Wenzetu wamefiwa...

Pole MwenyeNeema kwa msiba wa binti yako.Hiyo ni safari ya sisi wote, kila mwanadamu lazima aonje umauti.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana libarikiwe.
 
Inna Lillahi wa Inna ileyhi Raj'oon...
Verily to Allah we belong & to him we shall return
Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ndio marejeo.

Poleni wafiwa, Mwenyezi Mungu akupe moyo wa utulivu juu ya msiba ulio kupata wewe na ahali zako na familia yako.

Insha'Allah Mwenyezi Mungu akujaalie mtoto mwingine aliye mwema, kwa hakika yeye Mwenyezi Mungu ni muweza juu ya kila kitu.
Amin.


"Surely Allah takes what is His, and what He gives is His, and to all things He has appointed a time...so have patience and be rewarded."
 
Pole mfiwa,nawezaje kukutumia angalau voucher ya mawasiliano,najua pole hapa utazipata za kutosha.
Kt.
 
pole sana!
Mzazi kufiwa na mtoto ni kati ya mambo magumu ambayo hayaeleweki!!
Mtumaini muumba na jiweke mikononi mwake, usikate tamaa, bado una kazi duniani, ndio sababu binti ametangulia, amekuacha.
Jipe moyo, ishi kama muumba anavyotaka tukiwa hapa njiani, kwenye mateso ya kila namna!!
Pole sana!
speechless!
 
Pole mwenye neema, Mungu mwenyewe akutie nguvu. May her soul rest in peace. Amen.
 
Poleni sana ndugu wafiwa. Mola awape nguvu muweze kukihimili hiki kipindi kigumu. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.AMEN.
 
Habari ya huzuni sana
Natamani ningempa mkono wa pole ila kwa sasa nimefulia kwa muda.

Pole sana MwenyeNeema. Mungu awe mfariji wako katika kipindi hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom