Why Tanzania is top 'beggar' after Iraq, Afghanistan

This has been known by our leaders for years! According to Dambisa Moyo's book Dead Aid, for every $1 received in aid, $13 goes back to the same people who gave you the money.! Now you understand with all the resources we are still one of the poorest country in the world. No country has ever developed because of aid. We take people to Norway to learn how to collect tax, yet Kenya here our neighbor finance more than 95% of their budget and we can just put all those people in bus to go and learn they have able to do it. How can you learn from a person way ahead of you and your neighbor is doing it right! And then someone has the audacity of saying the report does not reflect the truth! You have to accept your problems for you to solve them. He should ask what should be done not refute the report!

Huyu Likwelile sijui ndo alikuwaga mwalimu pale Mlimani?

SAM2000,
Viongozi wetu ni mfano wetu. Ndivyo tulivyo
 
Wanaotoa misaada hawawezi kutuwezesha tujitegemee. Watatuwezesha kuwa soko lao.

We have never learnt to learn. We seem we will never ever, for even our leaders praise themselves for begging.

Cry Tanzania. Mwee......Tubadilike
 
hayo ndio matunda ya safari nyingi za rais! Mungu saidia nchi itoke kwenye makucha ya shetani CCm.
 
I think it is in-material for naibu katibu to cite other countries not mentioned in the list as an excuse of us being beggars. The point is there, even if we rank no 15, it doesnt matter, what matters is what have we be doing with the monies? why this trend for almost 50 years since independency? are there any signs of getting out of this? how are we prepared to produce more from the God given resources?

Kweli Nyani Ngabu, miafrika ndivyo tulivyo. Hili nalo lilikuwa liprofesa la uchumi. Kumbe uchumi wenyewe ni wa kuomba omba! aibu sana!
 
Why TZ is top ‘beggar' after Iraq, Afghanistan Send to a friend
Sunday, 04 December 2011 10:43
digg

begger.jpg
By The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Tanzania, whose aid portfolio has ballooned to over Sh3 trillion (about $2.89 billion) in its 50 years of independence, is currently Africa's top beggar for development assistance, The Citizen on Sunday can authoritatively report today.That level of dependency makes it the third leading recipient of official development assistance (Oda) in the world after war-torn Iraq and Afghanistan.
The American organisation Visual Economics says the once-rich oil exporter Iraq tops the list of beggar nations with donations totalling about $9 billion followed by Afghanistan and Tanzania, whose development alms are nearly $4 billion and $3 billion, respectively, according to 2010 figures.

But the government yesterday questioned the accuracy of the report, saying there were many other countries that received much more in foreign assistance than Tanzania. Finance and Economic Affairs deputy permanent secretary Servacius Likwelile told The Citizen on Sunday that countries like Israel and Egypt receive a substantial amount of assistance from the US annually, and wondered whether the report included military aid.
"We need to know the criteria used in compiling the report. What I know is that the United States provides a great deal in assistance to countries such as Israel and Egypt, but they are not even on the list," Dr Likwelile said.Commenting on the trend, some experts said that while begging for the top two is understandable, it is incomprehensible for Tanzania, which is not only rich in both natural resources and human capital, but has also been stable and peaceful since independence.

They wondered why, despite the staggering amounts of aid the country has been receiving for five decades, the country remains one of the poorest in the world with a third of the population living below the poverty line.
Some attributed the limited value for money on aid to bad governance, a view supported by the 2009 Human Rights Report, which states that "senior government officials estimated that 20 per cent of the government's budget in each fiscal year was lost to corruption".

"We are still poor despite being among the top recipients of aid in the world…this is because of poor leadership and management of the aid provided. Worst of all, we are poor managers of our God-given resources," said Ms Saumu Jumanne, a lecturer at the Dar es Salaam University College of Education.
Saying Tanzania could forge ahead without aid, she added that foreign assistance has not helped to alleviate poverty as only a trickle reaches the targeted groups. Sometimes, she noted, even aid for orphans is misappropriated.

"What is needed is to make strategic plans and be focused on exploiting our immense natural resources for the public good. So far, the abundant natural resources we have benefit a few Tanzanians and their foreign partners. Our education, which is supposed to guide us in transforming our nation, is grossly inadequate.

Agriculture is not being taught at primary level yet 85 per cent of the populace depends on the sector for survival. That is having our priorities wrong."
Economist Honest Ngowi said foreign aid has not made Tanzania economically independent because the dynamics of the Oda industry are not geared at ending the dependency syndrome. He blames both donors and the authorities for aid's failure to address the country's development shortcomings, saying he does not foresee an end to the vicious circle of begging in the near future.But Dr Likwelile differed with this point of view, saying foreign aids had made "a lot of difference" in the water, education and health sectors.

Visual Economics, which claims to be the world leader in unravelling complexities of economic and financial data, says Africa has five of the world's top 10 aid recipients, Asia four and the Middle East one. Using data obtained from the Organisation of Economic Cooperation and Development (OECD) sources, it shows that Africa has 12 of the top 20 development assistance beggars in the world.
"The top recipient of developmental aid is Iraq, with $9.115 billion in donations. Number two is Afghanistan, with $3.951 billion in donations received. Number three is Tanzania, with $2.811 billion received in donations. Number four is Vietnam, with $2.497 billion in donations," Visual Economics notes in a publication titled How Developmental Aid Flows Around The Globe.

"Number five is Ethiopia, with $2.422 billion in donations. Number six is Pakistan, with $2.212 billion in aid received. Number seven is Sudan, with $2.104 billion in aid received. Number eight is Nigeria, with $2.042 billion in donations received. Number nine is Cameroon, with donations of $1.933 billion received. Number 10 is Palestine with $1.868 billion in donations received," it adds.

The US is the number one developmental aid donor with $21.787 billion donated followed by Germany and France, which donated $12.291 billion and $9.884 billion, respectively. Despite close relations between Tanzania and the US, the country is not on the list of the top 10 recipients of American aid. Topping the list are Iraq ($4.266 billion) and Afghanistan ($1.459 billion).

According to the OECD figures, Tanzania received about $39 million (about Sh66.3 billion at current exchange rates) in foreign aid in 1961, but the amount surged to about $2.89 billion (about Sh4.91 trillion) in 2009. In terms of sectoral distribution, most of the aid in the 1960s and the early 1970s was channelled to the agricultural and transport sectors.

During the second half of the 1970s, the emphasis shifted to industry and energy. Transport became an important aid recipient in the late 1980s and early 1990s. The general pattern of aid distribution since the 1990s has been (in order of importance) transport and communications, followed by agriculture, human resources development, health, integrated regional development and energy.

Additional reporting by Mkinga Mkinga

Ninyi Ndugu zangu, these are not my words, they come from one of the leading media houses in TZ
 
0dig


Shirika hilo linaloongoza duniani kwa kufichua takwimu za siri katika masuala ya uchumi na fedha limesema, misaada ya nchi wahisani kwa Tanzania imepaa kutoka Dola za Marekani 39.19 milioni (Sh66 bilioni) mwaka 1961 hadi Dola 2.89 bilioni (Sh3 trilioni) mwaka 2009 na kuifanya nchi hiyo kuwa kinara wa nchi za Afrika zinazopokea misaada kutoka nje na pia kushika nafasi ya tatu duniani ikitanguliwa na Iraq na Afghanistan.

Takwimu hizo zimewashtusha wananchi wengi ambao wamehoji kulikoni Tanzania imepokea misaada mingi kiasi hicho tangu ipate uhuru miaka 50 iliyopita lakini imebaki kuwa moja kati ya nchi chache duniani ambazo wananchi wake bado wanaogelea katika umaskini wa kutisha, kiasi cha wengi kuishi chini ya dola moja kwa siku. Wahisani wakubwa wa mipango ya maendeleo kwa Tanzania tangu uhuru ni Sweden, Norway, Marekani, Japan, The Netherlands, Denmark, Uingereza, Umoja wa Ulaya, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Inaeleweka kabisa nchi za Iraq na Afghanistan zinapoorodheshwa na shirika hilo la ‘Visual Economics' kama nchi ombaomba. Hakuna asiyejua kwamba nchi hizo zimekuwa katika vita kwa muda mrefu kiasi cha uchumi wa nchi hizo kuvurugika na watu wengi kuuawa. Katika mazingira ya vita, ambapo umwagaji damu na mauaji ya kujitoa muhanga hutawala, hakuna shughuli zozote za maendeleo zinazoweza kufanyika. Mkombozi pekee wa wananchi katika nchi hizo ni misaada ya nchi wahisani.

Lakini kitendawili kikubwa ambacho kimekuwa kigumu kuteguliwa ni juu ya Tanzania kuwa kinara wa nchi ombaomba barani Afrika na kushika nafasi ya tatu duniani, nyuma ya Iraq na Afghanistan. Kinyume na nchi hizo ambazo misaada nyingi inayotolewa ni ya kijeshi, Tanzania imekuwa ikipata misaada ya maendeleo katika nyanja za elimu, miundombinu, afya, maji, ujenzi, kilimo, nishati na usafirishaji, hivyo isingekuwa maskini iwapo misaada hiyo ingetumiwa kama ilivyokusudiwa.

Tanzania, mbali na kupata uhuru wake bila kumwaga damu mwaka 1961, nchi hiyo imekuwa kisiwa cha amani na wananchi wake wameishi miaka yote kwa amani na utulivu bila vita ya wenyewe kwa wenyewe. Nchi hii inao utajiri mkubwa na imetunukiwa na mambo mengi ya ajabu. Angalia ardhi kubwa yenye rutuba na rasilimali nyingine nyingi, zikiwamo madini ya kila aina, gesi, mbuga za wanyama, mazao ya biashara, misitu, mito maziwa, fukwe za bahari na wanyama pori.

Tafsiri ya takwimu za shirika hilo la ‘Visual Economics' ni kwamba Tanzania imeshindwa kusonga mbele kimaendeleo kwa sababu ya utegemezi mkubwa wa misaada ya wahisani na matumizi mabaya ya misaada hiyo, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa utawala bora, kama Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2009 ilivyobainisha na kusema asilimia 20 ya bajeti ya Serikali kila mwaka inamezwa na vitendo vya rushwa.

Kutokana na changamoto iliyotolewa na shirika hilo, jambo la kufurahisha ni kwamba wananchi sasa wamegundua Tanzania inaweza kusonga mbele kimaendeleo bila misaada ya wafadhili, kwani misaada hiyo imeshindwa kufuta umaskini tangu tupate uhuru. Siyo siri tena kuwa, rasilimali za nchi zimenufaisha kundi dogo la watawala na mawakala wao walio nchini na nje ya nchi.

‘Visual Economics' limetufumbua macho. Yatupasa tutafakari wapi tunataka kwenda kama taifa ili tujenge uchumi wa kutukwamua katika lindi la umaskini. Misaada ya wahisani haitufai, tuachane nayo sasa. Njia pekee ni kujitegemea, kwani tunazo rasilimali za kutosha. Kinachotakiwa ni utashi wa kufanya hivyo.


