Wezi wenye 'leseni ya kukuibia' Kariakoo

Unapoenda kwenye maduka ya simu ya Kariakoo hasa Yale ya mtaa wa Msimbazi. Yanaotazama shule za Uhuru. Jambo la kuzingatia ni kuwa kuna maduka mengi hapo yamejaa wezi na matapeli. Ambao wanatumia loophole za kisheria. Kuibia watu bila woga na polisi hawawezi kukusaidia

Nimeandika hili baada ya kupata experience na nilipofika polisi msimbazi. Ndio nikashangaa sheria zilivyo na why, Hawa wezi wa Kariakoo wanatamba mchana kweupe.

Iko namna hii asilimia 80 ya viduka vinavyouza simu hapo kwanza kabisa. Hawatumii mashine za efd. Wana vitabu vyao vya risiti za kienyeji. Na TRA Kariakoo wanawajua wote. Na jamaa bado wanadunda..

Sasa ikitokea wamekuuzia simu hapo. Mfano unaweza uziwa Samsung ambayo ndani pengine ni Itel au Tecno. Ukistuka Tu mgogoro unaanzia kwa risiti Kiduka kimoja na kina vitabu vya risiti kibao vya majina tofauti

Ikitokea umewabana wakupe risiti ya efd. Ukiwafikisha polisi na kesi ya simu feki. Kwa mujibu wa sheria polisi hawana mamlaka ya kusema simu hii ni feki. Unatakiwa uende Ubungo TBS ndio waseme hii simu ni feki. Otherwise kesi ya kukupa risiti ambazo sio za TRA inabidi uende TRA. Na sio polisi

Sasa hizi loophole za mara nenda TBS mara nenda TRA ndo zinazowafanya. Wajiachie mchana kweupe..
TRA wanacheza nao polisi Msimbazi wanacheza nao..

Matokeo yake watu wengi mno wa ndani na nje wanapigwa maeneo hayo kila siku

Utapeli mkubwa unaofanyika hapo ni huu
1. Simu used kuuziwa kama mpya.

2. Simu brand tofauti Kwa cover ndani mashine simu ingine
Mfano Samsung kwa nje mashine ndani TECNO unaweza kukuta nje LG au Sony Ndani Itel.

3. Simu kwenye cover ni 4g ndani ni 3g au 2g.

4. Utapeli wa kuambiwa tutakurudishia hela yako ukiwastukia.. halafu inaanza njoo kesho njoo kesho...


Ukweli watu wengi wanatapeliwa na serikali ni kama haina msaada kabisa

Nimejiuliza why Polisi wasiwe na vitengo maalum vya kutambua vifaa vya electronics? Vitu kama simu ni Ku Google Tu IMEI no
Je polisi hawawezi hadi TBS Ubungo?

Na Why TBS why wasiwe na ofisi Kariakoo? Kariakoo ni asilimia 90 ya simu za Tanzania zinatoka hapo na zinauzwa Tanzania yote. Watu wa mikoani wanakuja kukusanya. Na wafanyabiashara wa nchi jirani pia. Comoros, Zambia, Malawi n.k, Wanakuja Kariakoo kukusanya

Wangapi watakuwa wanaibiwa na hawapati msaada wa polisi au taasisi yoyote?

Sheria zibadilishwe kuwalinda wanunuzi. Polisi wawe na maaafisa wa TRA na TBS, Hasa pale msimbazi Polisi..

Opereshen maalum ifanyike kusafisha Kariakoo na wafanya biashara hawa matapeli

Ina maana TRA hawawaoni hao? Au ndio wenye hizo biashara?
 
Yaani hakuna mzenji atakaenunua simu nje ya Zanzibar. Kwa sababu huku zinapatikana kwa wingi na hakuna ujanja ujanja kama huko na bei pia ziko chini kidg
 
Vifaa vya electronics na vifaa vya umeme jitahidi ununue katika maduka ya wahindi. Hata kama ni bei kubwa.
Wao huwa hawana longolongo.
Wabongo wenzetu wengi si waaminifu
 
Sasa km ww ni kibabu... kariakoo unatafuta nn wkt wapo watoto na wajukuu wa kuwatuma??hapo nimekuelewa...maana napishanaga na vibabu town,ujaiuliza mjn wanafanya nn?
Sisi ndiyo tumekuleta town alafu unauliza tunatafuta nini?
 
Hawa walinitapeli mwaka jana Samora Avenue mkabala na maktaba ya British Council. Waliniuzia simu mbovu aina ya Vituz kwa 250,000 na t-shirt ya bure. Wanatembea na Noah.
Kweli kuna Shida kubwa sana unanunua cmu mpya mkononi mwa mtu kisha upewe katshirt? Sapna hupajui???
 
kupunguza utapeli, sheria ya umiliki wa silaa ibadilishwe kila mtu awe na chamoto.Hata mnapoanza kuzungumza na tapeli awe anajua fika uamuzi wa juu unaoweza fika pindi atakapoonesha ukaidi.Joking
 
Back
Top Bottom