Waziri wa zamani, Chadiel Mgonja afariki

Well, Jasusi

Unajuaje Mgonja hakukubaliana na uamuzi wa Nyerere ila alibeba tu ujumbe?
Wewe Kuhani kweli kweli! kwi!kwi!kwi!
Kweli siwezi jua kama Mgonja alikubaliana au hakukubaliana na uamuzi wa Nyerere, lakini inavyoonekana hakuwa originator wa idea ya kuitambua Biafra.
 
Wewe Kuhani kweli kweli! kwi!kwi!kwi!
Kweli siwezi jua kama Mgonja alikubaliana au hakukubaliana na uamuzi wa Nyerere....

No further questions there.

Turudi kwenye issue ya ngono.

Mgonja ameshutumiwa kufanya mapenzi na watu ovyo wakiwemo wasichana wanaosemekana kuwa wasio na umri wa kujiamlia ngono, kinyume na utamaduni na maadili yanayotegemewa kutoka kwa kiongozi wa Umma.

Una utetezi wowote juu ya mtuhumiwa?
 
Last edited:
No further questions there.

Turudi kwenye issue ya ngono.

Mgonjwa ameshutumiwa kufanya mapenzi na watu ovyo wakiwemo wasichana wanaosemekana kuwa wasio na umri wa kujiamlia ngono, kinyume na utamaduni na maadili yanayotegemewa kutoka kwa kiongozi wa Umma.

Una utetezi wowote juu ya mtuhumiwa?
Kuhani,
Hilo silijui. Nilisikiaga rumours kama wengine na ndiyo maana sikutaka kulizungumzia kwa sababu sina uhakika nalo. Kwa hilo sina utetezi kabisa.
 
Mgonja anazungumzia misukusuko ya kesi ya uchaguzi iliyomvua ubunge wa Same.

"
wote walionitakia heri walisisitiza kwamba nguvu sana imani yao kubwa na uhakika wao kuwa Raisi Mwalimu Julius Nyerere angechukua hatua za kurekebisha mambo na kunifanya mtu huru tena. kwa hiyo, mimi niliumia zaidi kwa kuwahurumia watoto wangu na watu wengi ambao waliteseka mioyoni mwao kwa sababu yangu na wakajitolea mhanga kwa hali na mali kunisaidia na kunitakia heri. Yaliyonipata mimi mwenyewe moja kwa moja, hayakuniumiza kama kule kushuhudia watu wengine wakimumia kwa sababu yangu. watu kadhaa wakiwepo wazee kutoka wilaya ya Same walijitolea wakasafiri mpaka Dar Es Salaam ili kuwasilisha risala yao kwa Raisi kuhusu ukweli walioujua kuhusu yale yaliyonipata. baadaye mimi mwenyewe nilipata fursa ya kumtembelea Mwalimu Julias Nyerere naye akanionyesha huruma kubwa kuhusu matukio yale. mimi ni shahidi mmojawapo niliyeona wazi kuwa Raisi Mwalimu Julias Nyerere ni mtu aliyekuwa na msimamo usioyumba ktk suala la kuutetea ukweli na wa kuwahurumia na kuwasaidia watu wote, haswa wale wenye shida. Tamko la kuniteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, lilinipa ushindi mkubwa kwa vile dunia ilielewa wazi maoni yake. kuanzia hapo, nilijisikia nafuu kubwa sana. hatimaye, Raisi Mwalimu Julias Nyerere, aliitumia mbinu ile ya kutamka msamaha 1984 kwa hayo makosa yaliyotajwa kuwa niliyafanya. ilikuwa kama muujiza kwangu. "

C.Y.Mgonja "Johari ya Maisha yangu"
 
Kuhani, Fundi Mchundo,

Naona mnasisitiza kwamba inakubalika kusema mabaya ya marehemu wakati bado hata hajazikwa! Ni maadili yetu kweli hayo?

Ni haki kumshtaki marehemu? Ndugu zake wanaofanya mipango ya mazishi watajisikiaje? Hawastahili pole? Hata kama marehemu alifanya makosa, ni sawa kweli kuwaongezea ndugu zake uchungu wa kumsema vibaya marehemu?

Kuhani anasema natetea ngono. Si kweli. Humu JF nina rekodi ya kuwasuta sana wakubwa wenye tabia chafu. Wengi mtakumbuka kwamba moshi mweupe ulipoonekana Dodoma nilipinga vikali nikisema: "Mtu ambaye hawezi kuwa aminifu kwa familia yake atakuwaje aminifu kwa taifa zima?"

Itafika siku ya kuanisha mchango wa Chediel Mgonja kwa Tanzania. Lakini kwa sasa tumpe tu heshima anayostahili kutokana na ukweli kwamba kaumbwa kwa mfano wa Mungu.
 
Mi nina maswali mawili bwana\bibi Moshi,

1. Kwahiyo sasa hivi watu tuongelee mazuri tu huku tukiwafariji wafiwa, tuwafariji bila kumuongelea marehemu au tuwachunie tu?

2. Kusema mabaya/mazuri ya marehemu kabla hajazikwa na akishazikwa kuna tofauti ya uchungu kwa wafiwa?

Kwa maelezo yako ni kwamba leo fisadi kama mkapa akianguka (simuobei kifo) kabla ya kuzikwa tunatakiwakumpa sifa tu kwamba alikuwa kiongozi bora na muadilifu lakini wakishazika tuendeleze libeneke. Hiyo itakuwa inatuelezeaje sisi tuliohusika katika kumuongelea wakati wa uhai, kabla ya mazishi na baada ya mazishi? itakuwa unafiki tu. Watu wasimeseme mabaya marehemu lakini waseme wasifu wake kama wasifu wake una mabaya ndani yake hiyo ndio inatuonyesha alikuwa nani.
 
Ukweli utabakia ukweli tu, kama mtu alikuwa firauni alikuwa firauni tu, kama amezikwa au hajazikwa haibadilishi kitu.
 
Kuhani, Fundi Mchundo,

Naona mnasisitiza kwamba inakubalika kusema mabaya ya marehemu wakati bado hata hajazikwa! Ni maadili yetu kweli hayo?

Ni haki kumshtaki marehemu? Ndugu zake wanaofanya mipango ya mazishi watajisikiaje? Hawastahili pole? Hata kama marehemu alifanya makosa, ni sawa kweli kuwaongezea ndugu zake uchungu wa kumsema vibaya marehemu?

Kuhani anasema natetea ngono. Si kweli. Humu JF nina rekodi ya kuwasuta sana wakubwa wenye tabia chafu. Wengi mtakumbuka kwamba moshi mweupe ulipoonekana Dodoma nilipinga vikali nikisema: "Mtu ambaye hawezi kuwa aminifu kwa familia yake atakuwaje aminifu kwa taifa zima?"

Itafika siku ya kuanisha mchango wa Chediel Mgonja kwa Tanzania. Lakini kwa sasa tumpe tu heshima anayostahili kutokana na ukweli kwamba kaumbwa kwa mfano wa Mungu.

Katika makabila mengi kuna institution inaitwa watani. Hawa ndiyo wanaosaidia katika kuandaa shughuli za matanga maana wao ndio wanaopika, kuosha vyombo na kuhakikisha kuwa watu hawalali. Lakini jukumu lao lingine ni kuwapasha wafiwa. Kwa kutumia lugha ya utani wanamchambua marehemu, familia yake, ukoo wake na kabila lake. Hawa hawasiti kuyazungumzia maovu ya marehemu bila kificho. Kama marehemu alikuwa mwizi wanasema. Makabila mengine wanatumia nyimbo. Wakati wa matanga zinimbwa nyimbo kumuelezea marehemu ( marehemu hakuwa anahudhuria misiba ya wenzake n.k.), mazuri na mabaya yake. Nyimbo hizi vile vile zinatumika kuwakanya na kuwachambua waliobaki. Hii ndivyo ilivyokuwa. Hii ya kwenu ya kudai kuwa marehemu asifiwe tu inatoka kwa wageni. Huko ndiko kuna tamaduni za eulogies.

Hilo la kuwa kaumbwa kwa mfano wa Mungu ni lako. Si wote humu wanaomwamini Mungu. Na hata katika hao wanaoamini kuwa kuna Mungu wanaamini kuwa sote tumeumbwa kwa mfano wake. Hata wale watoto tusiowatendea haki. Mnataka tungoje mpaka lini kueleza mapungufu yake? Wakati huo si mtatuambia kuwa tumwache apumzike kwa amani na mwenye hukumu ni mwenyezi?

Kwa nini unawaonea huruma ndugu zake na kusahau wale waliokuwa victim wake? Ni wangapi ambao wakisikia habari hii watakumbushwa yaliowapata mikononi mwake? Hao nao hawastahili sympathy yetu? Au kwa sababu machozi yao hayawekwi kwenye luninga?

Mimi nakazania kuwa lazima hizi shutuma zisemwe ili ziwe onyo kwa wale waliobaki. Nitawaelewa kama mtasema kuwa marehemu alikuwa anasingiziwa. Lakini hili la kusema huu si wakati wake silikubali. Thika.

Amandla.........
 
watanzania wenzetu wakiona barabara za milimani wanafikiri tumejengewa na cleopa msuya kwa kuiba tuko hazina ya serikali. kutoka ktk kitabu alichoandika kuhusu narakati zake za kisiasa chedieli mgonja anatoa maelezo haya.

"mbinu zilizotumika kuzichimba barabara zote za milimani zilikuwa ni karibu sawa. kila mahali walitumia mila ile ya kuweka siku maalum kwa wananchi wote kufanya kazi kwa pamoja, kwa manufaa yao wote. kazi za ina hiyo ziliitwa za "MISARAGAMBO." mila hiyo ilikuwa na nguvu sana. karibu wananchi wote walishiriki kwa moyo mkuu na kwa furaha. wachache walioacha kuhudhuria kutokana na utegaji au uzembe, walipigwa faini ambazo zilikuwa zinajulikana sana kama vile kuchukuliwa kwa kuku, mbuzi au hata mali nyingine iuzwe na mapato yatumike kuendeleza "MSARAGAMBO." barabara ya kwenda milimani vudee na ndolwa ilitumia nguvu nyingi za wananchi ambao waliiichimba kuanzia 1961 mpaka gari la kwanza lilipoweza kuingia milimani vudee mnamo mwaka wa 1969. gari hilo lilikuwa la serikali na liliendeshwa na dereva ayubu wa Same Bomani. "

"barabara ilikuwa imefika mahali pagumu kuliko kote, wakati Mwalimu alipafanya ziara yake hiyo ya pili. ilikuwa imefika ktk jabali kubwa liitwalo mhewe. jabali lenyewe lilikuwa limesimama wima sana na lilienea umbali upatao robo kilometa. ilikuwa imeleta picha kuwa bara ulifika hapo, ikaingia kwenye jabali na kukwama kabisa isiweze kuendelea tena. hata mimi mwenyewe, ambaye nilishirikiana na wananchi kuichimba barabara hiyo ktk vipindi mbalimbali kwa miaka mingi, moyoni nilikuwa na mashaka kuwa huenda tusiweze kupita mhewe. lakini sikuthubutu kumweleza mtu yeyote mashaka yangu hayo.

wananchi walikuwa na ari na moyo mkubwa sana ingekuwa ni kuwaumiza sana kujaribu kuleta wazo la kushindwa. risala ya wananchi kwa raisi mwalimu Nyerere ilisomwa kwa moyo mkuu na kwa ukakamavu sana, na mwanamke mwalimu napendaeli mgonja, mwalimu wa shule ya msingi vudee, hembua. akisoma risala alimwonyesha Raisi lile jabali la kutisha na akamweleza kwa imani kuwa juhudi za wananchi zilikuwa zimewafikisha pale, na kutokana na uamuzi wa dhati wa wananchi, jabali lilikuwa na wasiwasi mkubwa, kwa vile hi hakika watalipasua na kupitisha barabara hiyo."

"MWALIMU NYERERE aliagiza serikali itoe msaada ikiwa ni pamoja na baruti za kupasulia mawe ktk kukamilisha barabara ile. alifanya hivyo wakati akijibu risala ya wananchi. ni siku hiyo pia ndipo aliwaita wananchi wa Wilaya ya Pare kuwa ni "Wachina wa Tanzania, " na akaongeza kusema, kama ingeliwezekana, angewaleta Watanzania wengine waione kazi hiyo ya ajabu iliyokuwa inafanywa na wananchi waliojizatiti kujipatia maendeleo"

maelezo haya yanapatikana ktk kitabu "JOHARI YA MAISHA YANGU" C.Y.MGONJA
 

Tanganyika‐Zanzibar Union Cuts U.N. Members to 112


  • May 14, 1964
UNITED NATIONS, N. Y., May 13—United Nations membership dropped from 113 to 112 today with formal notification to the Secretariat that Tanganyika and Zanzibar had united under a single Government.

The two East African countries signed an agreement April 23 to unite, with President Julius K. Nyerere of Tanganyika as President of the new United Republic of Tanganyika and Zanzibar.”

Chedial Yohane Mgonja of Tanganyika and Muhamad Nassor Abdulla of Zanzibar called on the Secretary General, U Thant, and notified him formally of the union.

The Tanganyikan mission said that a decision on the design of the flag for the union was expected by June 1.

cc Taisho fuyaki
 
Back
Top Bottom