Why Tanzania is top 'beggar' after Iraq, Afghanistan

wanasema nchi zinazopewa misaada mingi
nyingi ndo masikini zaidi
yaani misaada inawaongezea umasikini
hiyo yaweza kuwa sababu

Nakumbuka miaka ya nyuma kulikuwa na thread hapa kama sikosei ilianzishwa na Mwanakijiji. Katika thread ili wengi waliona umuhimu wa kuanzisha kampeni ili kuzishinikiza nchi tajiri kuacha kutoa misaada kwa Serikali ya Tanzania hasa ukitilia maananii hatuoni mafanikio yoyote ya maana pamoja na misaada mingi tunayoipata. Mingi ya misaada hiyo inaishia mifukoni mwa mafisadi na Serikali kuishi kwa gharama kubwa kuliko hata Serikali zinazotoa misaada hiyo, kwa mfano Mawaziri na Vingunge wengine Serikalini kusafiri kwa 1st class kila waendapo nje ya nchi na kulipana posho kubwa kupita kiasi.
 
WAMETHUBUTU,WAME...................................Damn
huu mseme unanichefua kila nikiusikia

Mie kuna msemo mwingine alikuwa anapenda sana kuutumia Mkapa ulikuwa unaniudhi sana. "Watanzania tujipange upya"....Kujipanga gani miaka 50 ya uhuru na rasilimali chungu nzima lakini bado nchi ni omba omba na tunawaachia wageni waibe utajiri wetu na sisi tumechapa usingizi tu!!! Chukueni hiyo dhahabu yetu mtuachie sisi 3% inatutosha kabisa!!!!
 
Misaada mingi inarudi kwa kampuni za waliotoa msaada in the name of experts pay, capacity building, manunuzi ya thamani...etc

Mikopo tena yenye riba kubwa mingi inarudi kwa kampuni za waliotoa mkopo in the name of experts pay, capacity buildings, manunuzi ya thamani ..etc

Nchi inatakiwa kuachana na misaada na mikopo kwani uwizi wa mchana..

hivi hata iraq inaweza kusemwa inaomba kutoka Ulaya au ndio ule ujambazi wft
 
saa zingine huwa najisikia aibu kujitambulisha mimi ni mtanzania....nchi ya 3 kwa kuomba duniani na bado ni maskini wa kutupwa. Halafu huyo Likwelile anadhani kujilinganisha na Egypt na Israel kutaleta unafuu?? hamna kitu kama hiyo bora angenyamaza tu asingejilinganisha na wengine. Ujilinganishe na wengine kimaendeleo si kwa kupitisha bakuli la kuomba kila siku. Hata matonya ana afadhali
 
Sikuwa nimefahamu hivyo kabla. Something must be done. Mungu aturehemu
 
Tamaa ya viongozi wetu ndiyo inatuletea aibu hii. Leo MOVENPIK kuitwa SERENA. je si ujinga huo? Na sasa watoa pesawameona tamaa yao ya fedha imekuwa kubwa wameeamua kuwaingiza kwenye u-masonic. Kwani tunawaona wasivyojali wala kuogopa mtu wakijua tayari ni wabaya.Yahu na awakemee ktk jina la Yeshua.
 
Mimi nahisi ni kwa sababu ya ufisadi wa Edward Lowassa ndo maana nchi yetu ni maskini, akivuliwa gamba tutakwea juuu!
 
Mimi sio Matonya, ni Kiherehere cha kikwete na Mafisadi wenzake ndio wanotutia aibu

Ukiwa Tanzania you are automatically Matonya, you like it or not. Pamoja na wengine hatupendi tabia ya kuombaomba, Rais wetu alisema wazi kuwa asipenda kutembea tutalala njaa. That is exactly what got us where we are.
 
Tatizo ni kwamba hiyo misada haiendi kwa mambo yaliyolengwa. Wachumia tumbo wanagawana kwa njia wanazojua wao. Kila mtu akiwa kwenye madaraka anajifikiria mwenyewe. Hakuna mwenye uchungu na nchi hii kwa wote walio madarakani. Wakiendelea kuwepo marakani hao hao maendeleo ni ndoto kwenye nchi hii.
 
Hili li-nchi linatia aibu! Uzembe wazi wazi. Ivi kweli tunaweza kuendelea na hawa wajinga wakitutawala?
 
Tanzania, whose aid portfolio has ballooned to over Sh3 trillion (about $2.89 billion) in its 50 years of independence, is currently Africa's top beggar for development assistance, The Citizen on Sunday can authoritatively report today.That level of dependency makes it the third leading recipient of official development assistance (Oda) in the world after war-torn Iraq and Afghanistan.

Maelezo haya peke yake yametosha... Haki ya nani, hakuna cha kujisifia hata kidogo..
 
Tanzania, whose aid portfolio has ballooned to over Sh3 trillion (about $2.89 billion) in its 50 years of independence, is currently Africa’s top beggar for development assistance, The Citizen on Sunday can authoritatively report today.That level of dependency makes it the third leading recipient of official development assistance (Oda) in the world after war-torn Iraq and Afghanistan.

Maelezo haya peke yake yametosha... Haki ya nani, msifikirie beggars tu, fikirie kuwa haya ni madeni ambayo tutayalipa.. hakuna cha kujisifia hata kidogo..
 
""But the government yesterday questioned the accuracy of the report, saying there were many other countries that received much more in foreign assistance than Tanzania. Finance and Economic Affairs deputy permanent secretary Servacius Likwelile told The Citizen on Sunday that countries like Israel and Egypt receive a substantial amount of assistance from the US annually, and wondered whether the report included military aid. ""

Yaani huu upuuzi wa viongozi wetu ndio kashfa kubwa zaidi. Huyu Likwelile anadhani report za watoa misaada zinaweza kuwa wrong?? Yaani bank ikopeshe watu halafu isijue ni kiasi gani imekopesha?? Kichekesho.

Israel na Egypt wanapewa misaada mikubwa ya vifaa vya majeshi ie F16 blah blah hawapewi pesa cash.

Report iko very open kuwa inazungumzia DEVELOPMENT AID.

Yaani aibu ya mwaka, Iraq na Afghanistan wao nchi zao ziliharibiwa vibaya baada ya vita, so ina make sense wapewe Aid kubwa, sisi Tunaoambiwa Kisiwa cha Amani, si Aibu hii.

Week ijao iwe ni week ya kutafakari, miaka 50 ijayo tunajipanga vipi, na kuomboleza balaa lililotupa miaka 50 iliyopita. HAKUNA SABABU YA SHEREHE KUBWA zinazotumia mabilioni ya hela.

Tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
ndio hapo. Niliposoma maelezo yake nilitaka kutaapika. Hizi ndio akili zinazotuongoza. The first step to help urself is to admit your mistake. Hawa ni wapuuzi kweli. Hovyo wote...
 
ndio hapo. Niliposoma maelezo yake nilitaka kutaapika. Hizi ndio akili zinazotuongoza. The first step to help urself is to admit your mistake. Hawa ni wapuuzi kweli. Hovyo wote...
Ni kwa sababu viongozi wetu hawasomi kilichoandikwa bali wanarukia tu... Imesemwa wazi beggars for Development Assistance, sasa sielewi Egypt na Israel zinaingia vipi hapo.
 
Back
Top Bottom