Whozu ana kipaji kikubwa, akikazana na kujifunza atafika mbali sana

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,796
Juzi nimeletewa wimbo na mdogo wangu unaitwa Mi Amor wa huyu Whozu. Huwa nasikiliza Bongo Fleva lakini ni wasanii wachache sana huwa nawafurahia kwa uwezo wa kufanya ubunifu wa kujitenganisha na wasanii wengine. Mara nyingi wasanii wengi huwa wanaigana sana kuimba na mwisho kabisa huwa unakuta radha inapotea kabisa.

Mimi napenda sana Jazz, Soul Music na Afro-Pop na niliposokiliza huu wimbo kuna vitu vilinifurahisha mno. Kwanza kabisa ni vile vionjo vya Jazz kwa kutumia lile tarumbeta, pili kumuiga King Kiki (huyu ni mzee legendari), lakini tatu na kubwa zaidi ni uwezo wa kuchanganya Afro-Pop, Bongo Fleva na Jazz bila kuharibu (Wasanii wachache sana wanaweza kufanya hivi)

Kuna baadhi ya vionjo ametumia kwenye wimbo huu ni vya Burna Boy, hasa alivyokuwa anapanda kwenye daraja (Bridge) na kuimba NIKIKIKUONA kwa mara ya pili. Pia ile suati ya kuvuta kwa kukoroma kama chura dume (Bull Frog) ni Jingle ya Burna Boy, hii siyo mbaya kwasababu hata Platnumz ameiga kwenye baadhi ya nyimbo zake, lakini kubwa zaidi ni kwamba hata Burna mwenyewe huwa anaiga.

Sasa kitu cha msingi ili huyu ndugu yetu aweze kufika mbali kimuziki ni lazima ajikite kujifunza vitu vipya kimuziki kila siku ili kuwa mwepesi (Flexible). Apanue uwanja wake kwa kuweza kufahamu aina mbalimbali za muziki, upigaji wake na uimbaji wake pia.

Kama ameweza kumuiga Burna Boy na akafanya vizuri nadhani pia ni vyema kufahamu wasanii wengine wa Afrika wanafanyaje ili kufanikiwa kimuziki. Diamond Platnumz alifanikiwa kufanya hili vizuri hivyo siyo vibaya kuiga mambo mazuri kutoka kwake. Leo hii unaweza ukamuweka Diamond Platnumz na msanii kutoka nchi yoyote duniani na bado akafanya vizuri sana: iwe ni Sebene, Zouk, Jazz, House Muzik, Reggae, Taarab, RnB na HipHop atatoa kazi nzuri tu.

Platnumz ameweza kuimba vizuri sana na wasanii wakubwa kama Papa Wemba, Mafikizolo, Ne-Yo, Omarion , Rick Ross, P-Square na Burna Boy ambao wametoka kwenye misingi tofauti kumuziki. Hii yote inatokana kupenda kukaa chini kujifunza vitu vipya kila siku, kitu ambacho watanzania wengi huwa tunakipuuza hata kwenye maisha yetu ya kila siku.

Burna Boy mwenyewe anajifunza sana mentors wake ni Femi Kuti na Angelique Kidjo ambao kwenye tasnia ya muziki ni miamba mikubwa sana hapa Afrika. Mtanzania wa kawaida akisikiliza muziki wa mtu kama Burna Boy anaweza asivutiwe nao lakini watu ambao wamesomea muziki na kuufahamu vizuri ni lazima watampenda.

Hivyo kama anataka soko lake liwe nje ya mipaka yetu basi ni lazima akae chini na ajifunze aina mbalimbali za muziki. Hapa sisemi kwamba ni lazima aige kila kitu cha huko nje, lakini ni lazima ajue vitu vingi ili aweza kutofautishwa na wasanii wengine wa hapa Tanzania hasa linapokuja swala la ubora wa msanii. Nimefuatilia nimeona ashaanza kufanya baadhi ya kazi na wasanii wa nje, hivyo ni muhimu sana ajifunze vitu vingi ili aweze cheza nao ngoma moja. Diamond Platnumz ameweza, Harmonize ameweza na wewe ukikazana utaweza na hata kuwashinda hawa wawili, maana una muda mwingi wa kujifunza.

Mwisho kabisa menejimenti yake ni lazima ishirikiane sana na vyombo vikubwa vya burudani ili kuweza kung'amua soko linataka nini ili kumuwezesha msanii ajifunze kubadilika kwa haraka. Hapa ndipo wasanii wengi wa kitanzania wenye vipaji vikubwa hasa wale wakongwe walishindwa. Jamii yetu inabadilika haraka hivyo hata mahitaji ya mashabiki yanabadilika kwa kasi, hivyo ni lazima menejimenti ikae karibu na vyombo vya burudani maana wao ndiyo wanahusika na hadhira moja kwa moja. Wasanii wakubwa wanakuwa na utaalamu wa kuimba vizuri kisauti, uandishi unaofikirisha na kugusa jamii na menejimenti yao inawasaidia kutengeneza video nzuri (Haya ndiyo mahitaji ya Millenials wengi)

LA KUKUMBUKA:
Msanii Davido alivyosajiliwa Marekani alipata shida sana mara ya kwanza lakini alikaa chini na kufahamu vizuri muziki ambao wenzake wa kule wanafanya hivyo akaacha kuiga kila kitu lakini akatumia ule ujuzi mpya kuboresha muziki wake.

Ndiyo maana hadi leo hii ameweza kufanya wimbo mkubwa kama Blow My Mind na msanii kama Chris Brown. Burna Boy, Yemi Alade, Tiwa Savage na WizKid ukiwasikiliza kwa makini mtathibitisha hili ninalolisema, wote wanajifunza vitu vipya kwa bidii kila siku hata vile ambavyo viko nje ya muziki lakini vinagusa jamii nzima. Video nzuri, mashairi mazuri yanayogusa sana jamii na uwezo mzuri kisauti ambao unawawezesha hata kuimba moja kwa moja.
 
Whozu ana kipaji gani sasa au ndio umeamua kutudhihaki watanzania wenzio?
Binafsi naona dogo ana kipaji TENA KIKUBWA SANA TU, kama asingekuwa nacho sidhani kama angefanya hata haya aliyoyafanya leo hii hadi akafahamika nchi nzima. Uzuri ni kwamba hata hao unaohisi wana vipaji huwa hawazaliwi hivyo walivyo ila kuna juhudi wanaifanya hadi wanakua na kukomaa, Diamond Platnumz ni ushahidi mzuri kabisa wa ninalolisema hapa. Nakumbuka wakati anaanza 2009 kuna baadhi ya watu walishawahi kusema kwamba ni wa kawaida sana lakini leo hii yuko wapi ??? It's Nature X Nurture.
 
Whozu ana kipaji kizuri sema watanzania wengi hawajui maana kipaji Ni nini?
 
Kwa sasa kipaji sio tatizo , tatizo ni nan anakushika mkono, Kwa Tanzania hii ni menejiment ya WCB tuu mpak sasa ndo imeonyesha uwezo wa kumtoa msanii toka sehemu moja kwenda nyingine, media kubwa hamna kitu , mchango wao ni kukutambulisha tuu , ukajulikana lakn kumove from one step to another only WCB can do this , ......
Ukisainiwa WCB ni uzembe wako Tu kutokutoboa , ukiwa na juhudi mapema Sana unapepea , Harmonize ametumia vizur nafas ya kukaa na magenius ya WCB , na anatoa mawe Sana , tatizo anakosa menejiment yenye ushawishi to reach the sky, watu ambao wanaweza wakagonga hodi hata Mtv base wakafunguliwa milango na kusikilizwa , ......Whozu kipaji anacho tena cha upekee tatizo linabak nan anakujua, the same case to Maua Sama,
 
Kuna ukweli mwingi sana kwenye hili mkuu
 
Binafsi naona dogo ana kipaji TENA KIKUBWA SANA TU, kama asingekuwa nacho sidhani kama angefanya hata haya aliyoyafanya leo hii hadi akafahamika nchi nzima. Uzuri ni kwamba hata hao unaohisi wana vipaji huwa hawazaliwi hivyo walivyo ila kuna juhudi wanaifanya hadi wanakua na kukomaa, Diamond Platnumz ni ushahidi mzuri kabisa wa ninalolisema hapa. Nakumbuka wakati anaanza 2009 kuna baadhi ya watu walishawahi kusema kwamba ni wa kawaida sana lakini leo hii yuko wapi ??? It's Nature X Nurture.
Kusema ukweli Whozu ana kipaji ila cha kawaida, hatishi yaani!
 
Nadhan huyo dogo ni exptional!ana kipaji kikubwa sana sema wengi hawaelewi!
Mie mpaka leo nashangaa nandy anafikaje juu na huku anaimba flat sana!..nandy hakai bench moja na Rubby au Vanessa! Au Maua!
Nadhan connection ni kitu muhimu pia!
Naunga mkono hoja😊
 
Back
Top Bottom