Who is Francis Cheka..?

Mythbuster

Member
Dec 12, 2010
92
50
Wazee nimekuwa nikipata habari za kusifika sana kwa Bondia Francis Cheka hasa miaka hii ya karibuni. Hivi huyo jamaa ana sifa gani hasa katika fani ya ngumi. Mwenye data naomba atujuze , jamaa ana ufundi gani hasa.
 
cheka ni mzaliwa wa kinondoni,kabla ya kujitia katika masumbwi alikuwa mcheza kandanda kama walivyo vijana wengi wa kitanzania...makazi yake ya sasa ni morogoro ambapo alitia nanga hapo alivyokuwa katika harakati za kwenda south africa kutafuta maisha ndipo ailpokutana na kocha wake almaarufu kama komandoo aliyeweza kumtia katika boxing na kuzima harakati zake za kwenda south africa,hapo morogoro kuachana na masumbwi cheka ni mfanyabiashara wa chupa za plastics......umaarufu wake katika ndondi ulikuja pale baada ya kumtwanga nguli wa masumbwi tanzania rashid ''snakeman'' matumula...ni bondia mzuri anayeweza kutumia urefu wake ana pumzi za kutosha kuliko mabondia wengi wa bongo na pia hupenda kutumia ngumi za kudokoa kuchosha wapinzani wake
 
Nasikia ana nidhamu kubwa sana ya mazoezi...anapandisha milima na tairi ya trekta ili kupata na maintaini pumzi na nguvu kifua na mikono....anajitahidi sana kwa kwelii...akiendelezwa na kupewa support atafika mbali sana....tangu aanze sijasikia akipigwa...bado kwa mapambano ya ndani!!! Ingawa jana ametolewa sana jasho ile ni kama draw tu...
 
Back
Top Bottom