Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, MUONGO

....aisee wee jamaa kwa kukariri ligi........!.....sasa unamtaka SMU ili uendeleze ligi au....?

Hakuna ligi hapa, watu wanajadiliana tu, hujui kuvuta hisia katika mada. Nilikuwa wala sina haja SMU aje. Soma na kisha fikiri ndio ujibu. Nani katangaza kuwa kujadiliana hapa JF ni ligi?, na kama itakuwa hivyo kwamba mtu akijadili kitu ni ligi, basi mijadala itakufa hapa JF, na mijadala ikifa ina maana hakuna haja JF iwepo. Soma vizuri kabla hujajibu kitu, ama unaongeza "posts".
 
Hii thread ina kichwa cha habari "Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, MUONGO". Mimi kule kwa thread ya "JK amteua Jaji Kiongozi mpya" nilitumia neno Muongo, Mkuu SMU aliniomba niliombe radhi, SMU upo?, manake limetumika tena.

Nipo Mkuu Mfumwa

Nadhani mtoa mada amepata ujumbe wako. Ingekuwa vema kama mtoa mada angetuonesha kinaga ubaga kwamba bwana Membe kwa makusudi alitupotosha kwa kutupa taarifa isiyo sahihi. Nimejaribu kusoma hiyo post yake bado sijaona kama amefanya hivyo.

Kama wewe ni muungwana (au unataka kuwa muungwana) basi usijilinganishe na wasio waungwana. Ni hayo tu kwa sasa.
 
hii thread ina kichwa cha habari "waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, muongo". Mimi kule kwa thread ya "jk amteua jaji kiongozi mpya" nilitumia neno muongo, mkuu smu aliniomba niliombe radhi, smu upo?, manake limetumika tena.

Tukija kwa mada viongozi wetu hukulupuka mno. Watatue matatizo ya wapemba hayatakuwepo hayo wanayotueleza eti kuwa kuna watu wamepanga kuvuruga ziara ya ban. Wanaogopa nini ujio wa ban kuvurugwa kwa mfano mabango, manake wale wazee sidhani kama walikuwa watumie nguvu yotote, badala ya kuogopa yanayofukuta kule pemba. Hawa tatizo wanafagia na uchafu kuutumbukiza chini ya zulia.

natumaini wana jf ndiyo tunatakiwa kupima thread ya uongo kulingana na hoja na siyo mmoja wetu anakurupuka membe ni muongo bila hoja hayo ndiyo tunasema matusi. Hoja ni kipimo kizuri cha ubora wa thread, kipimo cha kutenganisha ukweli au uongo. Kumuita mtu muongo bila hoja muongo atakuwa ni yule anayetuhumu wengine bila hoja
 
CCM iache kutafuta visingizio vya kumwaga damu,ilifanya majaribio ya Tarime,Kiteto,Ujambazi,Albino na sasa Wapemba.Wasifanye maandalizi mengine ya kuiba/kununua kura kwani Zanzibar haikubaliki na Bara wakibaatisha Urais,Wabunge wa upinzani watakuwa wengi.Watanzania mjiandae kupinga kura ya kuikomboa Nchi yetu mikononi mwa manyang'au.
 
watu kama membe na wa aina yake wote,ambao kwenye magazeti yote ya kila siku NDDIO MISALABA YA JK!aliamua kuingia nayo,ataenda nayo NA ATONDOKA NAYO..!misalaba mizitomizito ANAIDROP kama mnavyoona,mingine anasonga nayo MDOGOMDOGO!!.............hatujui itakuwaje kwa sasa...lakini twende tu

WATU WALIOKAA KWENYE KIZA KINENE SASA WAMEONA MWANGA MKUU!
 
Membe yeye kiherehere chake zaidi ni nn?
Halafu yaonekana uwezo kwenye hii post ilikuwa na mchechetooo sanaa.

Jamani anatoa image gani kwa umakini wake mhmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm....
Niklishanga alivyolijadili hilo suala as if kuna bonge ya tishiooo
wale wazee ukiwaita tuu ofisini kunywa gahawa watahairisha tuu jazba zao.

Hili fupa la zenj jamani linafanyiwa sanaaaaaa....mpaka utamuuu unaongezekaa
 
yeah ndivyo inavyodhaniwa na wengi. Ila elewa kuwa ili kuonyesha tofauti mjinga mmoja na mwingine ni lazima umteue mjinga kuliko. Yaani aliye mbumbu kuliko wewe,,, hapo watu watasema afadhali ya aliyepita.

hebu nipatie c.v nikupe kazi inayokufaa hapa
 
Hii thread ina kichwa cha habari "Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, MUONGO". Mimi kule kwa thread ya "JK amteua Jaji Kiongozi mpya" nilitumia neno Muongo, Mkuu SMU aliniomba niliombe radhi, SMU upo?, manake limetumika tena.

Ukweli hapa limetumika ndipo ,hivyo kama unakumbuka mkubwa mmoja wa CCM ambae alikuwa ndani ya jeshi la polisi alionekana kwenye luninga za Tv akitangaza kuwa vijana wake wamekamata kontena lililojaa mapanga na visu ambalo lilikuwa ni la Chama cha CUF wameleta ili kueneza silaha hizo kwa wanachama wake tayari kwa mapambano ,nadhani utakumbuka tu au sio ?
Ndio hivi hivi alivyozuga huyu mwengine kuwa Wazee wa Pemba wamejiandaa kulala barabarani na kuzuia msafara wa Bin Kimuni na kujaliza mambo kibao akiwapaka matope WaPemba hao ,jambo ambalo ofisi ya UN imelitolea kauli kuwa si kweli wala hakuna mpango huo ,hapo tu inataka ufahamu kuwa hata UN wana makachero wao na waligundua na mapema hila za Waziri huyo kuwa anaudanganya umma ,na fahamu kuwa baadhi ya watu ni wa kweli kabisa hawasiti kukupa ukweli na ndivyo alivyofanya muwakilishi wa UN hapa Tz,kummulika Waziri kwa kumwambia usitayarishe mamluki mpango huo haupo na kama ukiwepo wewe Waziri ndio umetayarisha ,ndugu sijui kama unafahamu namna ya kupaka matope ,unaweza ukatayarisha watu na kuwavalisha unifomu za watu wengine na kuanzisha fujo na kuonekana kuwa waliofanya fujo ni kundi fulani wakati sio kweli ,hivyo lazima uwe macho na kauli za jamaa hawa ,kama tulivyoona kwenye visu na mapanga ambayo pandikizi la CCM ndani ya jeshi la polisi alifika hadi kuvipaka rangi silaha hizo ziwe na alama ya bendera ya CUF na ndio hivyo pengine alivyotaka kufanya ,huwezi kujua alikuwa na nia gani ya kutangaza ilani ile ambayo ilitisha sana ,wazee wa Pemba wamesema wala hawakuwa na nia hiyo hayo ni yake huyo waziri alietangaza ,sasa kamuulize waziri habari zile alizipata wapi au kwa nini akatunga mawazo yale ?
 
membe anajidanganya kuwa atakuwa rais baada ya kikwete...tanzania iendelee kuwa chini ya wasaniiiiiiiiii.........president in wait bennard membe...teh teh!!
 
Mwiba,
Mimi nilishangaa ni kwa nini waziri aliamua kwenda public na hizo allegations. Hata kama zingekuwa kweli, serikali ina njia nyingi ya kuzima dukuduku hizo za Wapemba bila kwenda public. Hayo matatizo wangeyashugulikia kimya kimya kama alivyofanya mwakilishi wa UN
na hata ingeshindikana basi Wapemba wangeambiwa kuwa polisi haitawapa kibali cha kufanya maandamano. Inanikumbusha yule kijana aliyekuwa anapiga makelele kuashiria mbweha, mbweha, kumbe hamna kitu.

Huo ndio mchezo wa Siasa na lengo hapo ni kuugombanisha upinzani kwa wananchi. Ni wajibu wao wananchi kupembuwa.
 
Je ni yule yule Membe aliyekuja na hoja ua OIC ? Leo kaja na habari za Wapemba ? Hivi hao wapemba wako wangapi ? Je kubeba mabango na kutoa ujumbe ni kuharibu ziara ya mkubwa ? Haki ya kupeleka ujumbe mbona inakataliwa ?
 
Je ni yule yule Membe aliyekuja na hoja ua OIC ? Leo kaja na habari za Wapemba ? Hivi hao wapemba wako wangapi ? Je kubeba mabango na kutoa ujumbe ni kuharibu ziara ya mkubwa ? Haki ya kupeleka ujumbe mbona inakataliwa ?

Ni ubabe na kumalizika na kufikia mwisho wa upeo wa utawala wa CCM kufikiri ,mambo ambayo yanahitajiwa kusemwa na wengine wanajipachika wengine ,ndio maana kila wanapojaribu wanaumbuka,si umeona mwengine , Mkuu wa Nchi Mheshimiwa Jemedari Mkuu wa Majeshi ya Tanzania anakuja na kali ya mwaka ,wananchi wapige kura kuwafichua wauaji maalbino,wanaooua vizere sijui majambazi na mambu kibao ,hivi hawa waliogunduliwa mpaka leo wamewafanya nini ?

Yule jamaa kakamwatwa na mabilioni kibao mpka leo Tanzania haijasema lolote na ushahidi kuwa mali aliyokuwa nayo hakuiwakilisha kakule alikohitajiwa kuzieleza ,amefanywa nini ? Mbona nasikia amepewa kamati aongoze ninachokuwa na wasiwasi hapa ni kuwa hii nchi wanataka kuwafanya wananchi wote ni wajinga ,hakuna jingine ,wanatuona akili zetu ziko chini zaidi ya wao ,jamani akili nywele kila mtu ana zake ,msitake kuwafanya wengine wafanane na ninyi kwa kuwaunga mkono mengine hayaungiki.

Nilijitahidi kumsifu huyu Mkuu wa Nchi na kuona timepata kiongozi kumbe tumepatikana.

Kura yangu sijawahi kuipeleka CCM na ndio kwa mambo haya hawaioni kabisa na wala hawana la kunishawishi.

Upinzani Tanzania tunahitaji Katiba mpya na tume mpya ya uchaguzi ,hakuna cha kungojea ,au maneno ya kila siku ya kusema hii katiba haina kasoro si ya kweli ni kutulazimisha kuwa na kifaa kilichochaa ambacho hakiwezi kutuvukisha kule tunakotaka kuenda.

Siku nikisikia CCM imeanguka katika kuiongoza Tanzania ndio siku nitakayokwenda kukata kadi ya CCM ili niendelee kuwa mpinzani.
 
Back
Top Bottom