Wenye hii tabia siwaelewi kabisaaa!

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
538
Unakuta mtu kakupa lifti kwenye gari yake binafsi, tena wala hukumwomba alafu cha ajabu sasa...barabara nzima anazungumzia mambo ya mafuta, mara oooh nnapokuaga safari huwa nasave hela nyingi sana, mara ooh unajua uzito unavyokuwa mkubwa ndivyo hivyo hivyo gari linavyotumia mafuta mengi sana...sasa mimi nipo humo humo ndani, hivi huwa mnafikiriaje?

kama umempa lift mtu mwenyewe inakuaje tena unajisahau kiivyo mpaka unaanza kuongea maneno ambayo yanamkwaza abiria wako..? kwani nani alikwambia umpe lifti....mi naichukia sana hii hali kwa kweli......
 
Afu siku ya pili akikupa lift unapanda tena! Hapo na wewe tutakuwa hatukuelewi kabisaaaaa!
 
Dah...
Kutembea kwa miguu kuna faida kibao, kunachangamsha akili, kuna nyoosha misuli, kunakufanya uwe na afya nzuri, unajionea vitu vingi kwa ukaribu zaidi.
Kama hauna haraka ya kuwahi uendako, tembea kwa miguuu.

Kama utakuwa na haraka panda daladala. Bora shida ya daladala kuliko masimango ya lifti.
 
Ni vizuri kuchangia mafuta kama mtu anakupa lift. Hata kama hajisemeshi semeshi, tafadhali jitolee kuchangia mafuta kama unaweza.
 
Inawezekana anaongea kwa kuwa ndio kitu alichonacho karibu. Sema watu tunatabia ya kujishuku. Tuache kwanza tabia ya kujishuku
 
Utapandaje ride ya mtu ambaye humfahamu akiwa serial killer je?...inabidi mtu kuwa muangalifu sana,....yaaniw ee mtu anakusimamishia gari anakwambianakupa ride na wewe unaignia tuu na wala humjui huyo mtu?wow!
 
Utapandaje ride ya mtu ambaye humfahamu akiwa serial killer je?...inabidi mtu kuwa muangalifu sana,....yaaniw ee mtu anakusimamishia gari anakwambianakupa ride na wewe unaignia tuu na wala humjui huyo mtu?wow!


Binti maringo huyu sio stranger....ni mtu unaemjua kabisa, hapa town kupanda gari la mtu usiemjua ni kazi sana labda wale walioko sokoni wakijinadi lakini si vinginevyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom