Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
Najua wengine mtashangaa kwa nini Lunyungu anarudi nyuma lakini ni katika kuweka rekodi sawa .Ziara ya Kiongozi mkuu huyu iligubikwa na matukio mengi sana .Lakini TV yao yaani TBC walijitahidi sana pamoja na Uhuru kuweka sura ambayo si sura yake .Mbeya ilikuwa ngumu .Ilimfanya JK aanze kujibu hoja za JF akiwa Mbeya .Kumbe hawakumweleza ukweli kwamba watu wa Mbeya hawakuwa na beef naye kwa ajili ya Mwandosya bali ni watu wanao taka maendeleo lakini hawako na hawakuwa tayari kuimba wimbo wao wana CCM wa kusema Maisha bora .
Waliamua kuhoji kwa matendo na sauti pia na ndiyo maana JK alipata kushindwa mara kadhaa kusema na wananchi na badala yake akawa anawaita viongozi wa wilaya kataka na tarafa na kusema nao .Alipata bahati ya mkutano mmoja akiwa Mbeya lakini hakuweza tena kuipata bahati ile hadi anamaliza ziara .
Mawe yakarushwa na wananchi kuziba njia akidhani wana hamu naye kumbe walitaka kuona ahadi zake ziko wapi .Kwa mfano Tunduma hakuweza kufika maana hali ilikuwa mbaya na Mbeya mjini ilibidi awe na mikutano ya ndani pekee maana kwingineko anajua moto ulivyo kuwa .
JK ameanza kuamka na kujua kwamba U rais si lele mama na watanzania wamechoka na longo longo na wanataka ahadi za ukweli ?
Wote mnajua yaliyo jiri Mbeya sasa tuendelee kuangalia ilikuwaje ili tumsaidie kumweleza kwamba CCM haitakiwi tena .