Who are they: Mbowe, Sitta, Slaa, Zitto, Mwakyembe, Kubenea, Lissu, Rostam...

Madeni kwenye biashara kitu cha kawaida tuu, ila kama mnavyosema kesi hiko mahakamani or hukumu imeshatolewa basi tusubiri matendo, ila wangeapply kwa kina Manji/Mengi? Bro Ben as well

Huyu Joseph Kusaga ni mtoto wa yule mzee wa Mara Corp?
 
Inaelekea shutuma hizi hazina ushahidi wa kutosha kwa hiyo tuachane nazo tu tuendelee na mambo mengine ingawa mimi binafsi nachukulia financial problems za mwanasiasa kama red light.

Huyu Joseph Kusaga ni mtoto wa yule mzee wa Mara Corp?

Inawezekana; historically Kusaga alikuwa mtemi wa sehemu moja ya Majitta huko Musoma na kuna mtaa pale Musoma unaitwa Kusaga sijui kama ni kwa heshima yake. Waweza kuwa ni ukoo huo huo
 
Joe Kusaga, ni mtoto wa Mzee Kusaga aliyekuwa mkurugenzi wa kitengo flani hapo Bima, at one time yeye na Asha Baraka walikuwa makarani wa deski kwenye ofisi kama darasa pale Bima karibu na NBC, na leo wame-make it kwa kufanya kazi kwa bidiii, the matter of fact Asha Baraka mpaka leo bado ni karani hapa Bima,

Sasa Joseph, hupewa tenda nyingi za TBL kuwaleta wanamuziki mashurui duniania, na TBL humtumia Joe kwa sababu ya kuwa na jina kubwa katika hiyo industry ya muziki bongo, kwa hiyo majungu tuache jamani!
 
"The distance between genious and insane is measured only by success" - Kwenye picha ya James Bond

Kubeba maboksi ni kuajiriwa. Kumiliki radio na promotion agency ni kujiajiri. Ni vitu tofauti hivyo, hope mtanzania umeelewa.

Nyani Ngabu, Kinachonikera ni kitendo cha kuwabeza wajisiriamali kama Joe Kusaga!!!! Yes huwezi kumlinganisha muajiriwa mmbeba mabox na yeye aliyethubutu kujiajiri!!
 
Fikiraduni,

Muajiriwa na aliyejiajiri wote wana contribute kwenye jamii zao. Success inatokana na performance ya mhusika kwenye kazi yake. Contribution ya scientist kwenye maabara yake ya kutibu magonjwa inaweza kuwa kubwa zaidi ya mjasirimali aliyeanzisha kampuni yenye mabilioni ya pesa. Hivyo hivyo
contribution ya muuza vitumbua mtaani inaweza kuwa kubwa kuliko Dr. ambaye hatimizi wajibu wake ofisini.

Wenzetu wanathamini contribution ya mtu kwenye jamii yake bila kujali amejiajiri au ameajiriwa. Contribution hiyo sio lazimwa ipimwe kwa fedha.

Ni uhusiano mzuri kati ya walioajiriwa au waliojiajiri ndio unasukuma maendeleo ya jamii mbili.

Nafikiri aliebeza wajasirimali hana tofauti yeyote na anayebeza walioajiriwa. Kwamimi wote hawa wanachangia maendeleo ya taifa lolote lile.

Nafikiri ni arrogance kubwa sana kubeza kazi za watu ambao ni through hizo kazi wanaishi, wanasomesha watoto nk. na hawajatenda kosa lolote kwenye jamii.
 
Just carefully look around you wherever you are, you will soon notice that most people who are successful in life were not the cleverest at school! From kubeba maboksi watu waliweza kutengeneza utajiri na hata kusaidia wengine kujitoa kwenye umaskini. I mean we are not trying to justify watu kubeba maboksi lakini pia hatuna sababu ya kuwabeza wale wanaofanya hizo kazi. Attitides kama hizi ndo zinafanya vijana wetu wanaosoma vyuo vya nyumbani wawe ombaomba, hata hela ya kununua kondom inabidi waombe kwa baba zao kwa sababu hawataki/hawawezi kufanya kazi kama hizi za maboksi kwa kujifanya wamesoma na vitu kama hivyo. Acheni hizo bwana
 
Vile vile ni arrogance kubwa kubeza waliojiajiri.... AU SIVYO??????

Ngoma drooo, mkuki mchome nguruwe kwa binadamu mchungu eeeh??!!
 
Kweli Mwanasiasa Aka Kitila Mkumbo unaelekea kupoteza UMAKINI. Soma between the lines utaelewa nilimaanisha nini!!! Sikudharau, nilisema mtaishia kubeba mabox, haina maana kubeba mabox ni mbaya. Kama huna akili ya kujiajiri ufanyeje??!!

Vilevile usiwadharau waliojiajiri hata kama wanauza vitumbua!!! Mkitaka KUSPIN MAMBO nipo makini mnnooo!!
 
Sio nyinyi mnaomuita Mwanakijiji ana radio ya MBAO au redio ya VICHOCHORONI????!!! sema, uongo au kweli??!! Kwanini mnamkatisha tamaa?

Mbona mabox mnaipigia kelele?!! Nimewashikaaaaaaaaa!

Hapa jiwe kwa jiwe!! Jino kwa jino!! kama anavyosema Mzee ES ukileta za kuleta tunakuletea vilevile. Yupo wapi Semvulachole aliyekashifu watu. Kawaachia nyie mnamtetea???
 
Vile vile ni arrogance kubwa kubeza waliojiajiri.... AU SIVYO??????

Ngoma drooo, mkuki mchome nguruwe kwa binadamu mchungu eeeh??!!

Sidhani kama kuna aliyewabeza. Sema tu kwamba issue ilikuwa kuwahusisha na tuhuma ambazo si za kweli.

Ila kama ambavyo tunawalalamikia walioajiriwa kwa kutotimiza wajibu zao, vile vile hata wale waliojiajiri kama wanatumia hizo njia kulihujumu taifa hatutasita kuwafichua na kuwaleta mbele ya hadhara.
 
Fikiraduni,

Mimi nimechangia hoja yako, je ni wapi umesoma nikisema mwanakijiji ana radio MBAO? Au ni wapi nimedharau aliyejiajiri?

Hata kama unashambulia hoja ya mtu mmoja, usiwabeze watu wengi ambao hawahusiki kabisa na hiyo hoja. Generalization ni kitu kibaya sana.

Niliwahi kukaa Sweden, wakati wa summer vijana wao wanatafuta wenyewe pesa za kuendea holidays. Wanaenda kuchuma matunda na kufanya kazi zingine. Wengine baba zao ni mamilionea lakini wamejenga utamaduni huo, lazima pesa ya holiday atafute mwenyewe, labda baba anaweza tu kumwongezea.

Sisi tulio maskini zaidi tunaona kubeba maboksi ni karo. Kila jamii itakuwa na
watu wanaofanya kazi za kila aina, sasa kubeza baadhi ya kazi sidhani kama kunatusaidia.

Mfano wa Kitila ni mzuri sana. Mimi nilikuwa na kazi yangu moja Dar, ili ku save muda nikawaambia jamaa zangu kwamba watafute mwanafunzi mmoja mlimani au IFM na vyuo vingine vya biashara ili wapate mwanafunzi anayesomea marketing atusaidie hizo kazi kwa muda wake wa ziada. Mawazo yangu yalikuwa ataongeza kipato lakini kubwa zaidi atafanya mazoezi kwenye field yake na sisi tutapata data tulizokuwa tunazihitaji. Nikaambiwa wanafunzi wafanye vibarua, wachekwe?

Niliishiwa nguvu, tunajenga taifa la wakubwa.
 
sasa hapa mi naona tunarudi kule kule.they talk alot about the guy kuhusu academics and now tunarudi chini kwenye bussiness attacks.Anyway mimi ninaona afadhali yeye kakumbana na matokeo ya bussiness,i mean kudaiwa au kuwa na surplus kuliko ambao wanajua kutumia public resources for their private gain.Mugongo plz naomba umuulize Prez Jk an Pm kuhusu hiyo deficit ya Benki kuu maanake still tunasubiri kuwasikia watu wakijitetea.So achana na personal attacks and let us focus on public interests as institution.
 
Sure. Msg delivered. back to the business!!!

Mtanzania sorry kwa ku generalize!!! Nimekubali yaishe!

Tuendelee.............
 
Sio nyinyi mnaomuita Mwanakijiji ana radio ya MBAO au redio ya VICHOCHORONI????!!! sema, uongo au kweli??!! Kwanini mnamkatisha tamaa?

Mbona mabox mnaipigia kelele?!! Nimewashikaaaaaaaaa!

Hapa jiwe kwa jiwe!! Jino kwa jino!! kama anavyosema Mzee ES ukileta za kuleta tunakuletea vilevile. Yupo wapi Semvulachole aliyekashifu watu. Kawaachia nyie mnamtetea???

Mkuu FD.

si wao ni mimi ndiye niliyesema REDIO YA UVUNGUNI si redio Mbao au Uchochoroni kama ulivyodai.

ni kama mchezo wa kuigiza aufanyao Mwanakijiji. utasikia kwa niaba ya John Almas, Catherine Mwambene n.k huku akiwa peke yake chumbani.kuna siku nilimkomalia kuwa acha kudanganya kuwa uko na jopo la wafanyakazi huku uko peke.

siku iliyofuatia akawa anatangaza halafu akapiga simu yake ya landline kwa kutumia cellphone(mobile) ikawa inaita simu ya ndani (landline). huku akiendelea kutangaza. akazuga kusema Catherine pokea simu hiyo.tulikuwa katikati ya matangazo.yote ilikuwa zuga toto aonekane wako wengi kumbe yuko pekee yake.hiyo ndio redio ya uvunguni.

Kudharau kazi za maboksi ni ulimbukeni wa hali ya juu hasa kwetu sisi watu wa mainland, wenzetu wapemba wanazimaliza nyumba za Ilala kutokana na kazi za maboksi.
mkipitia kitabu cha Mzee Mandela " long walk to freedom" mzee mandela anaelezea alivyokuwa akifanya kazi za security ili kujikimu wakati anasoma London.
rais Kwame Nkrumah yeye alikuwa akiosha vyombo hotelini wakati yuko masomoni UK.
kufanya kazi hizo ni kipindi cha mpito ili usurvive ni kutokana na sheria za kibaguzi kuwalazimisha watu wenye students visa kubanwa kufanya kazi za kitaalam lakini ukiwa huna kizuizi kwenye visa yako unapata kazi ya maana.
vyovyote itakavyokuwa mimi nawazimia wabeba maboksi kwani unapata uzoefu mzuri ktk maisha yako. kuna jamaa yangu mmoja yuko UK kaenda kwa scholarship anasema yeye hawezi kufanya kazi isiyokuwa professional yake hata iwe kukaa tu.hivyo anatumbua pesa ya scholarship angekuwa mpemba akiweka pesa ya scholarship pembeni na angejishughulisha na maboksi .

ulimbukeni na ujuvi utatu cost sana wana Mainland. Zanzibarian in UK hivi sasa ndio walioushika mji wanatuma kwao kiasi cha pounds laki 4 kwa mwezi. wastani wa pound laki moja kwa wiki kwa mujibu wa source yangu moja tu niijuayo na wanatumia njia nyingi.
Mkuu Kitila usisikie mtu, beba boksi huko na utakuwa mwenyekiti kama Mandela au Kwame.
 
Redio za bongo inluding Clouds kuna malalamiko ya wenye redio kuwatumia vibaya hasa wasanii wa kizazi kipya kujitajirisha.msanii Juma nature imekuwa ikisemwa sana anatumiwa kama trekta na wenye redio binafsi. wanaaanda kongamano inapatika milioni 100 anapewa 10 unatumia ujanja kumlaghai kutokana na kutokwenda shule. na wahindi wao mbele sana kwenye kanyaboya hili kwa wasanii.

sasa hao waliojiari kama wanawatumia watu kama trekta na kudhulumu jasho la wasanii si kitendo kizuri.
 
Mswahili,

Poa. Unaonaje ukaanzisha topic ya kubeba mabox vs kujiajiri kisha tuchambue mambo huko? Au siyo. Nitakuwa tayari kupambana na baadhi yenu mnaobeba mabox huko majuu bila wasiwasi!!!
Waachie wenyewe hii topic yao tusije tukaiharibu au siyo Muungwana??!

FD
 
Back
Top Bottom