Mwananchi



 
katika vyombo vya habari taarifa hii imepewa nafasi baada ya utafiti wa shirika moja la marekani Visual Economics kutoa takwimu hiz(source Mwananchi), ninavyofikiri tumefikia hapo tulipo si viongozi pekee wa kulaumiwa hata sisi wananchi tunahusika kwa nia moja au nyingine. nitoe
maelezo kidogo

  • Taarifa hii ni kejeli ikilinganishwa na misaada inayotolewa kwa nchi zilizo kwenye mapigano ya vita miaka nenda miaka rud,i rasilimali zetu nyingi tulizonazo kama misitu,madini ,mbuga,bahari na maziwa zingetusaidia na kuweka uchumi wetu katika hali nzuri lakin mali hizi zinatumika hovyo na wawekazaji wanaotunyonya bila faida yeyote, viongozi wetu wanaingia mikataba ya kifsadi kwa manufaa yao na waliotufikisha hapo wapo na wanajulikana laikini wananchi nao tupo tu tunaangalia bila kulalamika wala kupinga hali hii tunakubali porojo za Kasi mpya,ari mpya na maisha bora kwakila mtanzania!!!!na slogan za tumethubutu,tumeweza na tunasonga mbele !!tujiulize au tuhoji kwa lipi?
  • Wanasiasa tumewaachia wanadominate kila kitu na wanaingilia hata wasomi wetu katika mambo ya kitaalamu ndo maana ni ngumu kwa nchi kupiga hatua kwa kutegemea wanasiasa...maendeleo ya nchi hayaletwi na wanasiasa bali watu wa taaluma husika.Wasomi wetu ni kama wamekosa mwelekeo ndo maana wengi wao nao wanakimbilia siasa ambako hakuna kazi ya kuumiza kichwa huku ukilipwa mishahara na marupurupu manono!!
  • Wananchi tunakubali kauli nyepesi hata wanasiasa wetu wakisema maisha yamepanda Dodoma tunaongeza posho tuko kimya tu wakati nchi nzima kwasasa hali ya maisha ni ngumu na vitu ni ghali sana inflation iko juu kila wiki 1au wiki 2 bei za vitu ni tofauti.
  • Wafanyakazi mko wapi? wananchi je tuko wapi? tubadilike na tuchukue hatua kupinga mfumo wa utawala ulipo wa kulindana na kutojali masilahi ya nchi.
 
Nafikiri ni muda muafaka wa kutafakari haya na kuhoji utaifa na manufaa ya kuitwa mtanzania, ni wakati sahihi wa kukataa haya kwa vitendo, tanzania nchi iliyosifika kwa kila kitu sasa imekuwa kinuyume cha hayo na kuwa kijiwe cha wanyanganyi na walanguzi wa nchi.

Napatwa na hasira ninaposoma ripoti mbalimbali na kuona eti sisi ni watano barani afrika kwa rushwa, sisi ni wa 3 kwa kuombaomba hali hatuna vita, hatuna ukame, sema tuna mali kila kona ya nchi, eti sisi ni mwisho kwa kukusanya kodi, hii inasikitisha sana na nakaa na hoji umuhim wa hawa wanaojiita wabunge, hivi kazi yao nini kama kuisimamia serikali wameshindwa, ona posho sasa wanajilipa 28b pa ka posho tu, napatwa na mshtuko, namwangalia mwalimu, polisi ambao kiwastan mishahara yao ni 150,000/ hali mbunge anapata marambili ya hiyo pesa kwa masaa ndani ya siku moja, hii ni chuki ya namna gani inapandikizwa ndani ya vichwa vya watanzania, ni uzalendo gani unajengwa?

Sidhani ka bunge ni sehem ya kujilipa na kuamua wafanye nini na pesa zetu, eti gharama zimepanda, nani asiyejua mfumuko wa bei ni zaidi ya 20% ila kisiasa nalipotiwa 17.9%? je ongezeko hili serikali imefanya nini ili kuwasaidiwa watumishi wake wanacover vipi hii gape??mwanachi mnamjali wakati wa kuomba kura???ipo siku NASEMA IPO SIKU, HAYA YOTE MTAYALIPIA, USANII MNAOFANYA KUKUSANYA KODI, KULINDANA KWA WALA RUSHWA, ITAWAKOST, I AM TELLING YOU. kaa tumefika hatua katibu wa bunge na speaker hawaongei lugha moja hii si hatari??? tunajivunia nini sisi ka watanzania na madini yetu, na bahari yetu, na maziwa yetu, na mbuga zetu, na milima yetu, na makumbusho yetu, haya yote tunakusanya eti billioni mara 480, mara 670? kweli?

Nina uhakika kama tungekuwa makini na kazi tunayoifanya, tukaweka ubinfsi pembeni na kudumisha utaifa aliotuachia mwalimu, elimu, afya, cement na mabo mengine yangekuwa kwa bei ya chini sana, kodi tungeweza kukusanya hata 3b per month! only 1.5 ndo wanalipa kodi alafu leo rais anasema wanachi wamsaidie kuwafichua wakwepa kodi hivi serikali haiwajui wakwepa kodi???mbona usanii ni mwingi? mkapa alijitahidi akakakusanya hadi 400b per month iweje leo for the pats 6 years tumekwama, tunajikwaa wapi? tuna haja ya kukopa for recurrent expenditure??sisi tunakopa kwa ajii ya matumizi ya ndani na si miradi ya maendeleo???

chedema,wanaharakati, nccr na wengine wenye majukwaa please call for action on this, it is very serious kuona mnayo majukwaa na mnakaa kimya, hii si issue ya kuangalia, mnapeana mishahara minono huku watu hata 500 hawapati a day!mnalea watnzania wenye akil na mtazamo wa namna gani???

nasikitika sana juu ya haya yanayotokea tanzania chini ya kikwete
mwananchi wa kawaida
mwenye kilio na majonzi yasioisha hadi niione tanzania niitakayo
luckman-true we created rich sema wachafuzi wamehanisi nchi yetu
 
Kikwete anapeleka wapi hiyo misaada anayopewa?

Ukiangalia barabara ujenzi umesimama, mishahara walimu wamedai mpaka wanataka kuingia mgomo, lakini pia humu jamvini wahadhiri wa UDOM wanalalamika tangu wapandishwe kutoka TA kwenda AL mwaka jana november 2010 hawajalipwa mshahara wao mpya na leo ni miezi 13 tangu wapandishwe. Mishahara kwa ujumla inachelewa na hata gazeti moja leo limeukuu habari kuwa fedha za budget zimepungua mno.
 
umenigusa sana juu ya mazingaombwe yanayofanywa na watawala, tungefika mbali ka tungepata viongozi lakini ka ulivosema naamini ipo siku watayajutia haya!
 
CCM oyee. Nafikiri baada ya miaka 5 tu, tutakuwa wa kwanza kabisa, yaani tutazipita hata hizo Iraq na Afghanistan.
 
Jamani hii ni zawadi nzuri sana kwetu tunaposheherekea miaka 50 ya Uhuru! Tujipongezeni!!

At least tumekuwa wa Kwanza kwenye hili shindano. Tumeshindwa kwenye mpira, riadha, kuogelea, karate, mbio za langalanga, mambo ya uchumi, lakini kwenye hili tumewatoa kamasi. :poa
 
Sifa zote hizo tunastahili. TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE. Aibu tupu, Kiongozi wa nchi kila siku kiguu na njia pamoja na kushauriwa sana kupunguza safari, AMEZIBA MASIKIO, yeye ndiye aliye tupandisha chati hii. SASA SUBIRI HOTUBA YA MIAKA 50 YA UHURU, uone porojo za maendeleo.
 
Ushauri tu kwa mods......please....wekeni hii thread kwa front page isihame kama ilivyo thread ya safari za jk....ili hawa majambazi serikalini wawe wanaiona kila wanaposoma jukwaa la siasa.......tena iwekeni sawia na thread ya safari za jk.....zisihame kabisa.....my worry is that there are some reports which are so crucial to the nation but are not really read.....i mean,seems to me that people prefer gossiping(especially in politics) than contributing to realistic problems facing tz........just my opinion.......
 
Back
Top Bottom