Who is Benson Bana?

Siku zilizobaki bado ni nyingi sana. Mkapa aliwahi kumteua mtu saa za majeruhi

Ok inawezekana lakini siyo matarajio yake huyu Benson.Matarajio yake ilikuwa angalau apate miaka 3 ya kukamua madarakani.
 
Jana nilitazama kipindi cha Kiti Moto cha ITV na niliumia sana kuona kuwa msomi kama Dr.Benson Bana akizidiwa nondo na dada ambaye ana shule ya kawaida, Ketty! Aliniacha hoi Dr. Bana alipoponda uamuzi wa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya Bunge wakikwepa kupiga kura ambayo walijua wazi kuwa,kwa idadi yao isiyofikia ya Wabunge wa CCM na wa vyama vyao shirikishi Bungeni, wangesaidia kuhalalisha uamuzi wa Bunge ulio kinyume na msimamo wao.

Wasomi wa kweli wanajua kuwa CHADEMA walitoka nje ikiwa ni hatua ya mwisho kabisa (last resort) ili isijengeke picha kwamba uamuzi walioupinga wa kuunganishwa kwa lazima kwa watu kucheza na kanuni, yalipigiwa kura na wote wakiwemo hao wabunge wa CHADEMA na hivyo uamuzi huo ni wa wote,yaani wa Bunge zima.

Dr Bana alisema kwamba wabunge hao wa CHADEMA walifanya vibaya kuchukua hatua hiyo aliyoitafsiri kuwa baadaye itakuwa ya kufuatwa na kila kundi la watu watakaopinga maamuzi ambayo hawakukubaliana nayo. Mpaka hapo sikuona tatizo la shule yake kwa hoja yake.Lakini alikuja nichosha aliposema walichopaswa kufanya wabunge wa CHADEMA ni kukomaa mjengoni na kupambana kwa hoja kutetea kile walichoamini kuhusu jambo lililokuwa liamuliwe dhidi ya msimamo wao badala ya kutoka nje kuikimbia hoja.

Daktari wetu huyu wa Falsafa ina maana kishasahau kwamba wabunge hao wa CHADEMA walishapambana kwa nguvu zote za hoja ndani ya mjengo kupinga walichoona si haki kutendewa katika suala hilo katikati ya miguno,kejeli,kauli kali kupitia vipaza sauti bila Mheshimiwa Spika kukemea waliofanya utoto huo huku "miongozo ya spika" ikiombwa hapa na hapa! Dr Bana alichotaka wabunge hao wa CHADEMA wazipige kavu kavu ndani ya mjengo na wapinzani wao baada ya Mheshimiwa Spika kutupilia mbali hoja zao na kuamua kura ipigwe?

Huyu ni Daktari wa Falsafa wa namna gani asiyelitazama suala kwa mapana na kuzama kwenye ushabiki wa kisiasa? Hivi taasisi yake inayotoa takwimu za kisiasa inapaswa kuendelea kuaminiwa kweli wakati yeye ameshajibainisha anashabikia upande gani katika staili isiyo tofauti na ya ushabiki wa Yanga na Simba usioona mazuri ya upande mwingine?

To me, PH D ya Dr. huyu ni very questionable.

Issue hapa sio PHD, ni matarajio ya maisha baada ya kupata level fulani ya Elimu. Wasomi wengi huwa na matarajio ya maisha ya kifahari wanapofikia level fulani za elimu. Kama ikitokea kinyume chake basi wako tayari kufanya chochote ili watoke ikiwemo kujipendekeza kwa watawala kama anavyofanya Dr Bana na wengine wa calibre yake.
Mpaka hapo sera yetu ya elimu itakapokuwa bora ndipo matatizo kama haya yatapungua.
 
Kwa nje namuona kama kinara mpya wa wahadhiri vibaraka Tanzania.

Anayetafuta vyeo kwa kuidhalilisha taaluma yake.

Anayewatii mabwana zake kwa kudhalilisha tasnia nzima ya utafiti Tanzania.

Msomi bandia, anayedhililisha demokrasia Tanzania.

Kwa wale wanaomfahamu zaidi tabia na Historia yake, naomba wamuelezee "Dk." Benson Bana.

Ivi Huyu Mzee Bado Ni Dkt Tu?Kale Kajopo Kakujadili Kumpa Uprof Vp?
 
Mie nimeipenda hii,

'The most potent weapon of the oppressor is the mind of the oppressed '
 
Benson Bana PhD, ni mhadhiri na mwalimu aliyenifundisha Political Science/Public Administration UDSM, ni mwenyekiti mwenza wa REDET pia ni mshauri wa Rais ktk mambo ya siasa.. Kama binadamu ANAMAPUNGUFU YAKE!

Mapungufu ya Bana sio ya kibinadamu, ni ya kimaslahi, Bana ni mtu mwoga, ni kigeugeu ambaye hufuata upepo wa maslahi unakokwenda, mikikimikiki ya kikazi iliyomkuta Prof Baregu ambaye ni homeboy wake imemtisha sana Bana, akaamua kutumikia tumbo Lake tu, taaluma kushoto
 
Ok inawezekana lakini siyo matarajio yake huyu Benson.Matarajio yake ilikuwa angalau apate miaka 3 ya kukamua madarakani.

Imekula kwake. Sasa atulie atumie taaluma yake vizuri aache usakaji tonge kwani sasa jua limezama.
 
Kwa nje namuona kama kinara mpya wa wahadhiri vibaraka Tanzania.

Anayetafuta vyeo kwa kuidhalilisha taaluma yake.

Anayewatii mabwana zake kwa kudhalilisha tasnia nzima ya utafiti Tanzania.

Msomi bandia, anayedhililisha demokrasia Tanzania.

Kwa wale wanaomfahamu zaidi tabia na Historia yake, naomba wamuelezee "Dk." Benson Bana.
Huwa anakiwakilisha vyema kile chama cha kijani,
 
Back
Top Bottom