Weledi wa mwanasheria mkuu wa serikali ktk kujibu hoja za wabunge

Godwin Mneng'ene

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
215
83
Najitahidi mara nyingi niwezavyo kufuatilia kupitia televisheni majadiliano ya vipindi vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea huko Dodoma. Nimeshamsikiliza mara nyingi sana huyu mwanasheria wetu wa serikali anapokuwa anajibu hoja zilizotolewa na wabunge kuhusiana na miswaada mbalimbali ambayo inaletwa na serikali ili ipitishwe na Bunge.

Mara nyingi ninapokuwa namsikiliza huyu mwanasheria mkuu wa serikali mara nyingi naona hajibu hoja au anazungukazunguka na kutoa maelezo marefu ambayo hayahusiani na hoja utafikiri na yeye kawa mwanasiasa. Kwa mfano kwenye majadiliano ya leo jioni yaliyoisha hivi punde. Huyu mwanasheria mkuu wa serikali alipokuwa anajibu hoja zilizotolewa kuhusiana na Mswaada wa mabadiliko mbalimbali ya serikali no 2 wa mwaka 2011. Kulikuwa na hoja moja muhimu na nyeti ambayo kuna baadhi ya wabunge waliibua kuhusiana na kutaifisha mali za watu wanaotuhumiwa na mambo ya fedha chafu. Kwamba mtu akiwa anatuhumiwa na kesi kuhusiana na fedha chafu na ikatokea bahati mbaya mtuhumiwa huyo kafariki kabla ya hukumu mali zake zinatifishwa na serikali.

Wabunge wengi walioji inakuwaje mtu hajahukumiwa na mahakama mali yake itaifishwe. Hata mimi niliona ni hoja ya msingi sana kwamba inakuwaje haki za warithi zinaibiwa na serikali na pia how come marehemu aadhibiwe kwa kutaifishiwa mali zake bila kuhukumiwa na Mahakama? nikawa nasubiri kwa hamu majibu ya serikali kuhusiana hoja hiyo. Sasa wakati huyu jamaa anajibu hoja za wabunge suala hili aliliburuza hata hakutoa ufafanuzi wowote, alichojibu ni kwamba wabunge wawe makini sana haya mambo wanayoyajadili ni nyeti mno sasa ndio majibu gani. Nimesikitika sana baadae mswaada huo ukapitishwa na wabunge . Na sio mara ya kwanza, mara nyingi sana nimeshamsikiliza huyu AG anashindwa kujibu hoja muhimu, anategemea kupitishiwa vifungu kwa nguvu ya spika au mwenyekiti wa bunge kwa kuamua kwa kupiga kura badala ya yeye kama mtaalamu kutoa maelezo ya kutosha hadi mbunge mwenyewe akubali hoja badala ya kupitisha kwa kupiga kura.

Nimejifunza vitu viwili hapa kwanza AG wetu ni kilaza au Mfumo wetu wa kupitisha miswaada ya serikali na mfumo wetu mzima wa Uwakilishi sio mzuri hivyo basi AG anautumia udhaifu huo kutojibidiisha kwenye kujibu vizuri hoja, manake anaamini mwisho wa siku lazima hoja hiyo itapitishwa tu kwa kura nyingi za wabunge wa ccm.
 
siyo mwanasheria aliyeiva hata mimi napata shida kumuelewa na hasa aliyemteuwa alitumia vigezo gani mpaka akashika nafasi hiyo nyeti?
 
angalieni historia tatizo halijaanzia hapo, aliyemuweka hapo alishawahi kuweka watu wazuri? na yeye ni mzuri?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom