Wewe umeifanyia nini nchi yako kabla na baada ya kikwete

Raia Mwema

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
535
79
Takwimu zinatengenezwa ili kukidhi matakwa ya kisiasa kwamba tushinde na kukesha tukikosoa wengine bila kujikosoa. Wewe wenyewe (mwanaJF) hujasema umeifanyia nini nchi yako. Ni nini mchango wako kwa chi yako. Hiki ndicho kipimo cha Marekani na kimewafikisha mbali sana. Kwa wenzetu, kushinda kutwa kumjadili mathalan Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete wakati waliharibu mambo ni kupoteza wakati wao wanashinda kutwa kusema Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete waliharibu pale wao wanajadili namna ya kurekebisha.

Wamarekani mmoja mmoja kwa nafsi yake anajikweza kwa kuzungumza alichofanya kwa nchi yake sio tu alichoharibu mwenzake. America wanajitapa mwananchi mmoja mmoja kwa kusahihisha makosa ya mwingine kwamba yeye ameshiriki vipi kusahihisha makosa.


nukuu ya mwanajamii. itapendeza ikiamsha mjadala mpya. wewe umeifanyia nini nchi yako?
 
Mimi nimekuwa nikilipa KODI kabla ya Kikwete na ntaendelea kufanya hivyo hata baada ya Kikwete nikiwa kama raia mwenye mapenzi na nchi yangu!Sasa kipi kitanizuia kuhoji matumizi ya kodi yangu?THINK!
 
hapo zamani niambiwa ccmchoo hata ikiweka jiwe ligombee litaita nimeamini hayo maneno
kwani mpaka sasa tunaongozwa na sanamu la rais
ina maana watanzania waliichagua sanamu ituongoze?
kwa huu mda sio muafaka kwa hilo swali
labda vumilia hii miaka 4 iishe tukipata rais tuulize swali kama hilo
na pia serikali iongozwe na chama na sio kundi la wahuni au la majambazi haya ya sasa.

kwa sasa sina jibu zuri.
 
Kwanza scale ya mshahara wangu inajulikana kwa bunge na kwa wananchi watanzania tofauti na J.K ambaye mshahara wake haujulikani kwa wananchi

Pili mie mshahara wangu unakatwa kodi kila mwezi kwa ajiri ya maendeleo ya nchi yetu

Tatu nawajibika kulipa pesa niliyoitumia kwa kusomea elimu ya juu serikalini ili watanzania wenzangu na watoto wa maskini waweze kusoma tofauti na J.K ambaye hataki kuirudisha pesa aliyoisomea ili wengine wakasome..sasa kama analikataa hili yeye hii nchi anaisaidiaje kama mzawa?
 
Hii kauli sana inatumiwa na mashabiki wa ccm siipendi,maana wamekaririshwa tu hata hawaelewi,
 
Nakatwa kodi ya mshaara wangu(PAYE),Nakatwa kodi directly niagizapo bidhaa kutoka nje(import,port charges,excise duty) tatu nakatwa kodi indirectly ninuapo bidhaa na nne kama muajiriwa nawapa services wanajamii kwa ajili ya kusukuma gurudumu

NB usifikiri kujenga nchi ni kwenda kujenga lami na maghorofa uwape serikali bure si hivyo kama mwananchi kitendo cha kulipa kodi umelitendea haki taifa lako
 
Back
Top Bottom