Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Kuna watu wanatembea kwa afya na wameishi maisha marefu sababu ya Wamarekani. Wapo ambao kila mwezi au wiki kadhaa wanaenda kuchukua dawa za ARVs ili kujiongezea Kinga mwilini na kupiga vita magonjwa ambukizi mbalimbali.
Madawa na tiba hizi zimetoka kwa msaada wa watu wa Marekani (na mimi mmojawapo). Ingekuwa wanataka kutupunguza kwa haraka hakuna pazuri kama pale tupapendapo!! Jinsi masikini wetu wanavyopenda kula na kulana, kulala na kulaliana, kutafuna na kutafuniana; maelfu kama siyo mamilioni ya maskini Hawa wangekuwa wamepumzika ahera madukani siku nyingi.
Tuache ufyatu!! Waacheni wazazi au jamii wanaotaka watoto wao wale chakula cha msaada. Tulikula sisi miaka ya themanini na tunashukuru. Wazazi au jamii wasiotaka kula wasilazimishwe. Wazazi wawakataze watoto kula chakula Nicholas. Lakini kuwanyima watoto na wazazi wengine wasio na tatizo na vyakula hivi ni ufyatu . Tukifika mahali kweli tu tunajitegemea kwa chakula tunaweza kukataa kwa sababu ya kutokujiabisha. Sasa hivi msemo wa wahenga "mwenye njaa hana haramu" una ukweli wake.
Nashauri serikali iache hamaki, itulie na kufikiria tena a more balanced approach. Tusiwe wote hamnazo.