembende, kumbe siri ni umafia wa wamiliki - ndiyo serikali. Ama kweli tunamkumbuka nyerere na azimio lake la arusha ambalo pamoja na mambo mengine liliwazuia viongozi kufanya biashara au kumiliki mali kubwakubwa!
Maelezo haya yanadokeza kwa nini tanzania bado tuko maili nyingi nyuma ya wenzetu tuliokuwa sawa au mbele yao kimaendeleo wakati nchi hii inapata uhuru. Hali hii pia inajibu kwa nini sasa miaka 50 tangu tujitawale tumekuwa taifa la mazezeta tuishio kwenye giza totoro kwa kukosekana nishati ya umeme (uliokuwa tele enzi za nyerere)huku viongozi wakipiga kelele kuwa uchumi wetu unapaa! Ufisadi ndani ya serikali ya ccm umetuletea shida na matatizo mengi mno, inatisha. Hebu ona , nchi iliyozunguukwa na mito isiyokauka lukuki, upepo, gesi,makaa ya mawe n.k. Imeshindwa kabisa kuzalisha umeme wa kutosha kiasi cha kuwakatisha tamaa wawekezaji wa kweli ambao wangeuokoa uchumi wetu? Tunasubiri nini kufanya yale yanayotokea tunisia, misri na kwingineko? Watanzania tutabaki punda wa kuwabeba wahuni hawa hadi lini na wapi?
down with ccm, down with its entire leadership. Long live tanzania's opposition. a luta continua.
inauma sana kwa kweli.
 
Najuta kuisoma hii thread. Imeniletea PSYCHOLOGICAL DISTURBANCE! Nchi hii inatuumiza sana na mbaya zaidi hatufahamu kama tunaumizwa, na tukifahamu there's nothing we can do about it.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom