WhatsApp Messenger chat Itanivunjia ndoa yangu..

Ingekuwa unaruhusu PM ningekuja na solution nzuuri kabisa ambayo ingekuondolea stress but naona umesema kabisaa Frobidden,Illegal basi ngoja nikanywe Cappucino sasa

sasa si ndo unataka kunivurugia kabisa ..
Naomba ushauri wako tafadhari
 
Kama we ni kademu ka ukweli, ulipaswa kuchukua namba za hao mademu wenzako, na kuwapigia kuwakanya. Inaonekana ni kademu kaoga.
Mkuu kumpigia demu mwengine kumkanya haisaidi wakati mume ndio fisadi,atajushushia hadhi ya mke bure yeye akomae
na mumewe kama mapenzi azidishe na kama kuongea waonge ili ajue kama anajua vituko anavyovifanya...
 
Once a cheater always will be,

Hata kama ukimkataza whatsapp haisaidii huyo mumeo ni malaya wa kutupwa,kama anamkewe mzuri nyumbani iweje aombe picha za wanawake wengine??

Kaa muongee umweleze anavokuumiza,kama anakupenda sana ataacha lakini kama ni tabia yake ni kama unatwanga maji kwenye kinu.

Kama huna kifua cha kubeba maumivu kwa nini uchokonoe simu ya mwenzio??Kisa cha kujipenguzia siku za kuishi duniani ni nini??

Pole sana dada.

Wanaume wote mlioko kwenye ndoa na walioko kwenye mahusiano,waoneeni huruma hawa wanawake maana wanawapenda sana ila mnawaangusha.

Thanks tian unajua kuna wakati mungu anaamua kukuonyesha kitu ,,,sijawahi kupekuwa simu ya baba watoto ila siku hiyo nilipekuwa na nikasema sirudii ingawa tayari nimeshajua mume wangu si mwaminifu..na ameniumiza sana
mtu hujari hata mogonjwa?
 
Last edited by a moderator:
Pole sana na ww nunua smart phone usevu picha yake kwenye profl na yy mshawishi asev picha yako muwekane bize hayo yapo tu tuliza akili na usw unachunguza cm jiepushe hakuna haja yakugombana mbadilishe taratibu huenda anapenda kuchat tu fanya hivyo
 
Thanks tian unajua kuna wakati mungu anaamua kukuonyesha kitu ,,,sijawahi kupekuwa simu ya baba watoto ila siku hiyo nilipekuwa na nikasema sirudii ingawa tayari nimeshajua mume wangu si mwaminifu..na ameniumiza sana
mtu hujari hata mogonjwa?

Najua kwa vyovyote vile hawezi kukubali kama anawanawake wengine wa nje,

Ukiona anazidisha hiyo tabia yake washirikishe wasimamizi wenu wa ndoa kama wana hekima au la sivyo mpeleke kwa viongozi wa kanisa(kama mkristu) au msikiti(kwa waislamu).

At least hapo maybe anaweza kuchange.Kila la kheri mamito
 
Last edited by a moderator:
Hebu na wew act like unamcheat ili aexperience maumivu unayoyapata.at least inawez punguz maumiv thn mkae chini muongee
note:usifanye kweli
 
@Egyps-women heri ya miaka mipya maana ni kitambo. Karibu na pole kwa hilo. Mie ninamtazamo tofauti kidogo ambao pengine mtanishambulia lakini karibuni. Mimi nadhani sio sawa kutilia mkazo sana kwenye haya ma-Whatapps sijui manini, huwezi kuitumia ile kama ndo kithibitisho cha kuwa mumeo anacheat kisa umekuta anachati mbambo ya mapenzi kwenye simu (pamoja na kuwa ni aina mojawapo ya cheating). Nasema hivyo kwa sababu watu wanawezachat mambo ya ajabu sana na mtu ambaye hata kuonana hawajawahi kuonana lakini katika chat mtu akajikuta wameshavuana na nguo kabisaaa kiWhatsap, whatsapp. Ni makosa ndio lakini ni wangapi wanaelewa kuwa hii nayo ni aina ya cheating? Wengi huwa wanachukulia kuwa ni kiondoleo cha stresses (hasa pale anapoanza na kabla hajafikia kukengeuka kabisa) na kutanabai tayari mtu ushakuwa addicted. So ninakuomba ukae chini na shemeji ongea naye, mweleze unavyoumia na kuwa kama haelewi ile ni aina mojawapo ya cheating ..... mwambie mume wangu hii ni aina moja wapo kama sio kichocheo cha kucheat please acha. Usivunje ndoa kwa sababu ndogo kama hii.............. ukitaka ujue umuhimu wa ndoa, achika.
 
I once was an active member of BBM, WhatsApp and FB. Hii mitandao inatengeneza mazingira flani ambayo si mazuri kutoka kizazi hiki cha sasa hasa mabinti (sorry if I have offended you), wanajilengesha sana mpaka basi!! I have decided to be an inactive member for a while replacing them with JF. In short nitarudi kwenye mitandao hiyo pindi nitakapokuwa na business project(s) ili kuitumia kuadvertise, otherwise.......!!
Ladies and Gents habari za siku nyingi.
nilikuwa busy na kitabu pia family ndio maana nimekuwa Kimya Kidogo
Leo nina tatizo naomba ushauri na msaada kimawazo..
Nimekuwa na mme wangu kwa miaka minne sasa na tumebahatika kupata mtoto ana 2 years old girl
Jmos moja mme wangu alinipa simu yake kuongea na mama mkwe baada ya kumaliza kuongea nikawa najifunza kutumia smart phone ya husb tukiwa kwenye sherehe nilishawishika kuingia kwenye picha na whatsApp pia
Huko nikaanza kuingia kila sehemu..Ile nafika WhatsApp walahi niliumia oho sana
mme wangu alikuwa anachat na wakina dada tofauti tofauti mambo ya mapenzi na kuombana kutumiana picha ...na mengineyo sipendi kusema
Pia nilikuta kwenye Picture profile mme wangu ana picha zaidi ya sita za kina dada waliomtumia kwenye WhatsApp

Nilimuuliza mme wangu hakunipa maneno ya kueleweka ,na mimeshajua mwenzangu ananicheat wakati mie nimejituliza nyumbani nalea mwanangu wa miaka miwili
lakini Bado nimesikia sasa ni kilio cha wanandoa wengi na mahusiano yanavunjika kwa sababu ya hizi wasapu..

Wapenzi niambieni nifanyeje roho inaniuma sana!naichukia ndoa kama ndo kuna usaliti wa hivi

Wenu Egyps
*********
 
tafuta mda mliongee na mwenzi wako kwa mapana huenda hakumaanisha ulikofika wewe,
 
dunia ina hama siku hizi, na ndoa nyingi zinafungwa wakati wa digital, kwahiyo ndoi nazo pia ni digital, cha msingi ni matumizi sahihi ya hiyo mitandao, pole kwa kuumia ila simu ya mkeo/mumeo usipende sana kugusa jamani, muaminiane mtafika mbali, kwanini mnapenda kumkaribisha shetani? tuifanye kila kitu kwa kiasi.
 
Na ww ingia whattsapp uanze chattin...utazeeka na watoto wako shauri lako...dunia inazunguruka hii...au unatumia nokia tochi?
 
@Egyps-women heri ya miaka mipya maana ni kitambo. Karibu na pole kwa hilo. Mie ninamtazamo tofauti kidogo ambao pengine mtanishambulia lakini karibuni. Mimi nadhani sio sawa kutilia mkazo sana kwenye haya ma-Whatapps sijui manini, huwezi kuitumia ile kama ndo kithibitisho cha kuwa mumeo anacheat kisa umekuta anachati mbambo ya mapenzi kwenye simu (pamoja na kuwa ni aina mojawapo ya cheating). Nasema hivyo kwa sababu watu wanawezachat mambo ya ajabu sana na mtu ambaye hata kuonana hawajawahi kuonana lakini katika chat mtu akajikuta wameshavuana na nguo kabisaaa kiWhatsap, whatsapp. Ni makosa ndio lakini ni wangapi wanaelewa kuwa hii nayo ni aina ya cheating? Wengi huwa wanachukulia kuwa ni kiondoleo cha stresses (hasa pale anapoanza na kabla hajafikia kukengeuka kabisa) na kutanabai tayari mtu ushakuwa addicted. So ninakuomba ukae chini na shemeji ongea naye, mweleze unavyoumia na kuwa kama haelewi ile ni aina mojawapo ya cheating ..... mwambie mume wangu hii ni aina moja wapo kama sio kichocheo cha kucheat please acha. Usivunje ndoa kwa sababu ndogo kama hii.............. ukitaka ujue umuhimu wa ndoa, achika.

Mamito za siku nyingi ni heri sana nashukuru mungu na pia asante kwa ushauri mpendwa wangu vip za kwako Dear
Kilichonishitua kwenye wasapu hii ni pale mdada alipokuwa anamuuliza utakuja lini pande hii na yeye kumjibu sasa niko kwa Family ila tutaonana tu hapo kweli si kuwa muzee anachit?
 
dunia ina hama siku hizi, na ndoa nyingi zinafungwa wakati wa digital, kwahiyo ndoi nazo pia ni digital, cha msingi ni matumizi sahihi ya hiyo mitandao, pole kwa kuumia ila simu ya mkeo/mumeo usipende sana kugusa jamani, muaminiane mtafika mbali, kwanini mnapenda kumkaribisha shetani? tuifanye kila kitu kwa kiasi.
kuaminiana kwa style hiyo jamani siku moja unashangaa gonjwa limeingia ndani lilipotokea aaah tulikuwa tunaaminiana
haya ndugu asante kwa advice
 
Egyps-women my dear hilo wala lisikuumize kichwa. Blaming whatsapp wont help. Ukimkataza whatsapp kesho ataingia telegram ambayo ni kali zaidi. Suala sio medium anayotumia bali ni ule uamuzi wa mume wako ku-entertain wanawake wa nje. Hii ni tabia binafsi ambayo lazima aamue yeye kuibadilisha. Utaumiza moyo wako bure msichana mdogo kwa ajili ya hii whatsapp. Potezea tu and just ignore his butt ila umweleze ajue kuwa unafahamu kamchezo kake na hujapendezewa nacho. Usilete bifu nae lakini, mwache. Intelligent people ignore. Hamna kitu kinatuumiza wanaume kama you cheat on your girl and then she doesn't give a hoot. Tunapata picha kuna kinjemba kinatukamulia. Hii pekee ni adhabu tosha kwa mumeo, na atajirudi.
 
Mamito za siku nyingi ni heri sana nashukuru mungu na pia asante kwa ushauri mpendwa wangu vip za kwako Dear
Kilichonishitua kwenye wasapu hii ni pale mdada alipokuwa anamuuliza utakuja lini pande hii na yeye kumjibu sasa niko kwa Family ila tutaonana tu hapo kweli si kuwa muzee anachit?

Mamii mimi niko mzima kabisa MUNGU ni mwema. Sasa mpenzi supposed ungekuta message toka kwa mdada ilimwuliza ... vipi mke mwenzangu hajambo? ungetafsiri vipi? Au Shemeji angeandika, vipi mwandani, umenitesa sana jana kutwa kucha umeniganda mawazoni................ Kama nilivyosema mwanzo ni cheating ya kihisia ambayo inawezapelekea akacheat kiukwelii, but until then huwezimpeleka mahakama ya mapenzi kwa kumshtaki kwa kosa hilo. Pengine yeye halichukulii maanani kiasi hicho. Sikatai kuwa ina madhara but ni vema ukajua kama anajua madhara yake au la!
 
kuaminiana kwa style hiyo jamani siku moja unashangaa gonjwa limeingia ndani lilipotokea aaah tulikuwa tunaaminiana
haya ndugu asante kwa advice

Ni kweli mamii Egyps-women uko sahihi kabisa but ndio maana tunashauriwa kuvunja ukimya pale tunapoona kuna mabadiliko na ku-keep on communicating kukumbushiana mara kwa mara. Kamwe usiichukie ndoa mpenzi kabiliana nayo pale unapoona unaweza.
 
Last edited by a moderator:
ndugu yangu hapo tatizo sio watsap kwasabbu nijuavyo mimi kwenye watsap ni lazima uwe na namba ya mtu ndo muweze kuwa na mawasiliano, sasa je hizo namba za hao wadada mumeo anazitoa wapi? me nnavyohisi mumeo huwa anachat kwenye hii mitandao ya kijamii iliyojaa sikuhizi ya kutafuta marafiki kama facebuk, darchat na mingineyo mingi tu, kwani huko ndiko kunaongoza kwa watu kupenana namba za simu wasiojuana tena waume wa watu wamejazana sana huko kuwalaghai watoto wa watu.

Wengine huishia kujifurahisha tu hivyo kwa mawasiliano ya simu lakini wengine huenda mbali zaidi kwa kukutana na hao wanawake na hata kuanzisha mahusiano, sasa sijui mumeo kafikia wapi.

Kuna mtu amekushauri hapo juu kwamba usubiri uongee nae kwa utulivu lakini labda kama una moyo wa tofauti mimi kwa upande wangu hali kama hiyo utulivu sitauweza na until umenipa majibu ya kueleweka humo ndani kusingekalika, mimi nafikiri kuwa mkali na sio mkali tu bali umuonyesha uko serious hujapendezwa na hicho anachokifanya na asipoacha basi na ndoa hakuna kama hatajali basi ndugu yangu hapo huna mume
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom