Wazo la kufungua biashara ya kushusha mafaili GB 1 kwa jero hadi buku kwa kutumia unlimited internet mnaliona vipi?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Kwa hali ya mabando jinsi ilivyo kwa sasa kuna shida kubwa kwenye kudownload mafaili, kufa kufaana mwanangu! penye shida mpya huwa pana mlango wa fursa mpya.

Ttcl hasa kwenye majiji wanatoa unlinited internet ya fiber kupitia nyaya za kwenye nguzo hasa maeneo ya town, unavutiwa waya nyumbani, ofisini au kwenye frem yako kisha unalipia elf 55 kwa mwezi kwa speed ya kudownload GB 7 ndani ya lisaa.

Sasa hapa cha kufanya unaenda town maeneo yenye nguzo za fiber, unakodisha frem hata ndogo tu ya elf 60 kwa mwezi.

Humo ndani utaweka viti kama vitatu, meza na Pc walau iwe na TB 4, wala hakuna haja kujaza vitu, kazi zote zinafanywa kwa PC.

Mtu akihitaji faili unamshuhia hapo hapo ama anaweza kupitia.

-muvi huwa ni takribani GB 1 hadi 3
-Series ndefu huwa ni takribani GB 10 na kuendelea
-windows huwa ni takribani GB 4
-Softwares zipo kibao za size ndogo hadi zenye Gb 20 kama adobe full pack
-Games kama za playstation huwa zinatembea kwa wastani GB 70 (zipo zenye 100+)
-Video za miziki zile HD huwa ni Mb 100 hivi, akiweka miziki 10 ni kama GB

hivi vingi utavipata kwenye mitandao ya torrents kwa hivyo inakubidi uongezee elf 15 ya huduma ya kudownload moja kwa moja kwa spidi ya juu, huduma pendwa huwa ni real debrid.

kuhusu video za youtube hizi unaweza kuzidownload bure.

Muhimu uwe na hard disk kubwa iwe hata na TB 4, vitu vingine sio kudownload kila muda, unavitunza ili mtu akihitaji unamhamishia hapo hapo fasta ila kwa bei zile zile tu za kudownload ama mnaweza kuelewana.

Kwenye bei hapa itategemeana na ukubwa wa faili.

-GB 1 hadi 3 shilingi 1,000 kwa kila GB

-GB 4 hadi 10 shilingi 850 kwa kila GB

-GB 11 hadi 20 shilingi 700 kwa kila GB

-Kuanzia GB 21 na kuendelea shilingi 500 kwa kila GB

-Mafaili yasiyozidi Gb kwamfano faili la MB 500 (GB 0.5), shilingi 150 kwa kila MB 100 (GB 0.1)

MAPATO

tutadeal na huduma ya kwanza tu kwenye hesabu za faida / hasara ili kupata makadirio walau ya kuyategemea kwa kudidimiza hesabu za mapato na kukuza hesabu za matumizi

1. wateja wa ku download mafaili - hawa kwa mwezi unaweza kuwahushia mafali ya takribani TB 1 (GB 1000). kwa wastani hapa inaweza kuwa shilingi milioni 1,

2. Wateja wa mafaili ambayo tayari ulisha download - kwa kuwa pc ina hard disk kubwa, mafaili mengine unayatunza, wateja wakija unawahamishia tu ama unaweza kuzuga una download wapitie badae, mfano kama muvi mpya, series mpya, window mpya, n.k. file moja unaweza hamishia hata watu 10 kuanzia wapenzi wa series, mafundoi computer, mafundi simu, n.k.

3. Huduma za ziada - unaweza kujiongeza ku install windows, games, software n.k.


MATUMIZI

Internet - 55,000
frem - 100,000
vingine - 245,000
JUMLA - 400,000


FAIDA

Mapato ya milioni 1 - matumizi ya laki 4 = 600,000 ( Laki 6 )

Haya ni mkadirio tu.
 
Umeeleweka vema, hapo muhimu kwanza ni location iwe na population nzuri. Na inayofikika kirahisi.
Kwa usawa huu wa mabando hii biashara inatoa huduma yenye uhitaji mkubwa ila hakuna pa kuipata kwa uhakika, naamini mtu akianzisha atajijengea jina haraka na kupata wateja wengi kabla wengine hawajaanza kuiga.
 
Shida internet ya ttcl ni shared. Usitegemee utapata 2mb/sec kama wanavyodai. Utajikuta 1GB unashusha kwa zaidi ya masaa 3 muda ule traffic ikiwa high.

cc Chief-Mkwawa
Internet ya ttcl ni fibre, hii ni internet ia nguvu kuzidi hatainternet ya minara ya simu, kafanye uafiti wako upya mkuu.

Watu huwa wanashusha games za play station zenye GB 70 usiku wakiamka zipo tayari.
 
Internet ya ttcl ni fibre, hii ni internet ia nguvu kuzidi hatainternet ya minara ya simu, kafanye uafiti wako upya mkuu.

Watu huwa wanashusha games za play station zenye GB 70 usiku wakiamka zipo tayari.
Hii game ya GB 70 unaenda itumiaje kwenye playstation.
 
Shida internet ya ttcl ni shared. Usitegemee utapata 2mb/sec kama wanavyodai. Utajikuta 1GB unashusha kwa zaidi ya masaa 3 muda ule traffic ikiwa high.

cc Chief-Mkwawa
Kwa fiber mkuu haijajaa, hizi waya zina capacity kubwa sana mkuu na watu wachache, zuku ukilipa kabla ya kukatiwa ukiwapigia wanakupa double speed kama ulilipia 10mbps wanakupa 20, kama 40 wanakupa 100mbps etc. Wanagawa hizi speed ovyo ovyo sababu network yao haijajaa.

Ila tech nyengine kama mobile data hizi kukiwa na watu wengi speed inadrop sana.
 
Cafe kama hizi mara nyingi inapendeza ikiwa unlimited, ila inategemea unam target nani.

Huwa kunakuwa kuna Cafe zinakuwa na unlimited internet na mtu analipia kwa session, biashara hii huenda sambamba na vinywaji moto na baridi, na bites bites.
maboresho zaidi yanahitajika kwenye cafes kuendana na mabadiliko ya kisasa, inabidi wasiendelee kufanya biashara kimazoea kama zamani enzi za 2010.

Cafes hadi sasa unaweza kuta wanabania kudownload, wafanyakazi wanadhani ni kama vifurushi vya simu nae boss hawaambii ni unlimited,

Kwa watu wanaohitaji mafaili wauziwe kwa kigezo cha Gb na sio muda wa kukaa cafe, ikibidi kuwe na huduma separate ya kudownload tu mafaili, mteja anawatumia link ya file, wao wana download, wakikamilisha wanamcheki mteja aende kubeba file lake.
 
Internet ya ttcl ni fibre, hii ni internet ia nguvu kuzidi hatainternet ya minara ya simu, kafanye uafiti wako upya mkuu.

Watu huwa wanashusha games za play station zenye GB 70 usiku wakiamka zipo tayari.
Hata fiber ni shared, si dedicated
 
Kuna jamaa kafungwa miaka 20 na Faini Milioni 5 kwa kutumia miundombinu ya TTCL kwa nia ovu
Na ndio maana tunajishughulisha kupata vipato vya halali kibongo bongo, ukitumia mitandao kutapeli, kudukua, kuleta uchochezi kwenye siasa za bongo, n.k. ukidakwa jiandae kisaikolojia
 
Na ndio maana tunajishughulisha kupata vipato vya halali kibongo bongo, ukitumia mitandao kutapeli, kudukua, kuleta uchochezi kwenye siasa za bongo, n.k. ukidakwa jiandae kisaikolojia
Yeye alikuwa anasambazia watu
 
Back
Top Bottom