Wenye Ukimwi Kuruhusiwa Kuingia Marekani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
3857930.jpg

Rais wa Marekani Barack Obama Monday, January 04, 2010 8:59 PM
Marekani imeondoa kikwazo kilichowekwa miaka 22 iliyopita cha kuwazuia watu wenye virusi vya ukimwi kuingia nchini humo. Rais wa Marekani Barack Obama amekiondoa kikwazo kilichowekwa miaka 22 iliyopita kuwazuia watu walioathirika na ugonjwa wa ukimwi kuingia Marekani.

Rais Obama alisema kuwa kikwazo hiko kilikuwa hakiendani na juhudi za Marekani kupambana na ugonjwa wa ukimwi.

Sheria hiyo mpya ya kuwaruhusu watu walioathirika kupewa viza za kuingia Marekani inaanza kufanya kazi leo na kwa mara ya kwanza Marekani itaandaa kilele cha kujadili jangwa la ukimwi mwaka 2012.

Kikwazo hicho kiliwekwa kwenye miaka ya 1980 kikiwazuia watu walioathirika ambao si raia wa Marekani kupewa viza za kuingia nchini humo.

Marekani ilikuwa miongoni mwa nchi 12 duniani zikiwemo nchi za Saudi Arabia na Libya ambazo mojawapo ya masharti ya viza ni kutokuwa muathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Kuanzia sasa sharti la kupima kama umeathirika halitakuwa miongoni mwa masharti ya uhamiaji ya Marekani.

http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3857930&&Cat=2
 
Hapo wameondoa undumila kuwili. Historia inaonyesha kwamba Marekani imechangia sana kusambaa kwa gonjwa hili,

Leka
 
Back
Top Bottom