Wazoefu zaidi wa biashara

fizo talent

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
2,257
3,882
Habari wakuu...
Niende moja kwa moja kwenye mada ni wakati gani utajua biashara unayofanya imekufa au imefilisika...nimejiuliza hili swali kwa nyakati tofauti na nimeshindwa kupata jibu la moja kwa moja ingawa nimepata mawazo yafuatayo

1)Pindi unapotoa pesa yako katika vyanzo vingine vya mapato na kuingiza ktk biashara

2)Biashara kushindwa kujilipia huduma muhimu kama frem,TRA,leseni

3)Frem kubaki nyeupe na kubakiwa na mashelf tupu au bidhaa chache

Hayo ni mawazo yangu...karibuni wadau je ni kwa wakati gani utajua hii biashara tayari imekufa ni ya kuachana nayo na kuangalia mambo mengine
 
Biashara haipotezi bei ila watu ndo wanapotenza bei.

Mtu anaanza biashara kwa vile wengine wanafanya na hajuwi kwanini wananfanya biashara. biashara ambayo haina malengo lazima ife.

Mtu kufanya biashara mradi nae ana biashara hii lazima iwe chali, yaan una hela alafu unauliza mtu biashara gani naweza kufanya. hiyo ni dalili ya kufeli.

Huna mfumo endeshaji wa biashara yako alafu ukute biashara ndo umeanza lakini unaitegemea kwa kila kitu, hiyo biashara lazima tu ifeki duka litakuwa nyeupe maana kinachopatika kinaenda kwenye matumiz yako binafsi.

Kutaka kuanza pakubwa wakati mteja wako mdogo. yaan business plan yako ni M1 wewe una laki 1, ila unafoce kuanza biashara kwamba utaongeza ukipata hela, hapo utafeli. fanya biashara inayoenda na laki 1.

Salimia watu upate kujua wenzako wanafanya nini hasa katika maswala ya bidhaa wanatoa wapi. masoko yako wapi. bidhaa gani iko kwenye top.

NK……
 
Ukitaka biashara ifanikiwe kwa bongo hii...ukwepe kodi
Chukulia mfano tu...
Ukiwa na vinywaji, hardware, gas..kwenye eneo moja..hizo ni biashara tatu tofaut na halmashauri itakudai kodi, tra itakudai kodi
 
Serikali ndio inadidimiza biashara zetu..tunafanya bas tu ila ukweli tunaumia...
TRA kodi
Halmashauri kodi
Kamisheni (kwa mawakala) kodi
Usafi kodi ( hapa unajiuliza ile ya halmashauri kaz yake nn)
Umeme kodi
Vibali vibali kodi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom