Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,010
Mwaka 2014 ndio unaelekea kututupa mkono na kubaki katika historia. Kuna mambo mengi kama taifa na kama Mtanzania mmoja mmoja tumeyaona katika mwaka huu; mambo ambayo mengine yameacha ladha chungu katika ndimi za fikra zetu. Ni mambo ambayo tumegundua au tumetambua kuwa yameendelea kuwa kweli na kwa namna fulani hatuoni ni vipi mambo hayo yatabadilika hasa katika mwaka huu mpya wa Uchaguzi Mkuu.
Mambo hayo ni ya kweli kwa kutokea kwake, falsafa yake au hata kujirudia kwake. Ni mambo ya ukweli ambayo hatuwezi kuupenda (unwanted truth). Kwa mfano:
1. Kuna watu - na kwa kuangalia kura za Serikali za Mitaa ni wengi - bado wana mapenzi ya dhati na chama tawala na wako tayari kusema, kufanya na kutenda lolote ili kiendelee kuwa madarakani. HILI NI KWELI.
2. Ufisadi umepewa kiti cha enzi; una watumishi wake na una watu ambao wanatoa sadaka zao kwenye madhabahu yake kwa mbinde na upinde. Bado hatujapata dawa ya ufisadi. HILI NI KWELI.
3. Siasa zetu bado ni za mambo ya watu (person-oriented) kulikuwa kuwa siasa za masuala (issue oriented). Bado tofauti zetu zimejikita katika watu zaidi kiasi kwamba unaweza ukaamini kubadilisha watu kunaweza kubadilisha mwelekeo wa taifa. Tumesahau kwa miaka zaidi ya hamsini tumekuwa tukibadili watu kwenye nafasi mbalimbali lakini bado tupo tupo tu. HILI NALO NI KWELI.
Sijui mwenzangu katika mwaka huu unaweza kusema ni mambo gani umeyaona kuwa ni ya kweli na kwa kweli kuyakubai kuwa ni kweli hupendi lakini inabidi uite kikombe kikombe na gudulia gudulia.
Heri ya Mwaka Mpya
Tujiandae kumkoma nyani giledi tena..... mchana kweupe...
MMM