Wazito PPF wachota ‘vijisenti’

Status
Not open for further replies.
Mwaka 2008 kulikuwa na mjadala ulikufa bila kujadiliwa kwa kina kuhusu wakurugenzi wa mfuko wa pension wa PPF waliojichotea takribani shilingi milioni 200 kila mmoja. Hali halisi ni hii hapa

1. HAO WALIOORODHESHWA MWAKA 2008 kwenye JF SIO WALIOJIGAWIA MILIONI 200. BALI NI WAKURUGENZI WA NDANI SIO BOARD MEMBERS ambao ni.Director of Finance, Chief Internal Auditor, Director of Computors, Director of Commercial Services, Director of Investiments, na Director of Pensions.
2. Mhasibu mkuu aliwagomea kulipa kwa kuwaambia sio haki yao kwa kuwa wao ni wa mkataba wanalipwa gratuity 25% ya mishahara yao kwa muda wote wa mkataba, wakamsimamisha kazi kwa vitisho vya kutaka kufukuza na kumhamisha idara. Toka June 2008 hadi March 2010 amehamishwa mara nne. Hivi sasa wamemtupa Mbeya asione madudu yao
3. Mafao waliyojilipa haikuwa stahili yao, kwani mafao hayo yapo kwa wafanyakazi wa kudumu tu pale wanapofikia umri wa kustaafu (55 years) na wawe wanaondoka kabisa PPF sio kama walivyofanya wao ambapo bado wanaendelea na kazi na karibu wote wana umri chini ya miaka 50.

4. Mwezi wa tatu 2011 wanamaliza mkataba mwingine watavuta kila mmoja karibu milioni 100 kama serikari ikiwaachia waibe tena.
5. Audit commettee ya bodi ya PPF walijua kuwa ni wizi, wakapelekwa Johanesberg kunyamazishwa.
6. Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikari alipigwa dongo la macho kusaini mahesabu ya 2008. Wakaguzi kutoka TAC walijaribu kuijia juu menejimenti ya PPF, lakini wakapewa vijisenti wakanyamaza kimya. Draft report yao tunayo ilionyesha wizi huo lakini ripoti ya mwisho haikuwekwa.
7. Mishahara kupanda kila mwaka kwa asilimia 25%.
Baada ya kuiweka bodi ya wadhamini mifukoni mwao, wamekuwa wakijiamulia mambo wenyewe. Wakurugenzi wana mishahara mikubwa, wakati walalahoi ndani ya mfuko huo huo wanasota. Kila mwaka wao hujiongezea kati shs. Milioni moja na nusu na mbili na nusu wakati wafanyakazi wadogo kuanzia mameneja kushuka wanaongezewa kati shilingi elfu kumi na elfu tisini tu. Usawa uko wapi? Waziri wa fedha anajua hili?
8. Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu aliitisha mkutano wa wafanyakazi akaruhusu maswali. Mfanyakazi mmoja alihoji kwa nini wakurugenzi wajiongezee mamilioni yote hayo wakati walalahoi wanapewa kiduchu? Aliulizia pia uizi walioufanya March 2008 wa kugawana shs.200m ambao wataurudia March 2011, kwa nini wapewe wakurugugenzi wasiostahili kabla ya umri wa kustaafu wa miaka 55? Masikini mzee wa watu, katibua hivi ninapoandika amesimamishwa kazi kwa kuhoji ufisadi wa wakurugenzi wa PPF.
9. NAOMBA PCCB, USALAMA WA TAIFA, SERIKARI-WIZARA YA FEDHA, UTUMISHI, WANAWAKE NA JINSIA WAINGIE PPF NA KUCHUNGUZA. WASIMWOGOPE DG KWA SABABU NI MTOTO WA MZEE MKAPA.

MALIPO HAYA NI NJE YA GRATUITY 25% TSHS 48M, NA PENSION 20% ZAIDI MILIONI 70
NAOMBA KUTOA HOJA
Naam,leo ni 31/03/2011.
 
Jamani jamani hii nchi inakwenda wapi?

Mbona wamefanya tena? Harafu ni wale wale?

Mkurugenzi wa Fedha Martini Mmari, na Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani (Boys' two MEN) walilipwa 2008 kwa uizi hawakukamatwa, wakajifanya wamemaliza mkataba. Tarehe 31/03/2011 umeisha mwingine wameanza mwingine. Hivi kuna haja gani ya kuwaita wa mkataba wakati wanajiendelezea bila kufuata taratibu za manunuzi?

Wamevuta nyingine 200M each.

Hawa wawili ndio waliojiuzia viwanja vinne vya PPF kwa 16M kwa vyote bahari Beach na kuporomosha maghorofa.

Zitto una kazi ya ziada

UTOUH una kazi. Tumia wakaguzi wengine sio TAC wala Deloit and Touche, wote ni wezi tu

Wazito PPF wachota ‘vijisenti’

Mwandishi Wetu Mei 7, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Walipwa kama wastaafu, kisha warudi kazini

WAKURUGENZI kadhaa wa Mfuko wa Pesheni ya Mashirika ya Umma (PPF), wamejilipa mamilioni ya fedha, ikiwa ni mafao yao ya kustaafu kazi, lakini imebainika kuwa wanaendelea na nyadhifa zao licha ya kujilipa.

Habari ambazo Raia Mwema imezipata wiki hii zinasema kuwa mafao ya wakurugenzi hao yanafikia kati ya Sh. milioni 130 na 220 kwa kila mmoja, kiwango ambacho kinafikia jumla ya Sh. bilioni 1.2, kilichotolewa na PPF kwa ‘wastaafu’ hao.

Raia Mwema imearifiwa kuwa malipo hayo yamefanyika kwa kufuata utaratibu uitwao Group Endowment Scheme, ambao unahusu mafao ya wafanyakazi yanayopaswa kutolewa kwa mtumishi anapostaafu kazi katika PPF.

Kwa mujibu wa habari hizo, chini ya mpango wa Group Endowment Scheme, wafanyakazi hukubaliana na mwajiri kabla ya kuanza kazi, ambapo shirika linakuwa linachangia kiasi fulani cha fedha kama akiba ya mfanyakazi, ambayo hupewa mara anapostaafu.

“Mnakubaliana wewe mfanyakazi na mwajiri. Ni kama mkataba wa aina fulani. Shirika linatoa fungu, linakuchangia…Unapoondoka kazini wakati unastaafu, unapewa fedha zako ili zikusaidie kwenye maisha yako mengine.

“Ukipewa fedha chini ya utaratibu wa Group Endowment Scheme, hatutarajii kuona mhusika anabaki kazini. Kama kuna watu wanafanya hivyo, basi wanauhujumu utaratibu huu,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa PPF, Naftali Nsemwa, ambaye aliombwa na Raia Mwema kutoa ufafanuzi wa jinsi mpango huo unavyofanya kazi.

Lakini Raia Mwema imeambiwa kwamba katika jambo ambalo linashangaza, wakurugenzi hao sita wa PPF wamejilipa mafao hayo ya Sh. bilioni 1.2, kwa maana ya kustaafu, lakini hadi jana Jumanne walikuwa wakiendelea na kazi, wakiwa tayari wameweka mafao yao vibindoni.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Badru Msangi, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alikiri kuwapo kwa utaratibu wa Group Endowment Scheme, lakini akakataa kuzungumza zaidi kwa maelezo kuwa yeye si msemaji wa PPF, bali Mkurugenzi Mkuu mwenyewe, William Erio ambaye yuko safarini Afrika Kusini.

Hata baada ya kumsihi azungumze, Msangi alisema: “Msubiri Msemaji wa Shirika, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu. Atakuwepo ofisini wiki ijayo. Unapotaka sisi ndio tuzungumze, hututakii mema, unataka tufukuzwe kazi.”

Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Gray Mgonja hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, na hata pale Raia Mwema ilipojaribu kuwasiliana naye, simu yake ilikuwa ikiita mfululizo na baadaye ikafungwa.

Raia Mwema ina majina ya wakurugenzi hao lakini kwa kuwa haikufanikiwa kuzungumza nao kuoata maelezo ya upande wao kwa sasa hawatatajwa.

Habari zaidi zilizopatikana zinasema kulipana huko kumehojiwa na mmoja wa wajumbe wa Bodi ya PPF, Monica Mbega akitaka kujua ni nani aliyeyaidhinisha.

Mbega alihoji suala hilo katika mkutano wa Jumamosi iliyopita wa timu ya ukaguzi ya Bodi ya PPF ambayo yeye ndiye Mwenyekiti wake. Yeye na Erio, na baadhi ya wakurugenzi ambao ni wajumbe wa timu hiyo, wako safarini Afrika Kusini.

Mikataba ya Group Endowment Scheme katika PPF imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka mitatu, na mwenye kufaidika na mpango huo anapaswa kuwa awe anastaafu na kuondoka kabisa katika ajira ya PPF.
 
Hivi CAG hili limemshinda?

Naomba kuuliza huyu William Erio au Eriyo (lazima kuna tofauti) Si ndio Ndugu au anauhusiano na William Benjamin Mkapa au Mama Anna Mkapa?

Siye aliyewekwa kindugu hapo? au nimekosea?

Huyu W Erio ndiye mjomba wa WB Mkapa sasa kuna kitu hapo alafu swali linafuata sio uwajibikaji wa Government machineries na CAG in particular kazi haionekani kabisa ila majigambo ndio mengi sana kuwa madudu ya mashirika haya ni hapa lakini hili PPF juu ya endowment hakuna majibu mpaka leo. Hapo kuna kazi kweli???
 
Kuna mambo yanafanyika Tanzania tu,huwezi kusikia yakifanyika mahali popote pale katika dunia hii.
 
Kuna mambo yanafanyika Tanzania tu,huwezi kusikia yakifanyika mahali popote pale katika dunia hii.

Kibugumo usiwe na wasiwasi, Serikali wala haijalala inaenda hatua kwa hatua. PPF soon itahamishiwa rasmi WIZARA YA KAZI NA AJIRA badala ya wizara ya fedha.

Kwa maana hiyo tutegemee uwajibikaji maana mama Kabaka ni jembe, timu yake iko vizuri, Ukichanganya na SSRA oh! mbona kumekucha. Wanachama wa PPF sasa kilio chenu kitasikilizwa. Miungu watu wajiandae..

Mungu ibariki Tanzania.

Queen Esther
 
Kibugumo usiwe na wasiwasi, Serikali wala haijalala inaenda hatua kwa hatua. Sasa PPF imehamishiwa rasmi WIZARA YA KAZI NA AJIRA ikitokea wizara ya fedha.

Kwa maana hiyo tutegemee uwajibikaji maana mama Kabaka ni jembe, timu yake iko vizuri, Ukichanganya na SSRA oh! mbona kumekucha. Wanachama wa PPF sasa kilio chenu kitasikilizwa. Miungu watu wajiandae....

Mungu ibariki Tanzania.

Queen Esther

Tena QE hapo ss madudu yote ambayo wamekuwa wanayafanya pale PPF under MOFEA kula dadadeki kwa Waziri Kabaka na SSRA Irene hayatapewa pumzi kabisa ni bora wanze kuli-resign kabla ya mizuka ya good governance na responsibility ikaanza kukata kama msumeno, nobody will survive there.
 
Mh. Waziri wa Fedha Mama Saada

Umeagiza watu waadilifu wakujulishe wezi wa Mashirika ya UMMA. Anza na PPF.

Waliiba zaidi ya Bilioni 2 kupitia Group Endowment. Wakawafukuza kazi wale waliokuwa wakiwapinga uso kwa uso mafisadi hawa wakiongozwa na DG Bw. William Erio akisaidiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa wakati huo na sasa amerudishwa tena.

PPF ijiandae kulipa mamilioni kwa kufukuza wafanyakazi bila kosa, tayari wameshalipa 800 milioni kwa mmoja licha ya pesa walizochezea kuwalipa mawakili, ambao inasemekana Bw erio ni shareholder wao.

Fanyia kazi tukiona uko serious, tutakuletea mengi
 
Hii nondo imekaa vzuri na imegonga ikulu Kubwa ya Ppf kwa haya yote yaliyotolewa na Okoanchi! Wadau karibu kwenye jamvi la kuokoa shirika!
 
Mh. Waziri wa Fedha Mama Saada

Umeagiza watu waadilifu wakujulishe wezi wa Mashirika ya UMMA. Anza na PPF.

Waliiba zaidi ya Bilioni 2 kupitia Group Endowment. Wakawafukuza kazi wale waliokuwa wakiwapinga uso kwa uso mafisadi hawa wakiongozwa na DG Bw. William Erio akisaidiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa wakati huo na sasa amerudishwa tena.

PPF ijiandae kulipa mamilioni kwa kufukuza wafanyakazi bila kosa, tayari wameshalipa 800 milioni kwa mmoja licha ya pesa walizochezea kuwalipa mawakili, ambao inasemekana Bw erio ni shareholder wao.

Fanyia kazi tukiona uko serious, tutakuletea mengi

ERIO William mototo wa Rais Mstaafu William Mkapa haguswi. amedokoa weeeeeeee, no one dares to touch him.

Ila naamini kuna siku atadakwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom