Wazo la kuuza gesi ya kupikia kwa kiwango cha pesa uliyonayo

SECRET AGENT

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
252
488
Habari wana JF
Nimekaa nikawaza biashara ya kuuza gesi kwa kupima kutokana na kiwango cha pesa mtu alichonacho.

Kutokana na maisha kuwa magum mtaani sometimes unakuta mtu ameishiwa gesi kwenda kuchukua mwingine inakua shida kwa mfano mtungi mdogo ni elf 20+ .

Nikawaza mtu aanzishe biashara ambayo atakua na gas points sijui iitwaje ila iwe gas point au vituo ambapo yeye atakua na mitungi mikubwa ya gesi kifupi awe na store kubwa ya gesi kama vile sheli ya mafuta. Na kuwe na mpira maalum wa kurefill gesi kwenye mtungi ambao umeunganishwa na mfumo wa kiditali wa kusoma kiwango cha gesi kama vile mpira wa kurefill mafuta ulivyo.

Mteja ataenda na mtungi wake na atatoa kiwango cha pesa alichonacho, mfano nina elfu tano kwahiyo napimiwa gesi ya kiwango cha elf tano tu. Muuzaji ataingiza gesi ya elfu tano. Inamaana kutawekwa viwango mfano kuna gesi ya elfu moja, elf 2, elf 3 na kuendelea mbele.

Mwenye kufungua biashara hii anaweza kuwa na vituo vingi kwenye miji ili wateja wasisumbuke kufika kwenye vituo hivi vya kuuza gesi.

Nawasilisha. Ni wazo tu nlikua najaribu kuliwaza ila ni wazo ambalo litasaidia sana watu wa maisha ya chini kusurvive.
 
Hilo wazo lishafanyiwa kazi, aliyelifanyia kazi ameshakuwa billionaire na ameshamurder mtu huko mtaani uchunguzi unaendelea.

Wewe tafuta investors ufanye nao pia. Ulete ushindani.
 
Hilo wazo lipo tayari, kama ushasikia kopa gas, ambae mgunduzi wake ana kesi ya mauaji ndio wanafanya hayo umeelezea.

Jaribu tena.
em soma tena, wazo lake tofauti na hao kopa,

pia hao kopa ni wezi, gharama zao ziko juu japo unalipa kiduchu kiduchu
 
Nimepitia tena, ila changamoto naona gharama zitakua juu zaidi.

Ni kama unavyonunua mkaa gunia,

Ukinunua wa makopo utajikuta umetumia gharama kubwa tofauti na kununua gunia, hivyohivyo kwenye gas, ujazo mdogo gharama itakua juu zaidi, kwasababu gharama za uendeshaji zitakua kubwa automatically.
 
Habari wana JF
Nimekaa nikawaza biashara ya kuuza gesi kwa kupima kutokana na kiwango cha pesa mtu alichonacho.

Kutokana na maisha kuwa magum mtaani sometimes unakuta mtu ameishiwa gesi kwenda kuchukua mwingine inakua shida kwa mfano mtungi mdogo ni elf 20+ .

Nikawaza mtu aanzishe biashara ambayo atakua na gas points sijui iitwaje ila iwe gas point au vituo ambapo yeye atakua na mitungi mikubwa ya gesi kifupi awe na store kubwa ya gesi kama vile sheli ya mafuta. Na kuwe na mpira maalum wa kurefill gesi kwenye mtungi ambao umeunganishwa na mfumo wa kiditali wa kusoma kiwango cha gesi kama vile mpira wa kurefill mafuta ulivyo.

Mteja ataenda na mtungi wake na atatoa kiwango cha pesa alichonacho, mfano nina elfu tano kwahiyo napimiwa gesi ya kiwango cha elf tano tu. Muuzaji ataingiza gesi ya elfu tano. Inamaana kutawekwa viwango mfano kuna gesi ya elfu moja, elf 2, elf 3 na kuendelea mbele.

Mwenye kufungua biashara hii anaweza kuwa na vituo vingi kwenye miji ili wateja wasisumbuke kufika kwenye vituo hivi vya kuuza gesi.

Nawasilisha. Ni wazo tu nlikua najaribu kuliwaza ila ni wazo ambalo litasaidia sana watu wa maisha ya chini kusurvive.
Mbn hii kitu ipo mtaani muda mrefu tuu
 
Nyie watu wa kopa gas mnajianzshia vi thread halafu mnaanza kujijbu wenyewe. Kwa kfupi hiyo gas yenu n upuuz kbs gas ya buku huwez pikia wali ukaiva n upuuz kbs bora mtu apambane na ma oryx tu.
Wazo langu sidhan kama ni exact na hao Kopa gas japo siwajui wanavyofanya ila huenda ni tofaut kabisa, toa maoni kwa wazo langu sio siasa za Kopa gas hapa
 
Mwenzio alikuwahi kulifanyia kazi wazo Kama hili,na Sasa Ni bilionea japo hizo billions zimemuingiza matatani.
 
Back
Top Bottom